TANZIA Msanii wa Bongo Flava, Haitham Kim afariki dunia

TANZIA Msanii wa Bongo Flava, Haitham Kim afariki dunia

[emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji125][emoji125]
chrismauki_-20230811-0001.jpg
 
Sina muda wa kujibishana au kutukanana na watu wajinga kama wewe. Hunijui sikujui. Kila mmoja hapa ana uhuru wa kusema anachotaka, frustration zako za maisha zisikusababishe kuvunjia heshima watu usiowajua. Kuwa mstaarabu. Kama nilivyosema mwanzo, sina muda wa kupoteza na watuu kama wewe, so kwa upande wangu haya maongezi na wewe yamefikia tamati sita respond lolote usemalo.
Sio muda tu, hata akili hauna. Mtu mzima mwenye akili timamu hawezi kuja hadharani na kumdhihaki marehemu.
 
Ila hizi shisha zinamaliza vijana🙆🙆🙆
R.I.P love

Mwimbaji wa Bongofleva na mwanachama wa JamiiForums, Haitham Kim amefariki dunia hospitali ya Temeke alipokuwa anapatiwa matibabu. Meneja wake amethibitisha.

Hivi karibuni Wasanii na Wadau wengine walianzisha kampeni ya kusaidia kuchangisha pesa kwa ajili ya matibabu yake.

Bryson ambaye ni Mume wa Marehemu alisema hali ya Haitham ilibadilika ghafla siku saba zilizopita akisumbuliwa na upumuaji ambapo ilianza kama homa ya kawaida lakini baadaye akawa anakosa pumzi hadi kupelekea kuwekewa mashine na kuchomwa sindano za kila siku zilizogharimu shilingi laki 7 kwa siku.
 
Matibabu ni zaidi ya Starehe mkuu, usiseme hivyo kabisa. Kumbuka kwenye Starehe unatumia wakati huo huo unaingiza. Unapopata maradhi huingizi kitu bali unatoa tu.
Hata wewe ukiumwa kufikia mwezi 1 tu maisha yako yanabadilika.

Tumemuona hapa Prof Jay, kama sio huruma ya Mama Samia ilikuwa anarudisha jezi mapema sana, alikosa pesa za matibabu ya uhakika na watu walichanga lkn mpka pale Rais alipotoa tangazo la kumgharamikia.

Ugonjwa sio starehe ndugu yangu. Usitukane watu wala kukashifu kisa amefariki na hakuwa na hela za matibabu, hadi anapatwa na umauti unajua alitumia kiasi gani kwa matibabu achilia mbali huduma zingine muhimu?

Tuache Dharau, sisi ni Binadamu tu. Pumzi yako isikufanye kuwaona waliotangulia mbele za haki kama wazembe.
Prof alichangiwa zaidi ya 50m ya kwenda india au utakua ulikua paje hukujua
 
Back
Top Bottom