Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amuonya Maulid Kitenge kwa uzushi wake usiovumilika

Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amuonya Maulid Kitenge kwa uzushi wake usiovumilika

Manara alishawahi kuwatukana watangazaji wa wasafi, watangazaji walinung'unika sana sasa sijui manara aliomba msamaha kimya kimya lakin watangazaji hawakuongea chochote kama manara aliomba msamaha , sasa subir manara akosewe alafu aombwe msamaha kimya kimya,yani utajua tu kama aliombwa msamaha
 
Ni taarifa ambayo bado ya moto moto kabisa ya kama dakika 15 tu zilizopita

Tumekuvumilia mara nyingi sana lakini kwa sasa uvumilivu umetushinda,

Kwanini kila siku ni ww tu kuiongopea Simba mambo ya uongo?

Unaitumia mara kadhaa @wasafifm kuelezea migogoro hewa kuhusu Simba na kutaka kuichafua klabu yetu Kwa maslahi yako binafsi!!

Umekuwa ukifanya hvyo hata ktk Wall zako.

Utadhani Wasafi ni redio yako binafsi.

Simba haitaki iandikwe na kutangazwa kwa mazuri tu, Waandishi na watangazaji wana haki ya kutukosoa Kwa mabaya pia kama tumeyafanya,,,,lakini haitavumilia tena story za uongo na kutunga ambazo hazina source, na zimejaa uzushi.

Ndugu yangu diamondplatnumz ongea nae huyu mtu,,tulio nje tunaona hana nia njema na ustawi wa uwekezaji ulioufanya, nadhan nia yake ni kuona Wasafi fm inakuwa na ugomvi na Wanasimba, na mimi sitakubali kazi niliyopewa na klabu hii ichafuliwe na mtu huyo huyo kila siku,,vinginevyo labda anataka Wanasimba waisuse kusikiliza hii redio, kitu ambacho mimi ntakuwa mtu wa mwisho kukisema, ukizingatia mahusiano yangu binafsi na wewe.

But akiendelea kututangaza uongo na kuandika uongo juu yetu na wachezaji wetu,zipo hatua‘Makhsuus’tutazichukua!!

Simba ni klabu kubwa mno haiwezi kumuogopa mtu mmoja Kwa chuki zake binafsi kutuchafua kila siku,,

Nipo hapa kuisemea klabu hii na kuitetea Kwa nguvu zangu zote hadi pale ukomo wangu utakapotimia ,,

Na ktk kipindi changu mm kama head wa idara ya habari na mawasiliano kwenye klabu hii, sitakubali story za upumbavu na za uongo dhidi yetu Kwa sababu yoyote ile. Narudia tena hili likijirudia la uongo uongo iwe Kwa wachezaji, makocha au viongozi na hata timu Kuna hatua’ MAKHSUUS’ tutazichukua!

Nani miongoni mwetu atakaekubali taasisi anayoingoza ichafuliwe?

Wanasimba hii ngoma kwanza niachieni mimi labda huyu mtu hajajua how Simba is BIG

Kaona tunapata matokeo kila mahali na kaona Simba imetulia anaanzisha uongo wake,,Safari hii nnae na akibisha aendelee.


Hata hivyo na Mimi All - Rounder nakulaumu mno Msemaji wangu wa Simba SC Haji Manara na Uongozi mzima wa Klabu yetu kwa Kumvumilia mno huyu Mpuuzi na Mshamba ambaye najua kuwa anatumika na Mmoja wa Wadhamini wa hiyo Klabu yake iliyolaaniwa katika Kuichafua Simba SC Kupitia hiyo Redio ambayo Yeye ndiye Mkuu wa Idara ya Michezo kisha kuwekwa katika payroll yao.

Uongozi wa Wasafi FM hasa kupitia CEO wake mwenyewe Nasib Abdul (alias) Diamond Platinumz msipokuwa makini na huyu Mtangazaji wenu Maulid Kitenge mnaweza kujikuta mnapoteza Audience Kubwa sana na hata Wadhamini kwani nina uhakika kuna Corporate Companies zingine Mabosi wao ni wana Simba SC hivyo wanaweza kuamua Kususa Kutangaza na Wasafi FM yenu (yako)

Kwa wale mnaotaka kujua nini kimetokea ni kwamba leo hii katika Ukurasa wake wa Instagram Mtangazaji Maulid Kitenge tena baada ya kusikia Simba SC imetoka Suluhu dhidi ya El - Merreikh ya Sudan ( japo Yeye tunajua alitamani kweli kweli Simba SC ifungwe ) ameandika Kiuzushi kabisa kuwa Mchezaji Mghana wa Simba SC Bernard Morisson ana Ugomvi na Kocha Gomez na kwamba ataihama Simba SC.

Maulid Kitenge unachokitafuta Simba SC na hasa kwa wana Simba SC wote (Mimi All - Rounder) nikiwemo utakipata kwani Umeonywa vya Kutosha naona husikii na bado unawashwawashwa tu na Simba SC. Nadhani umeshasahau ulivyoitia matatizoni Radio One ulipokuwepo kule kwa Upuuzi huu huu wa Uzushi na Kuchochea Vurugu Simba SC hadi Ukaonywa na Marehemu Mzee Mengi kisha Mzee Profesa Sarungi (mwana Simba SC ) akaingilia kuipatanisha Simba SC na Radio One kupitia IPP Media.
How Simba is big
 
Mi nimevutiwa na huyo Boss wa USA, maana maulid nae katisha, alivyokua EFM nikasema labda safar za kikaz , alivyohamia wasafi ndo safar zikazid kuchanja mbuga, nikasema hapa kuna namna, hizi safar sio za bure
Jamaa kwa miaka hii katisha,utmuona yko Egoli leo baadaye yuko Seattle ,mara Los Angels mara atapost yuko na Rose Chitala mara ooh yuko kwenye mwewe.
 
Manara kuna kipindi ali muattack shaffih Dauda alafu issue yenyewe ilikuwa ya kawaida,jamaa ana mihemko na Simba yake kwani kosa lake si kuliona.
Shida ya manara kwakuwa ameshawasoma akili za mashabiki wa simba, ndiohutumia udhaifu huo, kuwa fariji, kitenge ameelezea mzozo, wa morison na timu, ya simba, tena kuna mtandao wa kijamii, ndio source ya habari hiyo, kosa lake ni nini?hadi uanze kumtack yeye kama yeye!!ila manara akigeuziwa kibao ataanza kuomba huruma za watu kutokana na hali yake!!!
 
Back
Top Bottom