Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Wakati fulani hapa chamani tulikuwa na watu waliojulikana kama wanasheria wa chama na ninamkumbuka mmoja akiitwa Kunambi. Lakini zama hizi sijajua kama bado tunao wanasheria wa chama, ila ningeomba tupate mtu mwenye uwezo wa kujibu na kujenga hoja zitokanazo na changamoto mbalimbali. Haiwezekani leo hii Lissu au Zitto wanaibuka na hoja nyepesi zenye majibu ya kawaida lakini sisi kama chama tunabaki kimya. Leo hii Lissu anawaaminisha watanzania kwamba serikali ikiingia mkataba ni mwiko kuhoji au kuuvunja kwa sababu nchi itashtakiwa, na sisi CCM tumebaki kimya tukumbuke kuwa Lissu ni mwanasiasa na anaongea mambo yote kupitia chama chake chadema, hivyo anapaswa kujibiwa kisiasa na chama kilichounda serikali yaani CCM. Ahsante!
Wewe unataka watu wagombane ikulu lumumba unadhani lissu spoti spoti ujue hata pilato mkuu anamgwaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeeleza vizuri maana ya mbwa aliyoikusudia Yesu.Ni kule kuachana na lengo kuu na kuanza na kuhangaika na kila unaloliona na kulisikia. Ni kushindwa kuwa focused kwa jamii,famlia,Taifa kwa ujumla.Tafakari ni ndefu.Mbwa anaweza kutumika kueleza mengi
Tatizo linalofanya ni kuendesha nchi kama jumuiya za parokia au familia. Hapa husitegemee focus yoyote hata Malaika ashuke. Kumbuka tatizo/mahitaji ya Raia wa Muheza ni tofauti na matatizo ya Raia wa Katerero, japo yanaweza kushabihana ila sio kwamba yapo sawa au yanafanana, hapa focus utaipata wapi? Ili hali kama taifa halina hata sera yake kama taifa, zaidi ya kuongozwa na sera za chama cha makinikia.
Endeleeni kuwapa watoto (raia wa chato) hicho chakula ambacho mmnaamini hakikupaswa kupewa mbwa (raia wa Mbozi)
Pengine muda ndio utaweka bayana kati ya mbwa na mtoto
"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Issue serikali inadaiwa ama haidaiwi, hata kupiga kelele ni uzalendo pia na ndio maana serikali imejibu kuitia Mkurugenzi wa Idara ya Habari
 
Hebu fikiria mtu unamwita raisi wako hilo neno eti kwasabau tu unatumia Kompyuta ukiwa nje ya Tanzania.

Ni hasira gani hiyo uliyo nayo juu ya huyu kiongozi?

Kila binadamu ana mapungufu yake na hata wewe ungekuwa kiongozi leo ni lazima ungekuwa na kasoro zako.

Lakini kwa hii ya name calling umekwenda too much step brother/ sister.

Tafakari.

..lakini hata "mzee" naye hana lugha nzuri.

..umesahau alivyosema kwamba yule Prof ana mawazo ya kinyama?
 
Tanzania Ni Nchi Ya Ajabu Sana Siku Zote Taifa Hili Wananchi Wake Hupenda Kudanganywa Akitokea Msema Ukweli Huchukiwa Sana Mfano Mdogo Kafulila, Hivi Ile Hasara Ni Pesa Za Nani Zinalipwa? Ccm Wanajivunia Wapumbavu Wa Taifa Hili Taifa Linaendelea Kupata Hasara Mmoja Anashawish Watu Waone Hasara Kwa Taifa Ni Jambo La Kawaida Kwa Nini Yanatumbuliwa Majipu? Taifa La Hovyo Sana Makodi Yasiyo Na Vichwa Wala Miguu Kumbe Watu Wanavunja Hovyo Mikataba.
 
Msianze kuhangaika tunazungumzia kuvunjwa kwa mkataba na ni nani alihusika kuuvunja ndiyo msingi wa mjadala.

