TANZIA Msanii wa HipHop SALU T afariki dunia

TANZIA Msanii wa HipHop SALU T afariki dunia

Nasikia alikuwa ni Shabiki mkubwa sana wa Yanga SC hivyo huenda mambo yakawa yameshatiki kwa Babu.

Simba SC Kesho mkipona sijui kwani nasikia tena kuna Mchezaji wao Kafiwa na Baba yake Mzazi.

Shikamooni Yanga SC na huyo Babu.
FB_IMG_1681547407041.jpg
 
Nasikia alikuwa ni Shabiki mkubwa sana wa Yanga SC hivyo huenda mambo yakawa yameshatiki kwa Babu.

Simba SC Kesho mkipona sijui kwani nasikia tena kuna Mchezaji wao Kafiwa na Baba yake Mzazi.

Shikamooni Yanga SC na huyo Babu.
We ng'ombe inatakiwa upelekwe milembe Dodoma maana kichwani sizani kama ubongo wako unafanya kazi vizuri..
 
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Salutaba Mwakimwagile maarufu kama Salu T amefariki dunia jijini Mbeya leo tarehe 15 Aprili 2023. Msanii huyo amefariki akiwa anaendelea kupewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Akitoa taarifa ya awali, Msanii mwingine wa HipHop, Taikun Ally maarufu kama Mchizi Mox ameeleza kuwa jumanne tarehe 12 Aprili 2023, Salu T akiwa mkoani Mbeya katika harakati zake za maisha, alipata ajali ya gari iliyomsababishia majeruhi na maumivu ya mgongo. Imeelezwa kuwa hali ya Salu T ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili lakini hali yake haikuruhusu kusafiri na hivyo aliendelea kubaki hospitali ya Rufaa Mbeya mpaka umauti ulipomkuta.


Salu T amewahi kutamba na ngoma kama Chunga Sana aliomshirikisha msanii AY (2006) na kutayarishwa na Producer Lindu.


na ngoma nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na album iitwayo HAZINA.


Mchizi Mox ameeleza kuwa msiba wa Salu T upo nyumbani kwao marehemu mitaa ya Round about ya Mbuyuni, Kinyerezi Dar es Salaam na mazishi yanatajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 17 Aprili 2023 jijini Dar es Salaam.

Pole kwa familia ya Salu T na wanaHipHop wote.

Mungu ailaze pema roho ya Salu T.
View attachment 2588702View attachment 2588703
View attachment 2588709
Siku moja nilienda Micassa lounge Pale ubungo kushudia freestyle battle. Nakumbuka kulikua na kipengele cha "michano" hapo emcee unapewa beat unaanza kuchana. Huyu jamaa alikiwasha Sana.
Nakumbuka Slogan ndo alikua anasimamia shoo akasema Salu T ndo kamfundisha Nikki mbishi Ile staili yake ya uandishi na kifloo... Da nilifurahi Sana maana binafsi bongo nzima hakuna MC wa hip-hop nayemkubali Kwa rap style Kali kuliko Nikki Mbishi...

R.I.P Salu T
 
R.I.P Salutaba A.K.A Salu T, your legacy lives on, binafsi, Ngoma zako za Sikio la kufa, Uzoefu, Chunga Sana zitaishi katika kichwa changu mpaka Mauti yatakaponifika. Mungu akusamehe makosa yako uwe katika waliosalimika na gadhabu zake, Aamin.
 
Watch your back young man! Wenye Jamii Forums yao wakikuotea na huku, sijui utakimbilia wapi tena.
Sijui ni kwanini Mimi, Wewe na Wengine tunamchukia kweli hapa JamiiForums ila Kutwa hatuachi Kumfuatilia, Kumjadili na Kumpaisha Kiumaarufu bila ya Sisi kujua.
 
Back
Top Bottom