Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Mama anaupigwa mwingi, kafungulia uhuru wa kujieleza, mama anapenda kukosolewa, yaani ilikuwa nani kama mama! 🤣 🤣 🤣 🤣 Watanzania upenda kusifia mambo bila tafakuri ya kina!
 
Serikali ni dude kuuuubwa

inaweza ikashughulikia Umeme na mafuta na huku ikishusha Wenge la wenye vihele hele bila ya muingiliano
Hilo dude kubwa lililoshindwa kudhibiti wizi wa bandarini hadi kuamua kumpa DP World bandari, hilo dude litakuwa ni kubwa jinga.
 
Kitu simple kama KATIBA MPYA tu ambayo ni mali yetu sisi Wananchi hawataki kutupa.

Wanajifanya kutuhadaa na mambo ya Kitoto.
Katiba mpya ngumu kuipata hadi watu flani wasiwepo bila hivyo tutaimba sana.. katiba mpya kuna watu wameikalia
 
Amemchochea nani? Sisi wananchibona hatujachocheka?
 
Mama anaupigwa mwingi, kafungulia uhuru wa kujieleza, mama anapenda kukosolewa, yaani ilikuwa nani kama mama! 🤣 🤣 🤣 🤣 Watanzania upenda kusifia mambo bila tafakuri ya kina!
Mama anaweza kuwa na lengo zuri kwa Watu wake, lakini amezungukwa na Machawa Makupe na kila aina ya Nasty Bugs
 
...Kama upo upande wa ney nipe likee
 
Hivi ukiwa na kazi ambayo unaona kabisa huiwezi, si ukijiuzuru utaonekana wa maana zaidi na kuheshimika? Sielewi kwa nini huyu mama hadi leo hajakubali kuwa urais si fani yake?
 
Sio muda anatimkia Marekani au Canada akiwa kama mkimbizi wa siasa.
 
Hebu nifafanulie zaidi Mkuu?
Watu ambao wamejilimbikizia mali kwa mda mrefu sana katika hii nchi, kwa njia ambazo sio sawa, wamekita mizizi mirefu sana .. usifikiri itakuwa rahisi wao waruhusu katiba mpya wakati wanajua itawang'anata
 
Wanaitwa wazee wa kuwabambika kesi raia

Lakin mwisho wao uko karibu sana kuliko ilivyokuwa awali
 
Watu walishasahau hiyo nyimbo … mmeamua kurudisha tena … mi nahisi MAMA SAMIA anachafuliwa kwa makusudi
 
Msanii Nay wa Mitego anahojiwa na jeshi la polisi Dar es Salaam kutokana na wimbo wake “AMKENI”

Bado najiuliza ni nani anamshauri Rais kutumia hii style kukabiliana na wote ambao hawamsifii?
Rais ni kweli umechangua njia hii? Kweli njia nii utaiweza? Utakamata na kuhoji wa ngapi?

Rais mbona kuna mambo mengi ya kushughulika nayo kama ukosefu wa Umeme,mafuta na Dolla?

----
Msanii Emmanuel Elibariki maarufu ‘Nay wa Mitego’ ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi kupitia wimbo wake wa ‘Amkeni’.

Akiambatana na wakili wake Jebra Kambone, Ney wa Mitego amesema ameachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano yaliyochukua takribani saa tatu na kukamilisha masharti aliyopewa.

Ney wa Mitego alifika katika Kituo cha Polisi Central, Dar es Salaam baada ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano.

Hata hivyo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema halihusiki na kuitwa kwake polisi licha ya kwamba wamemuita mara kadhaa kufika katika ofisi hizo lakini hakuitikia wito huo.

“Tumetoa wito mara mbili kwa ajili ya maadili ya kawaida tu lakini kwa bahati mbaya sana hakuwahi kutokea, na jana tumeandika wito mwingine tukimtaka aje Ijumaa saa 4 asubuhi hajatujibu, sijui kama atakuja ama hatokuja.

Mambo ya polisi nafikiri hayo ni masuala ya kijinai, sisi tunahusiana na masuala ya Sanaa tu wala hatuna jukumu la kwenda kumshitaki,” amesema Mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha.

Chanzo: Swahili Times
Hao polisi Huwa hawajifunzi? Mbona wanapenda kujiabisha kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom