Uchaguzi 2020 Msajili amwandikia barua Maalim Seif akimtaka ajieleze kwanini kapanda jukwaa moja na Tundu Lissu kule Kilimanjaro!

Uchaguzi 2020 Msajili amwandikia barua Maalim Seif akimtaka ajieleze kwanini kapanda jukwaa moja na Tundu Lissu kule Kilimanjaro!

Tatizo tumeshindwa kusimamia sheria kanuni na taratibu tulizojiwekea na wanapenda kuzivunja ni wale tuliowapa dhamana ya kuzisimamia
 
Kwani ni marufuku kwa Mtanzania yeyote kupanda jukwaani na Tundu Lissu?

What kinda fuckery is that?!!

Hao jamaa wa NEC hawana hata busara tu hizi za kawaida?
Hao siyo NEC bali ni msajili wa vyama vya siasa. Hivyo wapinzani wanabanwa kote kote.
 
Katiba ya Tanzania inatoa uhuru

https://www.tanzania.go.tz/egov_uploads/documents/KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA.pdf

Ibara za 18 20 na 21 zinatoa uhuru wa maoni, uhuru wa mtu kushirikiana na wengine na uhuru wa mtu kushiriki shughuli za umma.

Haki ya Uhuru wa Mawazo
Uhuru wa Maoni Sheria ya 1984 Na.15 ib.6

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati. (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine Sheria ya 1984 Na.14 ib.6

20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo. (2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake- (a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya- (i) imani au kundi lolote la dini; (ii) kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia; (iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano; (b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano: (c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa; (d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano; (e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia. (3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika. (4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4

21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa.
umeandika kirefuuuuu umeacha kusoma katiba ya ACT WAZALENDO
1603290739465.png
 
Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT wazalendo maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lisu wa Chadema kumpigia kampeni.

Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.

Maendeleo hayana vyama!
Huyu msajili ana matatizo sana. Ile barua waliomjibu kina Ado Shaibu haikumwingia akilini?
 
Kuna mambo hua yanasikitisha sana...

Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha...

Cc: mahondaw
 
Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT wazalendo maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lisu wa Chadema kumpigia kampeni.

Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.

Maendeleo hayana vyama!
Leo Mrema alikuwa Moshi na alivalia Kofia ya CCM. Tanzania yangu Ehhhh
 
Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT wazalendo maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lisu wa Chadema kumpigia kampeni.

Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.
Na walikuwa wapi kuwaambia CCM wasiingize nchi za nje kwenye siasa za ndani kwenye majukwaa?

1603291817598.png

1603291708768.png
 
Mrema amempa na beberu...lakini yy ataachwa
 
Halafu utaambiwa hiyo msajili eti ni JAJI..! Too pathetic
 
Jemadari Nasoro Mazrui awaapisha Wazanzibari amfurushe Mtalii njaa arudi kwao Kisarawe
 
Msajili wa vyama vya siasa amemtaka mwenyekiti wa ACT wazalendo maalim Seif ajieleze kwanini alisafiri hadi Kilimanjaro na kupanda jukwaa moja na Tundu Lisu wa Chadema kumpigia kampeni.

Kiongozi wa chama Zitto Kabwe amesema wanatarajia na mwenyekiti wa TLP mzee Mrema atajieleza pia.

Maendeleo hayana vyama!
Mavi kabisa
 
Back
Top Bottom