Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Wakuu

Naomba tishiriki kibwagizo hiki;-


"Samia jiuzulu Sasa nchi imeshakushinda,ulambaji asali umekuponza""!


"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!!
 
Watumishi wamenyamaza, hakuna anayeongea Kuhusu Maisha ya Wastaafu ambao kuanzia Mwezi huu wanapigwa Kikokotooo kwenye Pensheni zao.
 
hawa watumishi wanafaa wafukuzwe kazi, vijana wengi wenye sifa wapo mitaani wanasaka ajira, tusibembelezane.
 
Kamwe aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Pamoja na sifa na tambo zote walizofanya serikali kuhusu kuongeza mishahara wameishia kuongeza elfu 20,000?

Ikiwa ni muda mchache toka bank ya NMB kunipa notification ya mshahara kuingia na kufanikiwa kuona kilichoongezeka. Nimepigwa butwaa kuona tambo zote zile increment haizidi 20K!

Nadhani Sasa ni muda wa watumishi wa umma kujitambua na kuacha kushoboka na serikali. Serikali ime-inflate gharama za maisha kwa kiwango kikubwa but then haina efforts za kuboresha maslahi.

Maamuzi ya namna hii yanapunguza morali ya kazi na kushusha uadilifu. Tutegemee uzembe makazini na kuongezeka ubadhirifu.

Serikali imeshindwa kusimamia utumishi wa umma hususani kwenye suala la maslahi.

Mama anaupiga mwingi sana
 
Huna majukumu kijana tuliza kifurushi hicho
Kama kipato hakikutoshi kuliko makelele namatamaa acha kazi ukalime utapata sana nautakuwa tajiri huko tupishe nasisi uone kama jicho haliwi nyanya uiarikiri unapikia kuni mbichi
 
Wengine hakuna nyongeza hata ya sumni moja.
Ahadi ya Mheshimiwa Raisi imetimizwaje hapo ?
 
Hiyo nyongeza kaongezewa mama yako mzazi ndio kakuhadithia na wewe mwanawe ?
 
Kuna jamaa yangu kaongezewa elfu ishirini kwenye mshahara wake (20,000/=), halafu jumla ongezeko kwenye makato yake ni shilingi 7,900/=, kwa hiyo ongezeko la pesa kwenye take home ni sh 12,100/=. Hiyo ndiyo wanasema unapewa kitu kwenye mkono wa kulia halafu unanyang'anywa kwenye mkono wa kushoto!!

Sasa huyu hawezi kusema nimeongezewa sh 20,000/=, bali atasema nimeongezewa sh 12,100/= ambayo haitoshi kulipia hata kodi ya nyumba ya nusu mwezi!! USHAURI: Ongezeko la mishahara liwe linalenga kumwongezea mtu kwenye TAKE HOME CASH!!
 
Mama anaupinga mwingi sana
Inaelekea sarakasi lote liko mikononi mwa yule waziri wa fedha! Anakupa kiduchu anakinyang'anya sehemu ya hicho kiduchu unabaki na kiduchu zaidi kwenye take home!! Halafu anakutarajia upige makofi!
 
Back
Top Bottom