Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Je, maamuzi haya magumu yanatuma ujumbe gani kwa wazazi wa Tanzania?
Kuwa mtoto wa nyota wa sinema wa kimataifa kama Jackie Chan ni dhahiri kwamba huja na marupurupu mengi na faida. Mtoto wa Jackie Chan, aliyekuwa na umri wa miaka 33 kwa wakati ule anayeitwa Jaycee, aliishi maisha yaliyojaa nyumba za kupendeza, likizo za kifahari, magari ya bei aghali, elimu bora na mengine mengi.
Jaycee hata aliweza kuzindua kazi yake mwenyewe ya kuimba na maigizo kupitia umaarufu wa baba yake. Lakini kuna jambo moja muhimu ambalo Jaycee hatapata kutoka kwa baba yake: Mamia ya mamilioni ya dola za urithi. Nyota wa movie maarufu ya Rush Hour tayari ameamua kutoa nusu ya pesa zake kwa taasisi za hisani na watoto yatima pindi atakapokufa.
Alipokuwa akiongea kwenye hafla ya tuzo miaka kadhaa iliyopita alisema kuwa hakuwa na mpango wa kumwachia mtoto wake Jaycee mamilioni ya dola ambayo ameyoyapata wakati wa kipindi chote cha kazi yake ya kucheza filamu. 'Kama ana uwezo, anaweza kupata pesa zake mwenyewe. Ikiwa hana uwezo wa kutengeneza pesa zake mwenyewe, basi atakuwa akipoteza pesa zangu tu hata nikimuachia, 'watu walimnukuu Chan akisema.
Chan pia alifichua siri yake ya muda mrefu ya kuwa alitamani amuingize mwanae Jaycee ajiunge na jeshi akiwa mdogo kama njia ya 'kumpima tabia yake'. miaka michache iliyopita uvumi ulisambaa ya kwamba Chan, aliyekuwa na miaka 56, alikuwa amekufa kwa ugonjwa wa moyo na salamu za pole 'RIP Jackie Chan' zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kama vile Twitter.
Chan alikuwa mwepesi wa kutupilia mbali ripoti hizo na kuchapisha taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwahakikishia mashabiki wake kuwa bado yuko hai na yuko vizuri. Akizungumzia uvumi huo, Chan alisema: 'Sijafa, ingawa niko busy sana ili niweze kufanya kazi hadi kufa. 'Natamani media ikiripoti zaidi juu ya huduma za umma na habari za huduma za kijamii badala ya kejeli kwa maana ni za thamani kubwa zaidi.
'Hata Will Smith alidanganywa na kuomboleza kifo changu kwenye mtandao wa Tweeter. Chan kwa wakati ule alikuwa anafanya kazi katika mashirika ya kusaidia kutoa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi la Japan na Tsunami.
Je, maamuzi magumu kama haya yanatuma ujumbe gani kwa wazazi waishio katika nchi hizi za Afrika Tanzania?
Mzazi tafadhali sana usipite bila kusema neno lolote.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.