Kiongozi wangu kwa sheria zilizopo ZEC au NEC zikikuondoa katika orodha ya wanaogombea Urais hasa katika kipindi hiki cha lala salama ujue rufaa yako itatolewa maamuzi baada ya Rais mteule kuapishwa na majibu ya rufaa husika unaweza kutabiri mwenyewe yatakuaje. Kitakacho bakia ni kelele za kuonewa kwa muda wote wa miaka mitano ijayo.
Maalim anakubalika kama ambavyo Lissu anakubalika tena siku zenyewe zimebaki chache sana. Kwa maoni yangu hapakua na sababu yoyote ya kufanya wanavyofanya(hasa Maalim Seif) kwani hali hiyo inahatarisha wanaomuwinda wapate uhalali wa kumhujumu kwa kumuondoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais