Msajili wa Vyama vya Siasa: Nitavifuta CHADEMA na CUF

Msajili wa Vyama vya Siasa: Nitavifuta CHADEMA na CUF

hqdefault.jpg

Green Guard Zanzibar ni Imara zaidi ya Chuma.​
images

Hivi hizi picha! Haya si mazoezi ya kivita kabisa?
 
"KAMA katiba zao zinaruhusu wazifanyie marekebisho"...

Ina maana huyu msajili hajawahi kuzisoma hizo katiba. Sasa huwa anaenda ofisini kila siku asubuhi hadi jioni kufanya nini!
Tena ni mtaalamu wa sheria,too low for him.
 
Matamko mengine yanatakiwa yaangalie Wakati wake, msije mkatuharibia taifa. TEAM WAZALENDO
 
Msajili wa Vyama vya Siasa, amedai wote watakao kiuka kuvunja vikundi binafsi vya ulinzi vya vyama hivo atavifuta.

Amedai kama Katiba zao zinatambua jambo hilo walifanyie mabadiliko haraka.

Tamko hill limetolewa kwa ushirikiano wa IGP Mangu kwa niaba ya Jeshi la polisi na ofisi ya msajili.


My Take.

Niwazi kwa ubishi wa CHADEMA bila shaka kitafutwa katika medani za siasa.

Chanzo. RFA magazeti

Ajaribu kufuta halafu aone cha moto. Aache kutishia nyau kwa maslahi ya ccm. Naamshauri avifute sasa hivi wala asichelewe.
Huyu si ndiye aliyesema atakifuta Chadema kikimsimamisha Mbowe kugombea uenyekiti kwa vile katiba ya Chadema mwisho vipindi viwili? Mbona Chadema walikaidi agizo lake na Mbowe ndiye mwenyekiti na mutungi yuko kimya?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
msajili amechewa sasa muda wote alikuwa anasubiri nini, mpaka watu wanatekwa na kuchanwa migongo, vyama vina mpaka vifaa vya kutesa bora vifutwe
 
Hata mwenzake aliyestaafu TENDWA alianza na mikwara kama hii mpaka amestaafu hajafanikiwa kufanya chochote labda huyu hujui majukumu ya kazi yake chama ambacho angetakiwa kukufuta haraka sana ni ccm.
 
Kikubwa imani ya mabadiliko ya uongozi , ccm hamna demokrasia kwa nini mnaruhusu vyama vingi huku mkivibana visipate nafasi ya kuongoza ? Chadema nyie komaeni Mungu yu nasi siku moja tutafanikiwa kuingia Ikulu!! Umoja wetu do mafanikio yetu kuingia ikulu na dola
 
Mmmmh, bora asingesema haya maneno, aliyemweka hapo ana hivyo vikundi na kamwe hawezi kuvifuta, mchezo uendelee
 
Chadema kilitakiwa kufutwa muda mrefu sana, naona msajili kachelewa kukifuta, hawa watu wanapiga biashara tu hawana nia ya dhati kuwakomboa wananchi, pale ni ruzuku, umaarufu basi.
 
...Inasemekana somo la kusoma na kuandika alipata F, hivyo yupo yupo tu. Kusoma nehi.

"KAMA katiba zao zinaruhusu wazifanyie marekebisho"...

Ina maana huyu msajili hajawahi kuzisoma hizo katiba. Sasa huwa anaenda ofisini kila siku asubuhi hadi jioni kufanya nini!
 
IGP Mangu na Msajili Judge Mutungi, kwani hii dhana ya ulinzi shirikishi imeondoka baada ya IGP mwema kustaafu au haihusiani na vyama vya siasa? Kama elimu imekuwa ikitolewa kwa kiasi kikubwa raia washiriki katika ulinzi na usalama wa wao wenyewe na mali zao kwa sababu jeshi la polisi halina uwezo wa kuwa na idadi ya askari wa kuifanya kazi hiyo kwa ukamilifu, nini kinachokuja kwa tamko lao hili kuwa USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO NI KAZI YA POLISI na raia (kupitia vyama vya siasa) wasihusike katika ulinzi?

Je! Wanatuambiaje au wanatoa ufafanuzi gani juu ya ULINZI NA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO kwa kuangalia haya yafuatayo:- 1). POLISI wenyewe, 2). WANAMGAMBO, 3). ASKARI WA JIJI, 4). PRIVATE SECURITY COMPANIES (Hapa ni utitiri wa makampuni na Polisi ndiyo watoa vibali). 5). GREEN GUARDS, 6). RED BRIGADE, 7). BLUE GUARDS, 8). "ZAMBARAU" GUARDS, 9). SUNGU SUNGU, 10). POLISI JAMII, 11). NEIGHBOUR HOOD WATCH, 12). KOROKORONI, etc. etc.

Inawezekana kutofautisha maana ya USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO na kazi inayofanywa na vikundi, majeshi au watajwa wengine hapo juu?

Kutakuwa na kuchanganyikiwa sana kwa watu wengi endapo msajili na IGP wataanza kujaribu kusema nani anahusika na ulinzi au usalama hapo.

WATAFAKARI KABLA YA KUCHUKUA HATUA kwa kufuata maelekezo ya kupotosha ya walioshika hatamu kwa sasa.
 
Au afute hawa sijui tuwahite chipkuzi waliokomaa na kila mwaka wanakimbiza mwenge, na kwa sababu mwenge ni wa chipukuzi na umoja wa Vijana wa CCM na makombati yao basi na mwenge aufute
Aanze na ccm wafute chipukizi na wengine watafuata hiyo ni njia ya kuzuiya uhuru wa vyama kulinda wizi wa kura na kwanni hili limetangazwa muda mfupi tu kuelekea uchaguzi?tunamashaka sana na msajili na mangu wana ajenda ya siri ambayo ipo wazi kwamba wana njama za kuibeba ccm.
 
Apo umegusa pabaya. miaka yote hii ulikua kipofu? au kwa kua unaona red brigade ipo juu mno
 
Hapa Watu Makini Hupita Tu Hawezi Toa Maoni Kwenye Fikira Za Kijinga Namna Hii
 
Ukanjanja haupo mahali pamoja tu Tz, Ukanjanja ni kufanya kitu tofauti na ujuavyo na utaalam wako wote, ukaamua kupindisha ili ufanikishe malengo tofauti.
Sasa Jaji wetu Mutungi na Kamanda wetu IGP Mangu mmepotea njia. Mtz wa leo hana woga tena. Kungekuwa na woga, mateso waliyopata kina; Kubenea, ulimboka na wengineo wengi kungeshaleta hofu kuu ndani ya watz lakin mhhhh.
Mabomu yaliyorushwa makanisani na mikutanoni yangewafanya watu waogope mikutano ya hadhara. Lakini mhhh. Watu wanajilipia nauli zao na kuhudhuria mpaka chepe chepe!
Sijui una maana gani
 
Back
Top Bottom