Mshahara wangu ni laki 3 kwa mwezi, nitumie shilingi ngapi kwa siku ili unitosheleze?

Mshahara wangu ni laki 3 kwa mwezi, nitumie shilingi ngapi kwa siku ili unitosheleze?

Hana haja ya kula mara tatu, breakfast na dinner ya mapema inatosha
Inategemea na aina ya breakfast. Kama ni hiyo ya 1000 maana yake kikombe cha chai kimoja na mihogo vipande viwili. Hapo lazima mchana ale.

Tena kwa mshaharau huo ni lazima awe anafanya kazi ya manual work hivyo lazima anahitaji kula ashibe.
 
300k ni pesa ndogo sana, tijahidi tu kila mwezi save 50k hivi nyingine tumia tu hasa kuupa mwili pole hadi hapo mambo yatakapokua mazuri.! Huwezi kufanya chochote cha maana na hio pesa utapata pressure bure.
 
Tangu lini mshahara ukatosha? Wewe hakikisha tu mahitaji yako yote muhimu yanapatikana ndani ya mwezi. Imagine kuna wenzako wanalipwa mara 10 ya huo mshahara wako, na bado na wenyewe wanalalamika hautoshi!
Umeongea kikubwa sana mtani...unajua una akili sana sema tuu uko utopolo... 😆 😆 😆
 
Pole sana inawezekana uliona laki 3 ni pesa nyingi Anza kubana matumizi acha kununua bando acha kununua mavitu ya kula kula njiani sijui karanga au mahindi pesa yako itumike kununua chakula tu na nyingine sevu
Tumia 3500
 
Ni pesa mingi kabisa hiyo ila nimeona wengi hapa hawajawahi kuishi kwa mshahara huo ndio maana wanakupa figire za kufikirika usizoweza kuishi.
Ukiifata screenshot ya jamaa hapo juu utaishia kua na madeni tu, mwanaume unakuaje na pocket money ya 10k vocha, kuhonga, maji, dharula za hapa na pale utatatua vipi..
Kwanza kabisa set vipaumbele kwamba mwezi huu nalipa kodi/nanunua kitanda/nanunua feni au mazaga flani. Pesa inayobaki unafanyia matumizi mengine ikiwemo na msosi.
Piga bajeti ya kutumia 200k au pungufu ya hapo, inayobaki 50k save na 50k pocket money.

Kwa hii mishahara kodi unaisotea mwezi wa mwisho, usimuwekee hizo 40k kila mwezi mwenye nyumba utateseka sana.


Iko hivi..
Kwa mshahara wa namna hiyo huwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja, huwezi nunua hayo makitu yote kwa wakati mmoja, utafeli mapema sana.
Mishahara midogo mingi huishia kwenye msosi, ukiweza kujibana hapa umewini. Kama gesi ipo ndani nunua mchele kg hata 10 na unga kg 5.
Mafuta hata lita 1 na dagaa za kutosha utajipimia. Mpaka hapa msosi ushaua.

Mambo ya nyanya sijui vitunguu, carrit hizo ni anasa achana nazo kwanza.

Mpaka unafika miezi 4 geto utajikuta geto limekamilika kwa vitu vingi. Hapo sasa utasave pakubwa na utazingatia mlo kamili kama binadamu wa kawaida.
well said brother
 
#1.....30,000 toa Dhaka.

Sado ya mahand na kusaga 2300 wiki.
Dagaa WA 2000 wiki
Mafuta 2000 wiki
Viungo 2000 wiki
Mchele 1.5 3000 wiki. sio lazima super
Chumvi 500 mwezi
Sukar ya 3000 mwenzi
Viungo vya chai 1000 mwenzi

Total 14,800 per week.

Bila kutoa bidhaa za mwezi. 14800 * 4 = 59,200.
Ukiweka dharura ya 20,000 ukitokea hujapata Muda WA kupika, inakuwa 79,200.
Hela ya gesi 20000 nayo Ni ukitokea ndo umejaza.
#2..........Jumla 99,200/=

Umemaliz Kula mwenzi mzima.

#3........... 30,000/= kODI
#4.......... 20,000/= kusaidia wengne

Nguo najua zipo fua piga pasi.
Viatu vipo.... vya kiwi Ni Bora zaidi. Ni kung'arisha tu.

Kwa mwenzi
180,000/= Matumizi Tena hapa nimezidisha sana
120,000/= imebaki

ISHI LEVEL YAKO MKUU 300K na Malengo unatoboa.
 
Back
Top Bottom