Tundu Lisu "Kibaraka wa wazungu" amesema aliehusika kuvunja mkataba ni raisi John Magufuli wakati akiwa ni waziri wa ujenzi na ushahidi wote upo umehifadhiwa.

Ila mkataba ulivunjwa mwaka 2009 na serikali huku Dr Kawambwa akiwa waziri husika.

Ukianza kuzungumzia mwaka 2010 rufaa ilipokatwa unakuwa unaanza kupotosha umma.

Yaani unaonekana unababaika.

Haya mambo hayataki pupa bali ni mwendo mdundo.
Kuna muda inabidi watu wapuuzwe. Mara alivunja mkataba akiwa Waziri hivyo kusababisha hasara mara wanabadili gia angani kwamba wakati hukumu inatoka Mheshimiwa alikuwa waziri. Mara nyingi njia ya muongo huwa haitoki ubungo hadi mbagala bali ni kutoka ubungo na kuishia ubungo.
 
Kuna watu humu JF wanaichezea serikali kwa kuleta taarifa za uwongo. Mmefikia hatua mnatumia hadi nembo za serikali. Msifikili serikali haiyoni huu ujinga. Mtapatikana tu.! Nikundi la watu wachache. We are tired of this. Kiukweli tunakosa uzalendo wa kweli. Serikali inasitahili heshima yake.Kuna mipaka inabidi tusiivuke no matter what.
Screenshot_2017-08-20-18-16-07.png
Screenshot_2017-08-20-18-15-46.png
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hamna lolote mapovu yanawatoka tu, mnaambiwa ukirusha jiwe gizani ukasikia kelele tu ujue limempata. Lumumba limewapata hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli limewapata maana Mkurugenzi wa Habari yote amekubali isipokuwa la kumhusisha Magufuri kwani kipindi hicho alikuwa Shukuru Kawambwa na amemtaka TL kuomba radhi ndani ya 7 days ...(hapa kweli ndio wameshikwa maana serikali hii utamaduni wa kumtaka mtu aombe radhi hakuna na hii ni dalili kweli wameshikwa)
 
Tafakari kwa kina yawezekana Mimi na wewe ndo mbwa wenyewe "tunaoswongomela" mahitaji ya "watoto".Sijamlenga mtu.Ila kwa staili na namna yotote ile ukishindwa kujali ustawi wa watanzania wenzio na Taifa kwa ujumla wake basi huna tofauti na mbwa wanaopewa tafakari katika mada hii.

Nikikuita mbwa mpumbavu nitakuwa nimekosea? Haiingii akilini mpishi wa hilo pishi lililotarajiwa kuliwa na kuzaswa ili mbwa mle awalishe mbwa lote as if aliambiwa awapikie mbwa! Kisha mpishi huyo yupo tu barazani kwa bwana akipunga upepo!
Ile mahakama ya mafisadi haikuwafaa wapishi wa haya madeni? Kama sivyo mliziazisha kutuzuga?
Katiba mpya ilitufaa sana lakini kwa ulaku wa kushare makombo mliivuruga huku mkijua mlitendalo eti imani itawaponya!
Tutaheshimiana tu kwa kufukua huku makaburi! Jipangeni enyi mnaoishika biblia mkono wa kushoto huku mkono wa kuume ukishikilia sandarusi iliyojaa fedha za wizi! Hamtapona kwa dhihaka hii mnayomfanyia Mungu wangu aliyehai.
 
Watu mnapiga kelele sana oooh ndege imekamatwa kwa sababu ya deni tulilokuwa nalo!! kwanza sidhani kama tulikataa kulipa hili deni.

Sidhani kabisa bali ilikuwa swala la Muda na hali ya uchumi wetu.kama serikali ilikata rufaa na bado tukashindwa hili ni suala la kawaida kushindwa siyo kwamba sisi ni watu wa kwanza kushindwa.

