Hawa wasomi ndio njaa na sidhani ata kama wanaelewa maana ya uzalendo au kuitakia mema nchi yao. Taifa linawatu takribani millioni 50 atuwezi kuwaachia kikundi cha watu wasiozidi miambili or more at senior civil services position wafanye maamuzi yote ya serikari kwa siri bila ya kuulizana madhara ya maamuzi yao kwa maslahi ya taifa ndio maana atupigi hatua kwa mambo kama haya na wala aturekebishi makosa pale tunapojikwaa.
Sikubaliani na Lissu kwa kila jambo na wala siwezi kuelewa motives zake zote lakini kuipa habari jamii ya kuwa ndege ipo mikononi mwa watu wengine na tuna deni fulani inasaidia na wengine kuona matatizo tuliyanayo, kuleta mijadala ya kitaifa na kutafuta suluhu iliyobora sio bora suluhu kama serikari ilivyozoea kufanya mambo.
Wenzetu wanajifunza mnamo Oktoba ya 1973, Egypt na Syria waliivamia Israel kwa kuishtukizia wakati wapo kwenye sikuu yao 'Yom Kippur' baada ya kuona inaelemewa Marekani wakaamua kuwapelekea ndege za kuweza kumudu mashambulizi. Kilichofuata ni kwamba nchi za kiarabu zilizokuwa zinawauzia mafuta zikakata supply Marekani pamoja na wale wote wanao support Israel; madhara yake kwa muda mchache mafuta sokoni yakapanda kwa asilimi 500%, bei za biadhaa zikapanda huko makwao, foleni za kufa mtu kwenye vituo vya mafuta, ajira nyingi zikapotea baada ya jamii kutokuwa na uwezo wa kumudu bei ya bidhaa, uzalishaji ukapungua, GDP zikashuka na mawaziri kadhaa wakafanywa mbuzi wa kafara kwa lawama za kushindwa kuwa na majibu ya changamoto. Nchi zingine zilizo athirika zakaenda mbali zikatoa vyama vilivyokuweko madarakani kwenye uchaguzi uliofuata.
Baada ya mgororo kuisha na hali ya kawaida kujirudia wazungu watu wakujifunza wakaitana wote walioathirika kutafuta majibu wanazuia vipi athari kubwa kama hizo kujirudia maana mafuta ndio gurudumu la uchumi wao, stability ya jamii na national security hilo somo walipewa kwa miezi michache sana na waarabu. Kilichofuata wakaja na sera za kuwa na reserve za miezi kadhaa kuweza kuhimili supply ya ndani wakati wanayafuata mbali zaidi, kuongeza kasi ya utafutaji mafuta nje ya nchi za kiarabu kusudi wawe na suppliers wengi duniani kutoathirika na chombo cha ushauri kwa athari zilizo mbele kutokana na siasa za dunia. Leo wao ndio wanachagua mafuta wayafuate wapi.
Leo hii mtu ambae tunaambiwa ndio chanzo kufanya nchi iende arbitration na kufanya ndege ichuckuliwe anarudia tena kufanya kitu icho icho sehemu nyingine na watu awataki kuulidhana kuna madhara gani kwetu, tunajikinga vipi na hizo athari kwa nchi maskini hawa watu kulipa haya madeni sio shida kwao lakini kwa gharama za huduma za jamii na wanaoumia ni wale wenye kipato duni. Sasa badala ya hawa wasomi kushauri kisomi wanaleta hoja za siasa hayo mambo wamwachie Joseph Msukuma na akina mdee, wasomi wanatakiwa washauri namna sahihi kuakikisha serikari aichukui tender zinazoweza tuletea madhara au kuingia mikataba inayolinda maslahi yetu pale tunapovunja tender na kushinda kesi mahakamani, kuishauri serikari kupima maamuzi yake; etc. sio huu upuuzi wa kumpa kichwa mtu kisa kujipendekeza watu wasifiwe kwa mazuri na wakosolewe kwenye mapungufu yao vinginevyo atujengi tamaduni ya kuwa kuwa wabunifu kwenye changamoto na ku handle haya mambo tofauti mbeleni yakitokea na ndio maana zaidi ya miaka hamsini tupo pale pale.