Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana. Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji.
Uzalendo my foot! Pambaff kabisa.. Hivi Ubomoaji unaoendelea Kimara una Uzalendo gani? Kwa nini watu walazwe nje kisa barabra ya mita 240 kama si kukomoana? Hivi hizo mita 240 zitajengwa lini? upanuzi umewafuata watu kwa nini wasilipwe fidia kwanza? Halafu mnaongelea uzalendo wa Lisu.. Upuuzi kabisa, Lisu ndio alikataa kulipa watu walioshinda kesi za madai dhidi ya serikali?
 
401857_heroa.jpg


DAMASI NDUNGURU
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

[Tatizo lenu ni kubwa hamtaki kulipa madeni sasa mtalipa pamoja na riba]

hqdefault.jpg


BENSON BANA
Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

[Taarifa za madeni, wizi, rushwa wananchi hawatakiwi kujua, Lissu kaleta balaa jamani !!]

picwachumi.jpg


HAJI SEMBOJA
“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja.

[ Wenye kujua uongozi hunyamza kimya mambo hakiharibika, hukenua meno mambo yakiwa mazuri kwao tu.]
Maprofesa uchwara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama legelege uzaa Serikali legelege, na hiyo Serikali legelege ndiyo inayo-sign mikataba usiku wa manane mahotelini ulaya tena bila kuzingatia exit clause.

CCM haiwezi kukikwepa kikombe hiki kushindwa kusimamia Serikali iliyoiunda yenyewe - Sasa mzingo wa adhabu wote unamwisha mtanzania lah!!!
 
ACACIA haiwezi kumtumia myopic thinker kama Lisu sababu tayari Ina team ya watu wenye uwezo mkubwa kwenye mambo hayo.

Huyo anaropoka tu sababu ni tabia yake.
 
Siding with the enemy makes one an enemy too, and enemies from within must be neutralised, at whatever cost!
The enemies from within are those costing this wonderful nation billions of money for their uncalled and most stupid decisions they make as if they were headless at the time they were making those decisions!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nlishasema kuliko watoto wangu waje kusoma Phd,ntachana vyeti vyao wote wasiwe na sifa kabisa.Bure kabisa hawa Phd Holder wa hii nchi.
Hakika umenena,maana aliyewahi kuwa rais wa Africa kusini aliwahi sema kuwa mwafrica hata akisoma huwa haachi upumbavu wake.Pia mwalimu nyerere alisema upumbavu in kipaji kama ilivyo urefu na ufupi.
 
The enemies from within are those costing this wonderful nation billions of money for their uncalled and most stupid decisions they make as if they were headless at the time they were making those decisions!

Sent using Jamii Forums mobile app
They are no different from Tundu Lisu!
They fill their stomachs , same as those promised 10% for siding with the enemy!
 
Jamani!! Hebu vitu vingine sio vya kuandika . Darasa la saba la kufeli anamjibu mtu mwenye masters ya sheria?? Watajibizana nini zaidi ya zero tu??

Sent using Jamii Forums mobile app
amefeli vyeti sio akili ya kuzaliwa.tumbo lissu amefaulu vyeti kafeli akili ya kuzaliwa na uzalendo ndio maana wana tofauti kubwa ya kipato.
wakati tumbo lissu akiwakuwadia wazungu kule orotea hotel ili apate rizki mwenzake ni tajiri anayejimudu na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania kupitia kampuni zake za kizawa
tapatalk_1503250562147.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joeph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.


​

Kideo kwa hisani ya Millard Ayo

Nenda shule brother bado hujachelewa juzi nimemuona mzee mmoja Kenya ana miaka 60 hivi anafanya 0 level. Kwa hivyo ndugu yangu muda unao wewe kama kiongozi wetu wa chama mkoa unatia aibu.
 
Ngoja tundu lissu awapige misumari ya nyundo. Mtakoma kufanya mambo kienyeji.
Hivi nyie mnapokuwa mnamshika shika ovyo ovyo, mnategemea hata mimi ningekuwa mzalendo?
 
Jamani.......

Hakuna msemaji mkuu aliyeandaliwa ili kuepusha hizi sintofahamu?
 
Back
Top Bottom