Mshahara wangu ni laki 3 kwa mwezi, nitumie shilingi ngapi kwa siku ili unitosheleze?

Mshahara wangu ni laki 3 kwa mwezi, nitumie shilingi ngapi kwa siku ili unitosheleze?

Jitahidi uwe unafunga, kula jioni tu.
Muda wako wa ziada jitahidi kutafuta kitu kingine cha kukuingizia kipato. Tafuta hata watoto wa majirani uwe unawapiga pindi. Anza kujibana na kufanya saving ili ufungue kiofisi cha kuku-boost
Hivi kwani pesa tunatafuta zanini yani nianze kufunga kula mlo mmoja kwa siku wakati pesa inatakiwa ikusave unaweza kutunza hiyo pesa na bado ukafa kizembe tu mie wacha nile vzr tu nachoamini pesa inatakiwa ikutunze muda wowote unapokuwa hai
 
Awapige pindi kwani umeambiwa mtoa mada ni ndugu yake na Mpwayungu Village ebu acheni kukariri maisha unadhani kufundisha ni kazi ndogo
😂😂😂 Bado hujayajua maisha wewe!!
Nakumbuka tuliwahi kufundishwa tuition na mwalimu ambaye sio mwalimu. Na hakuna aliyewahi kukosa akisahisha ila sasa yale majibu yahamishie shuleni ndio utajua hujui..!!
 
Hivi kwani pesa tunatafuta zanini yani nianze kufunga kula mlo mmoja kwa siku wakati pesa inatakiwa ikusave unaweza kutunza hiyo pesa na bado ukafa kizembe tu mie wacha nile vzr tu nachoamini pesa inatakiwa ikutunze muda wowote unapokuwa hai
Kwa kipato chake akisikiliza ushubwada wako basi week hamalizi hana hata mia
 
Kwa kipato chake akisikiliza ushubwada wako basi week hamalizi hana hata mia
Nyinyi mpotezeni mtoa mada mnadhani kushindia mlo mmoja kila siku ni kazi ndogo lazima ujali maisha yako kwanza kama unaingiza pesa unashindwa kula et sababu unasave pesa hv kutakuwa kuna maana gani ya kufanya kazi
 
Ni pesa mingi kabisa hiyo ila nimeona wengi hapa hawajawahi kuishi kwa mshahara huo ndio maana wanakupa figire za kufikirika usizoweza kuishi.
Ukiifata screenshot ya jamaa hapo juu utaishia kua na madeni tu, mwanaume unakuaje na pocket money ya 10k vocha, kuhonga, maji, dharula za hapa na pale utatatua vipi..
Kwanza kabisa set vipaumbele kwamba mwezi huu nalipa kodi/nanunua kitanda/nanunua feni au mazaga flani. Pesa inayobaki unafanyia matumizi mengine ikiwemo na msosi.
Piga bajeti ya kutumia 200k au pungufu ya hapo, inayobaki 50k save na 50k pocket money.

Kwa hii mishahara kodi unaisotea mwezi wa mwisho, usimuwekee hizo 40k kila mwezi mwenye nyumba utateseka sana.


Iko hivi..
Kwa mshahara wa namna hiyo huwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja, huwezi nunua hayo makitu yote kwa wakati mmoja, utafeli mapema sana.
Mishahara midogo mingi huishia kwenye msosi, ukiweza kujibana hapa umewini. Kama gesi ipo ndani nunua mchele kg hata 10 na unga kg 5.
Mafuta hata lita 1 na dagaa za kutosha utajipimia. Mpaka hapa msosi ushaua.

Mambo ya nyanya sijui vitunguu, carrit hizo ni anasa achana nazo kwanza.

Mpaka unafika miezi 4 geto utajikuta geto limekamilika kwa vitu vingi. Hapo sasa utasave pakubwa na utazingatia mlo kamili kama binadamu wa kawaida.
Umesema vyema kabisa.Naunga mkono na hoja
 
Wewe ndio umeongea mshangazi achana na Lamomy anataka kuuwa watu na njaa na ushauri wake wa kikatili
Mmh kushinda na njaa hapana asee atapata vidonda vya tumbo aanze tena kutafuta pesa ya matibabu.....

Sijui anafanya kazi gani mazingira gani, ila hapo hapo job anaweka aibu kando anawakaangia hata karanga za mayai hawezi kosa elf mbili mbili za chakula na nauli. (Karanga ni mfano ila vya kufanya ni vingi)
 
Inaweza kutosha kama ni bachelor na huna mambo mengi. Ili uweze kuwa na uhakika wa kumaliza mwezi mzima basi angalau on average kwa siku moja usizidishe shilingi 7,000/-

(Breakfast 1000, Lunch 2000, Dinner 2000, Nauli na Voucher 2000). Hapo maana yake usiwe na matumizi mengine ya ziada (yasiyo ya lazima). Hii itakusaidia walau kuwa na akiba kidogo mfukoni kwaajili ya dharura. Hapo tuki assume kuwa kodi, maji na umeme havipo kwenye hiyo hela.

Hapo sahau mambo ya kupiga gambe, kutembelea viwanja vikali na pia pisi kali utakula kwa macho labda upate wakukuhurumia tu.

Ila ndio harakati za maisha pambana kuna siku utatoboa jomba.
Hana haja ya kula mara tatu, breakfast na dinner ya mapema inatosha
 
Back
Top Bottom