Kwa hiyo kumbe hamas watashinda vita na Hezbollah pia?
Ni kheri kuangalia uhalisia wa mambo bila kushabikia upande wowote. Ukweli ni kwamba;
HAMAS kwa sasa hivi hali ni mbaya mno: kivipi?👇👇
1. Wanakabiliwa njaa kali kwani chakula cha msaada ni kidogo na hakifiki kwa muda stahiki na upatikanaji wa maji ni shida kubwa mno.Watu wanakunywa maji taka alimradi waweze kuishi.
2. Bado wanaandamwa na vita ardhini na angani na vyombo vya dola vinawanyamazisha kwa nguvu wale Raia wanaoonekana kuwa wapinzani wa HAMAS na ushahidi upo.
3. Kuna mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza na mahospitali mengi hayafanyi kazi au yamebomolewa na wahudumu kujeruhiwa/kuuawa.
4. Usambazaji au upatikanaji wa silaha umedhoofika sana kutokana na kulipuliwa kwa kiwanda cha kutengeneza makombora/maroketi huko Iran na Kivuko cha barabara kati ya Lebanon na Syria kimeharibiwa- hapapitiki tena ili ku-smuggle silaha ziweze kuwafikia huko Gaza.
Hezbollah anakabiliwa na:
1. Mapambano ya kivita esp. uvunjwaji wa majumba na miundo mbinu ya kijamii inaharibiwa kila siku na ndege za Israel na Hezbollah hana uwezo wa kuzuia na ndo mana IDF inatoa amri ya kuondoka/kuhama haraka kwenye eneo fulani na ndani ya muda mfupi tuu kitu kinatua na majumba yanasambaratishwa.
2. Raia wanahama-hama hovyo kwa amri ya IDF (
evacuation notice) yan wamegeuzwa ni wakimbizi ndani ya nchi yao na hatujasikia hata mara moja kwamba Hezbollah imewasaidia kwa namna yoyote ile.
3. Upatikanaji wa silaha -makombora , maroketi umetatizika kutokana na kulipuliwa kwa kiwanda cha kutengeneza silaha hizo huko Iran majuzi hapo.
4. Misaada ya hali na mali (mafunzo na silaha) imedorora kwani mfadhili mkuu
Iran naye anaandamwa na vitisho au "
Piga nikupige" baina yake na Israel, halafu Iran pia amezidisha (imepanua wigo) Ufadhili kwa makundi mengi mengine ya kigaidi huko Syria, Iraq, Yemen n.k. kiasi kwamba ule mgawo kwa kila kikundi Unapungua.
Kwa wote HAMAS na Hezbollah:
D.Trump kuingia madarakani Hakukuwafurahisha HAMAS au Hezbollah kwani huyo mwamba historia yake na chama chake kuhusiana na mambo ya ugaidi inafahamika na tena kuna madai kwamba Iran ilifadhili lile jaribio la kumuua Trump kwa risasi wakati wa kampeni zake kuwania urais.
Samahani ndg. zangu naomba radhi nimeandika gazeti .