Mnatulisha maneno eti tumchukie rais wetu lakini hamuoneshi kwa nini aliyekuwa waziri wa ujenzi kipindi hicho aliamua kuvunja mkataba husika. Lakini ni seme tena kwamba sioni sababu ya kumlaumu waziri mhusika kwa sababu kipini hicho alikuwa chini ya rais kwa hiyo mimi naamini kabla ya kuvunja mkataba huo alimshilikisha rais aliyekuwepo. Kwanini leo alaumiwe na isiwe serikali iliyokuwepo wakati huo?

Hata kama isingekuwa kukamatwa kwa ndege hii deni hili tungelilipa tu na serikali yoyote ambayo ingeingia madarakani lazima ingelipa deni hili. Kudaiwa ni kitu cha kawaida.

Wakulaumia ni serikali iliyokuwepo madarakani kipindi hicho kwa nini haikulipa deni hili mapoema kabla ya kuwa kubwa?

Je, waziri ndiye aliyekataza serikali isilipe kwa muda? kama ni ndiyo basi serikali iliyokuwepo ilikuwa legele !
 
Mbona magamba mnaweweseka sana?

Mambo ya msingi hamtaki kujibu, badala yake timu Lumumba mmepewa assignment na mabosi wenu muanzishe thread nyingi kadri muwezavyo ili kumponda Tundu Lissu......

Lakini kuna msemo unaosema penye ukweli uongo hujitenga.......

Nyinyi mtajitahidi kuleta kila aina ya propaganda lakini ukweli utabaki pale pale kuwa ndege ya Bombardier imepigwa "tanchi" huko Canada kutokana na maamuzi ya kibabe aliyoyafanya Rais wetu wakati huo alipokuwa Waziri wa ujenzi kwa kuvunja mkataba pasipo kufuata taratibu walizokuwa wamewekeana iwapo ingebidi mkataba uvunjwe. That's all and OVAA.....
 
Acha kumtetea dikteta uchwara dah!
Wapinzani wanaelewesha wapiga kura kama wewe hutaki kuelewa hilo ni tatizo lako binafsi, jiongeze.




Unafahamu mkuu hawa wapinzani hawajatambua watumie vigezo na mbinu gani ili waweze kuwaelewesha wananchi tofauti yao wao na serikali iliyopo.

Yaani wao wakiwa na serikali siku moja Mungu akiwaajalia watafanya mambo kadha wa kadha na kadha.

Hii ndiyo mbinu kubwa inayotumiwa na wapinzani kote duniani iwe nchi zilizoendelea au nchi zinazoendelea.

Tatizo kubwa la wapinzani wa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo ni kwamba wao wanakuwa rahisi kutekwa na mapebari na makabaila ili kuweza kushika madaraka.

Ndiyo maana mabepari wanaowakilishwa na haya makampuni makubwa na makabaila ambao ni wale watu wanaotawala kwa kutumia ardhi kama Edward Lowasa, Frederick Sumaye na wengine wa nje wanakuwa rahisi kuwatumia watu kama Tundu Lissu lakini kwa uangaaiifu sana.

Siku zote huwezi ukakaa na mzungu halafu mkubaliane kitu chochote kwa manufaa ya wote bali ni kwa manufaa ya wachache.

Na Tundu Lissu anadhihirisha hilo kwa kukaa chini na hao wazungu ili kujadili namna ya kumhujumu raisi John Magufuli kwa kutumia sababu ambazo zingine si sahihi.

Wapinzani wanatakiwa siku zote kujifunza kuweka mambo mbadala ya kufanya tofauti na serikal iliyopo na wakawa wanawaeleimisha wapiga kura.

Upinzani wa Tanzania na khasa wa leo ni wa wale wachumia tumbo na watafutaji matatizo kwa kuongea uchonganishi baina ya serikali na wanannchi huku wakitegemea kupata huruma kutoka kwa haohao wananchi.
 
Back
Top Bottom