Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Yale yale sie ni wazee wa kufanya siri kwa kila jambo...kama serikali ingekuwa inatoa updates mara kwa mara kuhusu hiyo ndege sidhani kama tungefika hapa...walishataja na muda wa kuwasili tena mbele ya waandishi wa habari sasa kwanini kama haiji wasiseme tena
 
Wanasiasa wanapanga kuhujumu usalama wapo wakashindwa kutegua mtego .....msemaji wa serikali analalamika kama akina sisi badala ya kutoa taarifa rasmi inayojitosheleza ....taarifa ya kihuni hii ...
 
Ktk Suala hili, kuna mafunzo 3:
  1. Rais awe na subira ktk maamuzi yake na awatumie/awasikilize washauri wake ipasavyo.
  2. Rais afanye kazi na wapinzani wake kisiasa. Chuki yake kwa wapinzani 'halisi' ipo wazi. Treatment anayopata Lissu na Lipumba ni tofauti. Vile vile CUF-Maalimu vs CUF-Lipumba, Chadema vs ACT, etc. Ajitahidi kuwaunganisha watanzania.
  3. Kama ni kweli Lissu alitoa msaada wa kisheria uliofanikisha kampuni ya Canada kupata akili ya kukamata ndege ya Tanzania, basi ina maana ni mtu hatari ambaye yupo tayari kutumia taaluma yake ya sheria kwa namna yoyote ili kuonyesha alikuwa sahihi kumpinga rais/serikali kuhusu mikataba. He just wanted to prove a point. Hapa sina maana amefanya kosa kisheria, ila kimaadili na kizalendo-sitegemei mtanzania aliyesomeshwa kwa pesa za jasho na damu la watanzania, atumie elimu yake kumsaidia mzungu kutukamua. Ni dhahiri kazi haikufanyika sawa sawa ndo maana tukavunja mkataba, kwanini mtanzania amsaidie mzungu kutukamua fidia wakati kosa lilikuwa la mzungu?
 
Watu 50 wa familia yenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inapofikia hatua kiongozi wa wananchi anaesema anatetea wananchi anataka Tanzania isipewe misaada, nchi wahisani wakate misaada yao, hivi nani anaumia? Wao au sisi wananchi? Kweli upinzani wa nchi hii tatizo sana, wao wanapata pesa nyingi wanatembelea magari mazuri misaada ikikatwa nani wa kuumia? Nimeanza kuuchukia upinzani sana siupendi kabisa, kauli zao sio za kizalendo, ni waongo upeo.
Leo tena jambo linalohitaji weledi na hekima msomi mzima anashabikia Tanzania kudaiwa!! Tukisema ni kibaraka wa wazungu tutakuwa tumekosea!! Hivi nani wanaopanda hizo ndege kama sio yeye na wenzake? Nchi ikikwama maendeleo hasara ni ya nani. Upinzani wa nchi hii matope sana, waende kujifunza upya kwa nchi nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi naomba niwe muwazi tu kwa hili naona kuna mchezo mchafu unafanyika sema aimjui anayeufanya.
Hiyo tenda ilikuwa mwaka 2010 na kuporwa mawka 2013.
Mkataba wa kunua ndege umefanyika mwaka 2016.
Kampuni iliyoporwa tenda inahusika na ujenzi wa barabara.
Kampuni inayouza ndege kwa Tanzania ni kiwanda cha kutengeneza ndege.
Sasa maswali yangu ni haya.
1.unaruhusu vipi bidhaa uliyoagizwa na kulipwa gharama zote itumike kulipa deni la mtu mwingine kabla bidhaa hiyo haijamfikia mnunuzi?
Kama serikali imeingia mkataba na Bombardier inakuwaje Bombadier waruhusu mzigo uzuiliwe na mtu ambaye sio mteja wao?
Hiyo kampuni ya ujenzi iliingia mkataba na serikali ya Tanzania au na kampuni ya Bombardier?
Nadhani kuna kitu hakipo sawa hapa.
 
Mlienda shule kukua viimo au nn mbona mna arguments za kitoto sana, so kodi yetu inayotumiwa vibaya inafananishwa na shamba la babako? You a fool at highest level

Wewe ndo huyo uliyemtaja hapo juu, maana utaendelea kulipa kodi zaidi na ukishangilia.
 
Mfano wa kijinga Sana, shule ulienda kusomea ujinga ???
 
Published on 19 Aug 2017
Serikali Yafungukia Mgogoro wa Ununuzi wa Ndege ya Bombadier

Msemaji wa Serikali ya Tanzania akiri kushikiliwa kwa ndege ambayo ni mali ya serikali ya Tanzania kupitia amri iliyotolewa na mahakama. Hatua za kidiplomasia na za kisheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili .

Msemaji wa serikali amekwenda mbali na kulaumu baadhi ya watanzania kutokushabikia mambo yasiyohusu Bombadier kama vile mauaji ya Kibiti n.k bali hili imekuwa nogwa kuhusu bombardier........ maana suala hili la kukamatwa kwa ndege linamgusa Mh. Rais moja kwa moja na anashangaa mkuu wa nchi kubezwa.......

Source: Global Tv Online
 
Deni liwepo lisiwepo kibaraka m.se.nge mzawa hawezi kujitia msemaji wa wadai. Serikali mukiweza Kill him shenzi type
Hii inaitwa msumari wa moto umepenya ukatokelezea kwenye koromeo..

Tulia....Serikali imeamua kujivua nguo yenyewe
 
Mfano wa kijinga Sana, shule ulienda kusomea ujinga ???
Wewe ndiyo maana maana mfumuko wa bei utaenda juu na utalipa kodi zaidi hata ukifanya biashara hela itapungua. endelea kufurahia na hao traitor wenzako. Unafikiri hapo unaimaliza serikali, ulichoenda kusomea huko shuleni ndo hicho?
 
Kila kitu kinachofanyika na kulisababishia taifa hasara, kimekuwa kikifanywa kwa mbwembwe huku wafuasi wakishangilia na kupiga makofi lakini linapokuja suala la kulipa gharama za ukurupukaji watu tena wakiwemo viongozi wakubwa wanaanza kuweweseka eti wanahujumiwa.

Waliotuhujumu ni wale ambao walifanya maamzi ya hovyo na kusababisha hayo yote
waliotuhujumu ni wale ambao walituwakilisha katika kesi na baadae wakarudi kutuambia eti tumeshindwa kesi

Lissu hahusiki hapa na kumhusisha ni dalili za kuchanganyikiwa
over
 

Lissu katika mtandao wake wa twita ameonekana kuyacheka majibu ya serikali juu ya "kupotea" kwa Bombadia.

Serikali imetoa majibu yasiyoridhisha na ya kujikanganya kuhusu kashikiliwa kwa ndege yake nchini Canada. Serikali imelaumu wanasiasa kuingilia mchakato huku ikiogopa kuwataja wanasiasa hao

Maoni Yangu
Lissu acheki kukamatwa kwa ndege nchini Canada,anacheka majibu ya serikali. Ikumbukwe kuwa waziri Mbarawa alitoa kauli inayokinzana na msemaji wa serikali
Nini maoni yako
 
Haya ndio tumekuwa tukiyasema kila siku....Hawa wapinzani wa nchi hii wakae wakijua hawamkomoi MAGUFULI bali wanatukomoa sisi WATANZANIA
Hivi anayekomoa ni nani hasa?
Ni yule anayegundua matatizo yaliyopo na kuyasema watu wayajue au yule aliyesababisha hayo matatizo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…