Ungekuwa mfuatiliaji wa michezo wala usingeshangaa alichofanya Manara kwahiyo si lazima kuwe na motivation behind! Kwanza, Kitenge ana ule uandishi wa uchokonozi. Ingawaje watu wanamtuhumu u-Yanga lakini sie wafuatiliaji tunafahamu ndo staili yake! Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita Kitenge aliwahi kushmbuliwa kwa maneno makali live (on air) ama na Mzee Mwanamkatwe au Ndolanga; sikumbuki vizuri!! Sasa tatizo la Manara anajifanya yeye ndo ana uchungu sana na Simba kuliko Dewji aliyeweka pesa yake matokeo yake, akiona watu wanaisema "vibaya" Simba lazima awashambulishie hata kama kinachosemwa ni cha kweli! Sasa kwavile Kitenge ana uandishi wa uchokonozi, na ukichanganya kwamba yeye ni Yanga basi ndo ndo hapo Manara anapokuwa kama Mwajuma Ndala Ndefu! Kuna siku aliwashambulia LIVE Watangazaji wa Wasafi hadi Kawambwa aka-mind vibaya sana baada ya kuwaita wapumbavu! Thanks to Edo Kumwembe akatuliza hali.
Tatizo lingine la Manara ndo ile kujifanya yupo karibu sana na matajiri ndo maana akianza kushambulia waandishi wa Wasafi, lazima amwinginze Diamond.