Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha Msanii wa BongoFleva, Emanuel Elibariki, maarufu kama 'Nay wa Mitego' kufunguliwa madai ya Uchochezi, Jamii Forums imeongea na Wakili wake, Jebra Kambole ambaye amethibitisha kuwa Mteja wake alipata wito wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati, DSM kwa tuhuma za uchochezi kupitia baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa 'Amkeni'

Amesema mteja wake alitoa maelezo yake na kukanusha tuhuma hizo akieleza kuwa nia ya Mashairi yale ni kuonesha upungufu kwenye Utawala kwa nia ya kurekebisha, ambapo alipewa masharti ya dhamana, kisha akaambiwa kama kutakuwa na hatua za kisheria atajulishwa

Kuhusu Madai ya Nay kuzuiwa na BASATA kufanya matamasha, amesema hakuna taarifa rasmi kutoka BASATA, japokuwa BASATA walikuwa wakiwasiliana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa ambao ndio walimnyima Mteja wake vibali. Amesema BASATA imempa Nay wito wa kwenda Ofisini kwao bila Mwanasheria Septemba 8, 2023
 
Hapa ndipo wasomi tunapopata thamani yetu.

Political tolerance ni ngumu sana hasa ktk nchi za Kiafrika.

Sasa twende tu maneno ya vijiweni "Nchi imefunguliwa/imefungukaa" maana Jpm aliifunga sana
 
Kwahiyo Wasanii wetu wanatakiwa kuimba Mashairi na Kaswida za kumsifu mtukufu Mwenyekiti wa CCM?

Hizi siasa za kulamba makalio (ashakum si matusi) nilidhani zimeshazikwa Chato?
 
Msanii Ney wa Mitego anahojiwa na jeshi la polisi Dar es Salaam kutokana na wimbo wake “AMKENI”

Bado najiuliza ni nani anamshauri Rais kutumia hii style kukabiliana na wote ambao hawamsifii?
Rais ni kweli umechangua njia hii? Kweli njia nii utaiweza? Utakamata na kuhoji wa ngapi...
Mama Samia kama mama Samia naamini ana nia mzuri sana na wananchi wa Tanzania.

Tatizo lipo kwenye washauri wake wa karibu hasa upande wa siasa.

Washauri wake wengi wanatoka mlengo wa sukuma gang ambao nia yao ni kumharibia mama
 
Serikali ni dude kuuuubwa

inaweza ikashughulikia Umeme na mafuta na huku ikishusha Wenge la wenye vihele hele bila ya muingiliano
Sukuma gang mnampoteza sana
 
Back
Top Bottom