Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

Kingine mleta mada umezungumza kitu kama kuna wakati mumeo alikuwa anakataa watoto siyo wake na kwamba wapeleke kwa baba yao,unaposema mlikuwa na migogoro ya hapa na pale yumkini alikuwa anakuhisi kupungukiwa uaminifu?
 
Kwa alichoandika kasema yupo tayari watoto waende kwa Baba wakuitimiza umri sahihi. Sheria inatoa custody ya watoto kwa mama mpaka miaka 7. Baada ya hapo custody unaweza kubaki kwa mama au kwenda kwa baba.
Swala la pili kuhusu kuacha kufanya kazi. Hata Mimi ningependa Mke wangu alee watoto lakini Kuna kitu lazima nikifanye vizuri. Kwanza lazima nihakikishe Nampa fedha ya matumizi binafsi. Anataka kununua pedi, kusuka je ataniomba Kila siku? Mwamba anazingua ukimkataza mke asifanye kazi hakikisha unanunua vitu vya ndani vyote, unaweka akiba ya watoto ikitokea umekufa, na unampa fedha ya matumizi binafsi. Zaidi ya hapo unamnyanyasa.
 
Mimi nakuonya tu ni bora kutumia Busara kuliko kutumia hasira,
1.Vita ni watoto
2.Vita ni uchumi.

Ukisha shinda hii vita itaanzisha vita nyingine ambayo ni kutaka baba watoto wako aanguke kiuchumi.
Una uhakika ulikua muaminifu kwenye ndoa yako?
Ulienda kukaa nje na mumeo kwa muda gani ukapata kazi?

Hilitakughalimu sana mbeleni

Wote kuweni makini KIAPO CHA NDOA kitawatafuna.
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Hii imetokea wapi tena au ni uzi mwingine?
 
Ubinafsi tu wa wanadamu
 
Ukiona mwanaume kafikia hatua hii ya kukuficha mpaka watoto walipo jua mmefikia hatua mbaya, hapa ninaona kati yenu nyote wawili hakuna mtu anayetaka kujishusha nyote mnajiona mna haki sometimes mambo humalizwa kibusara zaidi kwa mustakabali wa watoto najua mpaka kufikia hatua hii mlikosana sana nakushauri yule ni mzazi mwenzako unajua madhaifu yake naye anajua yako unajua jinsi ya kumlegeza jifanye mjinga japo simaanishi mrudiane no weka urafiki na mmeo mjenge kisaikolojia asikuone kama adui yake naamini mambo yatakuwa sawa mkumbushe umuhimu wa kulea watoto mkiwa na maelewano pasipo chuki na uadui
 
Kumbe kuna mtu kakatazwa kufanya kazi??
Ahhh hii sio sawa.
 
Wanawake bwana ,we chunguza fujo nyiingi kwenye ndoa, ni wanawake wakishapata uchumi. 90% hata kama sababu ni mwanaume, ila huwa anakua provoked na mwanamke baada ya kuanza jeuri sababu ya uchumi. Wenzetu hawa ni dhaifu sana before money and wealth. Very very wicked
 
🤣🤣🤣🤣 Ili ukaharibu ndoa yake? Tafuta namna nzuri ya kuonana na watoto! Lakini sio kutaka kujua wanapoishi.
 
Amewachukua watoto wakiwa bado wadogo sana, nadhani umri sahihi ni miaka saba kama sikosei - hapo kisheria utapita.

Kwa mbali naona ndoa inaenda kuvunjika, ila wewe na mwezio hamjajizaa hapa duniani.

Wazazi wako na wazazi wa mmeo wakutane wafanye jambo.​
 
Dada angu olika mbona sijaona tatizo haswa kati Yako na mumeo.
Sali sana, Sali sana nasisitiza Sali sana.
Umesema kweli, huyu dada yetu kuna vitu hajasema. Ila mimi binafsi namshauri afanye sana sala. Vinginevyo washashindwana na mumewe kwaio anatafutwa mshindi😂
 
Kumbe kudharauliwa inauma. Angeacha kumsimanga na kumdharau mkewe hayo yote yasingetokea
Mazungumzo ya upande mmoja, inawezekana kabisa mmiliki wa mfugo akajua tabia zote za mfugo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…