Mshtuko mkuu ndani ya CCM. Ushindi wa Lissu na Heche ni chanzo. Je, Mungu anaifuta CCM?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Duru za ndani ya CCM zinanyetisha kuwa hali ya mtafaruku na mfadhaiko mkubwa imeikumba CCM kutokana na pigo takatifu la ushindi wa Tundu Lisu na John Heche katika uchaguzi wa CHADEMA taifa.

Vikao vya wakubwa vimekuwa haviishi, na kupelekea kuleta hofu inayoweza kuzua mpasuko mkubwa wa ndani ya chama.

Azimio la Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 19 Januari 2025 ukumbi wa White House Dodoma, ulipitisha jina la Samia kama sole contenstant na jina la John Nchimbi as running mate wake kwa nafasi ya umakamu. Azimio hili tayari limeshaonesha kuleta mpasuko wa ndani. Juhudi za vikao, kubembelezana na hata kutishiana zimekuwa zikiendelea ndani ya Chama ili kupunguza madhara ya msuguano uliosababishwa na uvunjivu wa Katiba na kanuni za chama.

Inasemekana, upo uwezekano wazee wa kazi chafu wakapewa orodha ya watakaoshughulikiwa ili mifumo iwabane kiuchumi au kuwawekea mazuio muhimu au hata kukabiliwa na changamoto ya maisha yao (kinga ya wale jamaa itahusika kutekeleza hili).

Hotuba ya Tundu Lisu hususan alipokuwa anateua Sekretarieti mpya CHADEMA, ailitamka kuacha nafasi moja ya uteuzi wa mjumbe, akielezea uwezekano wa kupokea wageni kutoka chama dola ambapo hilo lipo wazi hadi sasa.

Jambo linalochagiza wanyetishaji kupata nguvu ya hoja ya mpasuko wa ndani, ni kitendo cha CCM na viongozi wake wote kutosema lolote kuhusu Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CHADEMA. Hata Mwenyekiti wa CCM hajasema lolote hadi sasa hivyo hofu na uoga vinazidi kuongezeka ndani ya korido za Lumumba.

Ushindi wa Lisu na Heche umeleta hasara kubwa na unaweza kupelekea mabadiliko makubwa serikalini na kitengoni kutokana na uwekezaji mkubwa kufanyika na kuambulia kuvuna mabua. Inasemwa na wapenda haki ndani ya CCM kuwa, pesa iliyotumika kwenye uchaguzi wa CHADEMA ni hasara na pigo kubwa sana dhidi ya CCM na Serikali. Kitendo cha polisi kushindwa kulazimisha (mbinu za vurugu) ushindi kwa mapandikizi ya CCM ndani ya CHADEMA ni dhahiri kuwa mfumo umecheza ngoma kubwa kuliko uwezo wake. Msemakweli ndani ya chama dola anasema, kitendo cha wawakilishi wa Kibalozi ndani ya Mkutano Mkuu hadi mwisho wa zoezi la uhesabuji wa kura na uwepo wa kundi kubwa la wananchi kuzingira ukumbi wa Mlimani City ambao walikesha siku zote za Mkutano hadi ulipofungwa tarehe 22 January 2025 usiku, ulisababisha nyenzo za kuvuruga uchaguzi wa CHADEMA ziendelee kubaki salama ndani ya magari ya polisi 19 yaliyozingira eneo hilo wakiwa na silaha kali.

MY TAKE

  1. Mungu anaifuta CCM kwa kasi kubwa na hakuna wa kuzuia
  2. Ushindi wa Lisu na Heche ni mpango wa Mungu
  3. CCM ipo hatua moja kukaribia kishindo cha MPASUKO wake
  4. Rushwa na mbinu zote chafu za ndani ya chaguzi za Chama vimekuwa kansa isiyopona na kuzalisha makundi na manung'uniko ndani ya chama.
  5. CCM ijiandae kisaikolojia kwa uchaguzi mkuu ujao kwani umma umeshaamka kupitia matukio yaliyojiri kuelekea uchaguzi wa CHADEMA ambao ulifunika kwa mbali sana mkutano mkuu wa CCM ambao umemalizika kwa kuongeza ufa wa mpasuko unaoendelea chamani
 
Amen
 
Kwa hii safu mpya ya CHADEMA, maCCM lazima waweweseke tuhakuna namna. Na bado.
 
Back
Top Bottom