Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi

Mbona ni kibao muruwa kabisa na chenye maudhui ya kuwakumbusha walio kwenye Power.

Amenikosha sana pale kwenye ripoti ya CAG Kichere kudharauliwa
Ccm daima hawataki kukosolewa
 
Tusipokua makini masultani wa Zanzibar watarudi kututawala watanganyika. Na hii itakua kwa upuuzi wetu watanganyika wenyewe kwa kukamatana, kuhojiana na kufungana wenyewe kwa wenyewe kwa maslahi wakati mwingine ata wa watu ambao si watanganyika.
 
Kama Katiba itakuwa ni hii hii kama ilivyo sasa of course hata wao watafanya hivyo hivyo !!
Hata ikitengenezwa katiba nyingine, chama tawala huwa kinatabia ya kujijenga zaidi na kuwanyamazisha wote wanaokosoa. Hiyo hata wewe ungekuwa Rais lazma utengeneze mazingira ya kuendelea kusalia madarakani

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Msanii Ney wa Mitego anahojiwa na jeshi la polisi Dar es Salaam kutokana na wimbo wake “AMKENI”

Bado najiuliza ni nani anamshauri Rais kutumia hii style kukabiliana na wote ambao hawamsifii?
Rais ni kweli umechangua njia hii? Kweli njia nii utaiweza? Utakamata na kuhoji wa ngapi?

Rais mbona kuna mambo mengi ya kushughulika nayo kama ukosefu wa Umeme,mafuta na Dolla?

----
Msanii Emmanuel Elibariki maarufu ‘Nay wa Mitego’ ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi kupitia wimbo wake wa ‘Amkeni’.

Akiambatana na wakili wake Jebra Kambone, Ney wa Mitego amesema ameachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano yaliyochukua takribani saa tatu na kukamilisha masharti aliyopewa.

Ney wa Mitego alifika katika Kituo cha Polisi Central, Dar es Salaam baada ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano.

Hata hivyo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema halihusiki na kuitwa kwake polisi licha ya kwamba wamemuita mara kadhaa kufika katika ofisi hizo lakini hakuitikia wito huo.

“Tumetoa wito mara mbili kwa ajili ya maadili ya kawaida tu lakini kwa bahati mbaya sana hakuwahi kutokea, na jana tumeandika wito mwingine tukimtaka aje Ijumaa saa 4 asubuhi hajatujibu, sijui kama atakuja ama hatokuja.

Mambo ya polisi nafikiri hayo ni masuala ya kijinai, sisi tunahusiana na masuala ya Sanaa tu wala hatuna jukumu la kwenda kumshitaki,” amesema Mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha.

Chanzo: Swahili Times
Sa100 kanyweshwa kvant ya madaraka inampelekesha
 
Je jamii yetu haitakiwi kufikiri tena bali kusubiri kuwa watu hamnazo

Ney Wa Mitego aachiliwa kwa dhamana ya polisi

View: https://m.youtube.com/watch?v=_zYyCurieMg
Ney Wa Mitego akiwa kituoni Polisi imembidi kuwasomea mistari ya wimbo 'ulioukera' mamlaka waliowasilisha malalamiko Polisi ili waelewe kama msanii maneno yale ya ajira kukosekana, wizi wa mali za umma n.k ktk wimbo wake alimaanisha nini .

Mwisho apewa dhamana wakati mamlaka zinazohusika zikiendelea kutafakari
 

 
Back
Top Bottom