Mshahara wangu ni laki 3 kwa mwezi, nitumie shilingi ngapi kwa siku ili unitosheleze?

Hana haja ya kula mara tatu, breakfast na dinner ya mapema inatosha
Inategemea na aina ya breakfast. Kama ni hiyo ya 1000 maana yake kikombe cha chai kimoja na mihogo vipande viwili. Hapo lazima mchana ale.

Tena kwa mshaharau huo ni lazima awe anafanya kazi ya manual work hivyo lazima anahitaji kula ashibe.
 
300k ni pesa ndogo sana, tijahidi tu kila mwezi save 50k hivi nyingine tumia tu hasa kuupa mwili pole hadi hapo mambo yatakapokua mazuri.! Huwezi kufanya chochote cha maana na hio pesa utapata pressure bure.
 
Tangu lini mshahara ukatosha? Wewe hakikisha tu mahitaji yako yote muhimu yanapatikana ndani ya mwezi. Imagine kuna wenzako wanalipwa mara 10 ya huo mshahara wako, na bado na wenyewe wanalalamika hautoshi!
Umeongea kikubwa sana mtani...unajua una akili sana sema tuu uko utopolo... 😆 😆 😆
 
Pole sana inawezekana uliona laki 3 ni pesa nyingi Anza kubana matumizi acha kununua bando acha kununua mavitu ya kula kula njiani sijui karanga au mahindi pesa yako itumike kununua chakula tu na nyingine sevu
Tumia 3500
 
well said brother
 
#1.....30,000 toa Dhaka.

Sado ya mahand na kusaga 2300 wiki.
Dagaa WA 2000 wiki
Mafuta 2000 wiki
Viungo 2000 wiki
Mchele 1.5 3000 wiki. sio lazima super
Chumvi 500 mwezi
Sukar ya 3000 mwenzi
Viungo vya chai 1000 mwenzi

Total 14,800 per week.

Bila kutoa bidhaa za mwezi. 14800 * 4 = 59,200.
Ukiweka dharura ya 20,000 ukitokea hujapata Muda WA kupika, inakuwa 79,200.
Hela ya gesi 20000 nayo Ni ukitokea ndo umejaza.
#2..........Jumla 99,200/=

Umemaliz Kula mwenzi mzima.

#3........... 30,000/= kODI
#4.......... 20,000/= kusaidia wengne

Nguo najua zipo fua piga pasi.
Viatu vipo.... vya kiwi Ni Bora zaidi. Ni kung'arisha tu.

Kwa mwenzi
180,000/= Matumizi Tena hapa nimezidisha sana
120,000/= imebaki

ISHI LEVEL YAKO MKUU 300K na Malengo unatoboa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…