Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Swala siyo kushabikia bali wananchi wan
 
Sielewi umeandika vitu gani hapa!
Inaelekea ulichoandika hata hukijui.
Huelewi nini? Huelewi maana ya maneno "kuinanga" na "kuinusuru"?

Usipoeleza kinagaubaga usichoelewa usiowaelewa watashindwa kukuelewesha kwa sababu katika kusema kwako huelewi na wewe hueleweki.

Au na wewe ni kati ya wale msiojua tofauti ya nchi na serikali?

Wewe unasema huelewi nilichoandika halafu unasema kitu hicho hicho usichokielewa mimi niliyekiandika sikijui?

Ni kama umeangalia hyeroglyphics za Wamisri wa kale ukatoka patupu hujaelewa kilichoandikwa, halafu ukaishia kusema "hawa walioandika hapa hata hawajui wameandika nini".

Utakuwa mjinga. Kwa sababu umerukia kusema hawajui walichoandika bila ya kuelewa wameandika nini.

Acha ujinga, kama hujaelewa uliza ueleweshwe halafu kama ulichoeleweshwa unaona anayekuelewesha haelewi hapo ndipo useme hivyo, kwa hoja.

Si kwa ku dismiss kitu usichokielewa.

Dismissing what you don't understand is the hallmark of a fool.
 
Best comment of the day.... Ngoja nikalale sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unashangaa wananchi wanapohoji habari zinazohusu matumizi ya fedha zao za kodi?

Unafikiri serikali inatoa wapi hizo fedha za kununua ndege na kulipa wakandarasi?
Mbona zamani wewe na mafisadi wenzako mlikuwa mnasunda mifukoni na hatusemi.. haohao mafisadi ambao mmewakaribisha, mmewasafisha na mnataka waende ikulu kuongoza nchi kifisadi. Upuuzi mtupu
 
Wakikujibu 2020 gombea urais.

ACHA nikae KIMYA...!
 
mwenza ndani ya nyumba ukiona ana vitabia vya kutosema ukweli, kila mara kujitetea, jua huyo umeokota ghalasha. kwa wakristu ni kuvumilia, sahihi ni talaka tatu.
 
Yep...usumbufu ni sawa.


..inawezekana aliyevunja mkataba alifanya hivyo kwa nia njema kabisa.

..tatizo ni wahusika waliochelewesha kulipa deni hili. Tena baada ya hukumu mbili ya mwaka 2009 na 2010.

..Na msemaji wa serikali amekosea kutumbukiza siasa ktk majibu yake. Ingetosha tu kusema serikali inafanya jitihada za kukamilisha taratibu za kuileta ndege yetu.

Cc BAK
 
Reactions: BAK
Unashangaa wananchi wanapohoji habari zinazohusu matumizi ya fedha zao za kodi?

Unafikiri serikali inatoa wapi hizo fedha za kununua ndege na kulipa wakandarasi?
Mbona zamani mlikua hamhoji kuwa kwa nini ndege hazinunuliwi.. iweje leo. Au kwa sababu mmeona kuna mtu anachukua maamuzi sasa kitaifa na kufanya yale wananchi wanayotaka kusikia.. kaa kimya kamanda unyolewe.. kinyozi amepatikana
 
Sasa naanza kumwelewa Kagame kwa nn huwa hawachekei wasaliti wa nchi kama hawa! Huwezi kuhujumu nchi ukabaki kupigiwa makofi!! Ni Tz tu!!!!
Sina uhakika kama kuna watu wanakutegemea kama mlezi wao. Kama wapo na wakasoma post yako ukirudi home tu utashangaa wote wanatoka sebuleni kwenda chumbani kulala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona zamani wewe na mafisadi wenzako mlikuwa mnasunda mifukoni na hatusemi.. haohao mafisadi ambao mmewakaribisha, mmewasafisha na mnataka waende ikulu kuongoza nchi kifisadi. Upuuzi mtupu
Zamani lini?

Mimi ni nani? Mafisadi wenzangu kina nai? Tulisunda nini? Wapi? Kwa nini hamkusema? Tumewakaribisha mafisadi gani? Wapi? Lini? Tumewasafisha wapi? Tumetaka waende Ikulu lini? Wapi?

Jibu maswali yote hayo kwa ushahidi.

Ama sivyo umenipa leseni ya kukuita mzushi, muongo, mzandiki, mjinga na jina lolote baya litakalonijia kichwani mpaka uniombe radhi.
 
Ni sawa Mkuu, ila Siasa za sasa ni za chuki sana.

Hii ndiyo inayofanya watu kuombeana mabaya badala ya mema.
 
Mkuu wanataka kufanya uhuni wa kibongo kwenye mikataba ya Kimataifa, KAMWE hilo halitatokea na nchi itapata hasara kubwa sana kwa kukurupuka na kutaka kufanya uhuni. Hukumu $25 Million wakapotezea miaka 7 baadaye deni limeongezeka zaidi ya nusu!

Wakataka kuficha uovu wao, wasamaria wema wakawaanika hadharani badala ya kumkoromea husika Mkuu wanamgeuzia kibao Kamanda Lissu! Wapuuzi sana hawa Mkuu.

 
Mkuu huyu jamaa TL hata kipindi cha Mkapa sasa hivi ingekuwa story nyingine,ila dawa yake inachemka kwa kasi sana,kile kitambi kitashuka ghafla kama puto(balloon).Kagame huwa anawafata hata U.S anawatungua huko huko kwa maslahi mapana ya nchi.
Nyie mtakua mataahira sasa kama mnamshindwa mtu anakaa tegeta apo tuu!!!!

Mnakuja kufarijiana humu pumbaff kabisa
dawa gani hiyo inachemka miaka?
 
KWani nani kalisababisha deni ni la miaka 2006 aliyefuta huo mkataba ni Anna Abdalah.
Msitufanye Watanzania wote punguani kawadanganye Lumumba wenzako wenye akili za kushikiwa na Mkiti.
 
Naona tukija na hoja za mantiki wanasepa.

Kuna watu unaanza kubishana nao kwa kasi halafu mmoja mmoja anasepa hawajibu hoja.
 
Reactions: BAK
Na sisi tuishitaki Kampuni iliyopata tender ya kututengenezea ndege kwa kuvunja mkataba kwa kutotukabidhi ndege according to mkataba. Awali ya yote naona hao walioshika hiyo ndege wameingia mkenge kama tungekuwa nawanasheria wasiogopa wazungu. Mimi nahoji hiyo ndege inakuwaje mali yetu kabla ya kukabidhiwa? Au hayo yalishafanyika? Hiyo ndege kama ni yetu ina namba za uajili za Tanzania? Hatuoni kama madai ya kukurupuka kwa serikali yetu kunafanana na kukutupuka kwa serikali ya wenzetu? Basi na sisi tucheze karata zetu vizuri ili tufidiwe matrilion ya fedha kwa kucheleweshewa ndege yetu. Sisi tunakomaa na kiwanda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wa aina mbili duniani.

Wale wanaolipa madeni yao na wale wasiolipa madeni yao.

Kamwe usitake kuwa kwenye hilo kundi la pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…