TANZIA Msanii Costa Titch afariki dunia baada ya kudondoka stejini

TANZIA Msanii Costa Titch afariki dunia baada ya kudondoka stejini

View attachment 2546922

Taarifa zilizothibitishwa zimeripoti kuwa msanii Costa Tich amefariki dunia.

Msanii huyo alikuwa akifanya onyesho stejini, ndipo alipo anguka ghafla na kukumbwa na umauti.:👉

👉 Taarifa za kina zaidi, kuhusiana na chanzo Cha kifo bado hazijajulikana. Zaidi ya kusemekana ni ajali tu.

Miongoni mwa kazi zake zilizo vuma ni goat, super star, Mr big flexa, ma gang na nyinginezo.

Mwenyezi MUNGU, aipumzishe roho ya marehemu, mahali pema🙏🙏.

View attachment 2546885

View attachment 2546923
Too young to die
 
Vijana wanaondoka wadogo sana wengine fame ndiyo chanzo, sasa sijajua kama alitubu alivyo mpigia debe shetwan akiwa na mbossonyo au ndiyo shettwaa atakuwa mwenyeji wake kwenye makao mapya.
Lyrics zake Costa Titch hizi hapa

Oooh Monday to Sunday
Ooh sikalamanje I need a trip Zanzibar
Need a rock ??????????
Coz I don’t want no stress

So lets go to party
Mtoto wangu let’s go to party
So lets go to party
Kam hakuna wasi wasi aiya iyaaa

Wapi alipompigia debe Shetani mkuu?
 
Vizuri,asa hapo hukugoma ww bado roho wa Mungu hajaka kwako bado ana mashaka na ww,japokuwa mistari ya Bible unaitahamu.Siku akiona unafaa atakuongoza na hamna utakachopinga.Usisahau kunitag siku ukiwa mtumishi 😆😆
Muonekano wangu Yes naweza kua pastor Ila sihitaji kua pastor wa mchongo, na sina MPANGO huo nitabaki kua mtazamaji tu yaan mtu anakushawishi kwamba wewe una kitu ndani na ukichanganya na muonekano unafaa kabisa kua pastor aisee Mimi niwe pastor?
 
Kuna jamaa kanichek whatsup group mda huu huu ila bado siamini naona uongo hapa anadai jamaa alikua na uzito uliopitiliza.Ndio nasikilizia na wengine nihakikishe zaidi.
Yawezekana
Kama kazaliwa 95, na alivyokuwa kibonge utadhani ni kibaba cha 43yrs.
Duh
Sikuwahi jua kama anaweza kuwa under 30 aisee
 
"popote mlipo yatakufikeni mauti ijapokuwa mtakuwa katika ngome zilizo madhubuti...."
Qur'an 4:78

Eeh itakuwaje unarudi kwa muumba wako una nywele za kijani mchanganyiko pink, umejichora tatoo mwili mzima, umefikwa na umauti stejini ukifanya show isiyoeleweka hata inahusu nini, hivi ndugu zangu namna hii ndio mwisho wa mwanadamu unapaswa kuwa?.

إنا لله وإنا إليه راجعون
 
Jamaa hakua sawa pale on stage sijui kwanini hawakugundua kabla?, Yaan kamdondokea hadi yule body guard mara ya kwanza akamuinua hajagundua tu kwamba jamaa hayupo sawa...
Mtatafuta tu cha kusingizia huyo hapo alidondoka chini ni death experience ilimuanza akajaribu kunyanyuka akanyoosha tu mkono juu akamalizikia, kama ni moshi wako nao hapo stejini miaka yote kwani mkuu ni moshi wa mkaa huo mpaka akose hewa.

Na hapo alikuwa anapepesuka kuelekea huko kwenye moshi ni kitendo cha sekunde kadhaa tu wala hakukuwa na dalili yeyote kabla.
 
Back
Top Bottom