Gamba la Nyoka
Platinum Member
- May 1, 2007
- 7,038
- 9,353
Wewe unataka watu wagombane ikulu lumumba unadhani lissu spoti spoti ujue hata pilato mkuu anamgwaya.Wakati fulani hapa chamani tulikuwa na watu waliojulikana kama wanasheria wa chama na ninamkumbuka mmoja akiitwa Kunambi. Lakini zama hizi sijajua kama bado tunao wanasheria wa chama, ila ningeomba tupate mtu mwenye uwezo wa kujibu na kujenga hoja zitokanazo na changamoto mbalimbali. Haiwezekani leo hii Lissu au Zitto wanaibuka na hoja nyepesi zenye majibu ya kawaida lakini sisi kama chama tunabaki kimya. Leo hii Lissu anawaaminisha watanzania kwamba serikali ikiingia mkataba ni mwiko kuhoji au kuuvunja kwa sababu nchi itashtakiwa, na sisi CCM tumebaki kimya tukumbuke kuwa Lissu ni mwanasiasa na anaongea mambo yote kupitia chama chake chadema, hivyo anapaswa kujibiwa kisiasa na chama kilichounda serikali yaani CCM. Ahsante!
Nitautoa mahakamani. Uje.
Tatizo linalofanya ni kuendesha nchi kama jumuiya za parokia au familia. Hapa husitegemee focus yoyote hata Malaika ashuke. Kumbuka tatizo/mahitaji ya Raia wa Muheza ni tofauti na matatizo ya Raia wa Katerero, japo yanaweza kushabihana ila sio kwamba yapo sawa au yanafanana, hapa focus utaipata wapi? Ili hali kama taifa halina hata sera yake kama taifa, zaidi ya kuongozwa na sera za chama cha makinikia.Nimeeleza vizuri maana ya mbwa aliyoikusudia Yesu.Ni kule kuachana na lengo kuu na kuanza na kuhangaika na kila unaloliona na kulisikia. Ni kushindwa kuwa focused kwa jamii,famlia,Taifa kwa ujumla.Tafakari ni ndefu.Mbwa anaweza kutumika kueleza mengi
Sawa.Siku 7 za kwenda wapi nchi si ya baba yenu hii wezi wote lazima waumbuliwe
Lissu anakurupuka sana!!Hapa kweli Lissu inabidi atueleze kwa nini amhusishe JPM na uvunjwaji wa Mkataba wakati JPM wakati huo hakuwa waziri wa ujenzi?
Hebu fikiria mtu unamwita raisi wako hilo neno eti kwasabau tu unatumia Kompyuta ukiwa nje ya Tanzania.
Ni hasira gani hiyo uliyo nayo juu ya huyu kiongozi?
Kila binadamu ana mapungufu yake na hata wewe ungekuwa kiongozi leo ni lazima ungekuwa na kasoro zako.
Lakini kwa hii ya name calling umekwenda too much step brother/ sister.
Tafakari.
Kuna muda inabidi watu wapuuzwe. Mara alivunja mkataba akiwa Waziri hivyo kusababisha hasara mara wanabadili gia angani kwamba wakati hukumu inatoka Mheshimiwa alikuwa waziri. Mara nyingi njia ya muongo huwa haitoki ubungo hadi mbagala bali ni kutoka ubungo na kuishia ubungo.Msianze kuhangaika tunazungumzia kuvunjwa kwa mkataba na ni nani alihusika kuuvunja ndiyo msingi wa mjadala.
Tundu Lisu "Kibaraka wa wazungu" amesema aliehusika kuvunja mkataba ni raisi John Magufuli wakati akiwa ni waziri wa ujenzi na ushahidi wote upo umehifadhiwa.
Ila mkataba ulivunjwa mwaka 2009 na serikali huku Dr Kawambwa akiwa waziri husika.
Ukianza kuzungumzia mwaka 2010 rufaa ilipokatwa unakuwa unaanza kupotosha umma.
Yaani unaonekana unababaika.
Haya mambo hayataki pupa bali ni mwendo mdundo.
Kweli limewapata maana Mkurugenzi wa Habari yote amekubali isipokuwa la kumhusisha Magufuri kwani kipindi hicho alikuwa Shukuru Kawambwa na amemtaka TL kuomba radhi ndani ya 7 days ...(hapa kweli ndio wameshikwa maana serikali hii utamaduni wa kumtaka mtu aombe radhi hakuna na hii ni dalili kweli wameshikwa)Hamna lolote mapovu yanawatoka tu, mnaambiwa ukirusha jiwe gizani ukasikia kelele tu ujue limempata. Lumumba limewapata hilo
Sent using Jamii Forums mobile app
Tafakari kwa kina yawezekana Mimi na wewe ndo mbwa wenyewe "tunaoswongomela" mahitaji ya "watoto".Sijamlenga mtu.Ila kwa staili na namna yotote ile ukishindwa kujali ustawi wa watanzania wenzio na Taifa kwa ujumla wake basi huna tofauti na mbwa wanaopewa tafakari katika mada hii.
..lakini hata "mzee" naye hana lugha nzuri.
..umesahau alivyosema kwamba yule Prof ana mawazo ya kinyama?
Unafahamu mkuu hawa wapinzani hawajatambua watumie vigezo na mbinu gani ili waweze kuwaelewesha wananchi tofauti yao wao na serikali iliyopo.
Yaani wao wakiwa na serikali siku moja Mungu akiwaajalia watafanya mambo kadha wa kadha na kadha.
Hii ndiyo mbinu kubwa inayotumiwa na wapinzani kote duniani iwe nchi zilizoendelea au nchi zinazoendelea.
Tatizo kubwa la wapinzani wa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo ni kwamba wao wanakuwa rahisi kutekwa na mapebari na makabaila ili kuweza kushika madaraka.
Ndiyo maana mabepari wanaowakilishwa na haya makampuni makubwa na makabaila ambao ni wale watu wanaotawala kwa kutumia ardhi kama Edward Lowasa, Frederick Sumaye na wengine wa nje wanakuwa rahisi kuwatumia watu kama Tundu Lissu lakini kwa uangaaiifu sana.
Siku zote huwezi ukakaa na mzungu halafu mkubaliane kitu chochote kwa manufaa ya wote bali ni kwa manufaa ya wachache.
Na Tundu Lissu anadhihirisha hilo kwa kukaa chini na hao wazungu ili kujadili namna ya kumhujumu raisi John Magufuli kwa kutumia sababu ambazo zingine si sahihi.
Wapinzani wanatakiwa siku zote kujifunza kuweka mambo mbadala ya kufanya tofauti na serikal iliyopo na wakawa wanawaeleimisha wapiga kura.
Upinzani wa Tanzania na khasa wa leo ni wa wale wachumia tumbo na watafutaji matatizo kwa kuongea uchonganishi baina ya serikali na wanannchi huku wakitegemea kupata huruma kutoka kwa haohao wananchi.