Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

MKUU KAMA KUNA KITU CCM WALIJIPANGA BASI NI JESHI , HUHITAJI DARUBINI KUONA KUWA JESHI LINALOITWA LA WANAWANCHI NI JESHI LA CCM, ANGALIA WAKUU WA MIKOA, WILAYA, MABALOZI, NK
USITARAJIE KIKINUKA KUWA ETI JESHI HILO LITAKUWA UPANDE WA MLALA HOI, LITAFUATA MASLAHI YAO AMBAYO YAKO CCM, HIVI UNAWEZA TOFAUTISHA RANGI YA MAZIWA NA TUWI LA NAZI?
 
Ila kama ndie yeye vizuri sana jamaa ni kichwa sana huyu nimewahi kukutana nae na kumsikiliza nikatamani siku moja aje awe mtu mkubwa sana nchi hii.
 
It was clearly stated kuwa hakuna kufanya kazi mbili. Ameshastaafu huyo...au mnataka kila jambo la jeshini liwe published? Endeleeni kumtafuta Ben kama kashikwa ugoni kamlipieni fine arudi kijana wa watu lakini shughuli za uendeshaji wa serikali waachieni wenye mamlaka. Yakwako ndani ya nyumba yanakushinda iweje ufatilie ya jirani. Boss akirudi toka ulaya nadhani atatusaidia suala la kijana mpotevu
 
Tunajenga ukilaza kila mahali ili kuimarisha nguvu ya dikteta UCHWARA,YY ANAJUA KILA KITU,MAKOFI MEEEENGIII!!!!!
 
Tumia akili, jeshi limefungwa kisheria lkn lowassa hajafungwa kisheria. Huu ndio tunaoita kwa kingereza GRAFT CORRUPTION. Taasisi inahongwa ili itoe upendeleo.
Think out of the box, ni jeshi kama taasisi ndiyo limefungwa kisheria kutojihusisha na siasa, mwanajeshi kama raia hajafungwa kisheria kuacha jeshi ili kujihusisha na siasa. Kwa hiyo kwa huyo mteule anaweza kuamua aidha kukataa uteuzi huo na kuendelea na jeshi au akubali uteuzi na kuamua kuacha jeshi iwapo alikuwa bado anaendelea na kazi jeshini.
 
Kwani Lowassa alikuwa mwanajeshi wkt anahamia Chadema.....?issue apa ni mwanajeshi kuteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

Kaanza kuwa mwanachama siku hiyo hiyo aliyoteuliwa. Kabla hakuwa mwanachama wa chama chochote.

Jibu hilo hapo
 
Kipi kinaanza kuacha na kuingia kwenye siasa au kuingia kwenye siasa na baadae ndio unaacha? Ukweli unabaki pale pale kuwa vyombo vyetu vya usalama si huru a kwani ndani yake kuna wanachama wa vyama vya siasa na hivyo hutumika kutimiza matakwa ya chama ya chama kwa hope kuwa Siku moja watapewa nyadhifa mbali mbali wakiwa kazini au baada ya kustafu.
Jambo hili ambalo malaika mtukufu analianza litkapokuja kuturudia tutajuta.
JIFUNZENI KWA SIMBA, AKISHA KULA NYAMA YA BINADAMU HATA WATOTO WAKE HUULIWA. Unafikiri ni kwann?
 
Kwa haraka na uhakika nchi inageuzwa kuwa ya kidikteta. Na ukiona hivyo ujue wanatafutwa akina Goring, Himmler na Joseph Goebbels. Ee Mungu tuhurumie Watanzania tumekukosea nin!!!!!!!
 
Reactions: bne
Yani kweli kuna watu wanabahati zao,mtu yupo katika ajira ya serikalini anaachishwa na kuletwa kwenye chama, dah vyeti vyangu ngoja viliwe na panya tu

Alishastaafu muda akawa anafanya kwa mkataba. Na mkataba unasitishwa muda wowote. Ikiwa Lowasa aliacha CCM leo na kesho yake akapewa kadi na kugombea uraisi hamuoni ni ajabu bali hili la mstaafu kupewa majukumu mengine povu linawatoka
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
uanajeshi" hii ni nomination tu ambayo mtu yeyote yule leo rais ama yeyote mwenye mamlaka anaweza kumpatia raia? ama ni lazima upitie mchakato flani ktk hao wenye mamlaka ndiyo uwe mwanajeshi. Hivyo basi naamini huwezi kukoma uanajeshi wako eti tu kwa kuacha kuvaa gwanda za kijeshi ama kutimiza majukumu ya kijeshi kwa wakati huo.
Inabidi iwe wazi ukishapitia mafunzo yeyote ya kijeshi wewe ukae mbali na majukumu yote ya kiraia.
 
Kamshtaki basi kama imekuuma
Suala siyo kumshitaki, suala hapa ni uzumbukuku wako usiotaka kuuona ukweli. Jeshi la Wananchi wa Tanzania haliwezi kuchezewa kwa namna linavyoanza kuchezewa na viongozi muflisi wa Chama cha Mapinduzi. Ni lini askari huyu alistaafu na kuchukua kadi ya ccm?
 

jamiiforums.com Earn 10$ for every 30 second Task. Internet Job, ok it must be digested more
 
Nimepoteza Imani na jwtz na majeshi yote kaa haya yanayotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…