Baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha Msanii wa BongoFleva, Emanuel Elibariki, maarufu kama 'Nay wa Mitego' kufunguliwa madai ya Uchochezi, Jamii Forums imeongea na Wakili wake, Jebra Kambole ambaye amethibitisha kuwa Mteja wake alipata wito wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati, DSM kwa tuhuma za uchochezi kupitia baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa 'Amkeni'
Amesema mteja wake alitoa maelezo yake na kukanusha tuhuma hizo akieleza kuwa nia ya Mashairi yale ni kuonesha upungufu kwenye Utawala kwa nia ya kurekebisha, ambapo alipewa masharti ya dhamana, kisha akaambiwa kama kutakuwa na hatua za kisheria atajulishwa
Kuhusu Madai ya Nay kuzuiwa na BASATA kufanya matamasha, amesema hakuna taarifa rasmi kutoka BASATA, japokuwa BASATA walikuwa wakiwasiliana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa ambao ndio walimnyima Mteja wake vibali. Amesema BASATA imempa Nay wito wa kwenda Ofisini kwao bila Mwanasheria Septemba 8, 2023