Mzuka wanajamvi
Kamwe usingewaza tukio kama hili kutokea Uswizi. Korona (pathetic virus) imeleta shida kwa kipindi kifupi sana.
View attachment 1446109
Yani watu Uswizi wanapanga foleni ndefu tena ya zaidi kilometre moja kupewa chakula cha bure tena wanawahi kupanga mstari kwaanzia saa kumi na moja asubuhi.
View attachment 1446109View attachment 1446113
Kwa sasa hivi Uswizi imethibitisha watu 30, 305 wana maambukizi ya korona na vifo ni 1800.
View attachment 1446121
Uswizi ni nchi inayoongoza kwa maisha bora na malipo mazuri ulaya na duniani hata kwa wabeba boksi.
View attachment 1446118
Hata kwenye kati ya jiji Tajiri duniani Geneva hali ya uchumi imedorora na imeleta hali ngumu ya kiuchumi kwa watu waliokuwa wanafanya kazi kwenye housekeeping, hoteli, migahawa, kilimo na ujenzi