Msanii Ali Kiba azindua Redio yake, inaitwa Crown FM

Msanii Ali Kiba azindua Redio yake, inaitwa Crown FM

Staa wa muziki wa Bongo Fleva @officialalikiba amezindua radio yake mpya inayoitwa CROWN FM ambayo inapatikana 92.1 Fm.

Alikiba ameeleza sababu za kuzindua Radio kuwa ni njia pekee iliyoinua career yake na watu kumfahamu kupitia Radio.

Baada ya kuwa msanii kwa takribani miaka 20 sasa anakuwa miongoni mwa Wasanii na watu wanaomiliki Radio.
View attachment 2929868
Hongera sana kwake! Lkn Mimi naona hii tabia ya wasanii kuigana igana Kila kitu anachoqnzisha mwenzio ni ufinyu wa mawazo na tatizo hili lipo kwa Watanzania wengi sana.

Wasione mtu kafungua kibiashara flani mtaani..! Kesho utakuta Kila mtu mtaani anafanya biashara hiyo hiyo mpaka unajiuliza inamaana hawaoni frusa zingine???

Sio lazima wote tulime! Mwenzio akilima wewe wewe anzisha kampuni ya kununua mazao!

Mwenzio akifungua salon ya kiume wewe fungua ya kike that thing!!!
Haya mambo ya kuigana igana Mimi naonaga kama ni ufinyu wa mawazo ama kukosa jicho la kuchungulia frusa zingine.
 
Labda sababu Kings FM ipo Iringa. Ila ingekuwa ni mimi Kiba na jambo langu (achana na la Kusaga) ningeongea na hiyo mmiliki wa hiyo redio ya Iringa abadili jina.

Kings FM ingembeba sana Kiba. Hiyo Crown FM haikaikai sana kimatamshi, labda vile sijaizoea
Mi naona crown FM nzuri kibiashara, why menigi haku iita itv mengi channel
 
Vyovyote ilivyo hata kama ana Share ya 10%.

Mbona sisi Tanzania nzima tuna Share 16%tu na tunajidai tuna Migodi ya Dhahabu.

Naona shida kwenye hayo maandishi "azindua Radio yake" especially kama yeye sio main share holder kama mwenzake yule wa Tandale...

Maana hawa madogo wana majina ambayo mwisho wa siku yanawanufaisha wengine...
 
Bro kwani kuwa business partner sio sehemu ya umiliki??.

Rihanna mwenyewe ni ambassador wa Fenty beauty, ila pale ana share kiasi chake.

Nimetaka kujua tu, kwa sababu title imeandika kwamba "kazindua redio yake", sijajua kama haya maneno wewe umeyaelewaje kama tukiyageuza yawe katika %
 
Labda sababu Kings FM ipo Iringa. Ila ingekuwa ni mimi Kiba na jambo langu (achana na la Kusaga) ningeongea na hiyo mmiliki wa hiyo redio ya Iringa abadili jina.

Kings FM ingembeba sana Kiba. Hiyo Crown FM haikaikai sana kimatamshi, labda vile sijaizoea
Yeye angeinunua hiyo Kings akafungua Headquarters hapa Dar kisha huyo wa Iringa ndo akafungua mpya kwa jina jingine.
 
Back
Top Bottom