Moja kwa moja kwenye bandiko
Hi Vita ipo serious
Mtangazaji Vs Msemajii baada ya Maulidi ku'post kwenye ukurasa wake wa Instagram
Nanukuu
Mshambuliaji wa Klabu ya Simba raia wa Ghana, Benard Morrison akaachana na Klabu hiyo mwisho wa msimu huu baada ya kutokuwepo maelewano mazuri baina yake na kocha Didier Gomes Morrison ambaye amekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba tangu ujio wa kocha Gomes alikorofishana na kocha huyo mfaransa baada ya kukataa kujumuishwa katika kikosi cha Simba kilichoipatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Africa Lyon katita michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam. Tangu hapo Morrison amekuwa akiwekwa nje ya kikosi cha kwanza na huenda asicheze mchezo wowote mpaka mwisho wa msimu......MWISHO WAKUNUKUU
Manara nae akajibu kam ifuatavyoo
Nanukuu
Tumekuvumilia mara nyingi sana lakini Kwa sasa uvumilivu umetushinda, Kwa nn kila siku ni ww tu kuiongopea Simba mambo ya uongo? Unaitumia mara kadhaa @wasafifm kuelezea migogoro hewa kuhusu Simba na kutaka kuichafua klabu yetu Kwa maslahi yako binafsi! Umekuwa ukifanya hvyo hata ktk Wall zako.
Utadhani Wasafi ni redio yako binafsi, Simba haitaki iandikwe na kutangazwa kwa mazuri tu, Waandishi na watangazaji haki ya kutukosoa Kwa mabaya pia kama tumeyafanya,,lakini haitavumilia tena story za uongo na kutunga ambazo hazina source,na zimejaa uzushi Ndugu yangu
diamondplatnumz ongea nae huyu mtu,tulio nje tunaona hana nia njema na ustawi wa uwekezaji ulioufanya ,nadhan nia yake ni kuona Wasafi fm inakuwa na ugomvi na Wanasimba,,na mm sitakubali kazi niliyopewa na klabu hii ichafuliwe na mtu huyo huyo kila siku,vinginevyo labda anataka Wanasimba waisuse kusikiliza hii redio,kitu ambacho mm ntakuwa mtu wa mwisho kukisema ,ukizingatia mahusiano yangu binafsi na ww.
But akiendelea kututangaza uongo na kuandika uongo juu yetu na wachezaji wetu,zipo hatua'Makhsuus'tutazichukua! Simba ni klabu kubwa mno haiwezi kumuogopa mtu mmoja Kwa chuki zake binafsi kutuchafua kila siku, Nipo hapa kuisemea klabu hii na kuitetea Kwa nguvu zangu zote hadi pale ukomo wangu utakapotimia , Na ktk kipindi changu mm kama head wa idara ya habari na mawasiliano kwenye klabu hii,„sitakubali story za upumbav na za uongo dhidi yetu Kwa sababu yoyote ile,Narudia tena hili likijirudia la uongo uongo iwe Kwa wachezaji,makocha au viongozi na hata timu Kuna hatua' MAKHSUUS' tutazichukua!!!
Simba ni klabu kubwa mno haiwezi kumuogopa mtu mmoja Kwa chuki zake binafsi kutuchafua kila siku, Nipo hapa kuisemea klabu hii na kuitetea Kwa nguvu zangu zote hadi pale ukomo wangu utakapotimia , Na ktk kipindi changu mm kama head wa idara ya habari na mawasiliano kwenye klabu hii,sitakubali story za upumbav na za uongo dhidi yetu Kwa sababu yoyote ile,Narudia likijirudia la uongo uongo iwe Kwa wachezaji,makocha au viongozi na hata timu Kuna hatua' MAKHSUUS' tutazichukua!!!
Nani miongoni mwetu atakaekubali taasisi anayoingoza ichafuliwe? Wanasimba hii ngoma kwanza niachieni mm,„labda huyu mtu hajajua how Simba is BIG Kaona tunapata matokeo kila mahali na kaona Simba imetulia anaanzisha uongo wake,Safari hii nnae na akibisha aendelee......MWISHO WAKUNUKUU
Mwamba kitengee nae akamjibu Kama ifuatavyoo
NISIKILIZENI NIWAAMBIE.
Nina miaka 20 kwenye Taaluma hii hivyo siyumbishwi na mtu huruma kwenye jamii. yeyote sababu ya Popote ninaposimama najivumia maisha na ufanisi kwenye kazi yangu, siogopi wafitini wala simuhofii mtu katika hili na nitasimamia ukweli.
Nataka nitoe elimu kwenye jambo moja, kutoa habari ndiyo kazi yangu na hii nina uhakika nayo. Kuna kijana mmoja, ana roho mbaya sana na anatamani watu wote duniani washuke wawe chini yake. Haiwezekani kwa mtu anayeitwa MAULID KITENGE. Hii inatokana na kukosa taaluma ya msingi ufanyaji kazi.
Inapelekea kujipendekeza kwa kuwachonganisha watu. Kama unataka utajiri muombe Mungu sio kuwa ombaomba kwa matajiri na kusema watu vibaya. Fitina ina mwisho, mwisho wake mbaya.
Kwangu mimi huyu ni mtu asiyejielewa na nitaendelea kufanya kazi kulinda heshima yangu. Nasema tena, muda mwingi anatumia kuwasema watu na kutaka kuwahujumu na Taasisi wanazofanyia kazi. Hili haliwezekani kwani hatupo tulipo.
Nasema tena, kujipendekeza kunawafanya watu wa aina hii kuwa roho woga pindi ukweli unapoongewa.
Uzi tayarii
Comment ziwe fupi