Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

M
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Mnaongea vitu ambavyo hamjui kweli nimeamini jamii forum ni forum ya walala ho,wanafiki,wazandiki na wajinga hauwezi ona mtu anauejielewa akitumia huu mtandao wa kipuuuzi! I' m off mbakie wapuuzi wenyewe
 
sikia rafiki yawezekana wewe hujui,jk kwenye issue ya lowassa alifanya sawasawa na wala hana baya lolote alilofanya,sasa kuhusu haiba yake,wajihi wake,jk anaumwa kansa ya tezi dume hivi unategemea awe na nguvu vipi?,umri
🚮
 
Kikwete aliingia madarakani Kwa nguvu ya lowasa na wenzie, umoja wao ulipewa jina la Boyz 2 men. Na walikubaliana kuachana kit kikubwa. Sasa mkwele alipoona mwenzie ana ushawishi mkubwa serikalini akaanza wivu.inakuwaje Waziri mkubwa anasikilizwa kuliko mkuu wa nchi, Sasa ilipotokea zengwr la Richmond mkwele akawapanga wadau Ili mamvi aporomoshwe kutoka kileleni , alivyo mjanja akakaa pembeni akimwacha rafiki yake asulubiwe.
Wakati w kugombea urasi ndani CCM, jina lake likatupiliwa mbali chini ya mkwele
 
Kikwete ni rafiki wa Hayati Lowassa au familia ya Lowassa? Asiyejua maana haambiwi maana..

Kama Kikwete na Lowassa ndio walikuwa marafiki ,familia hata imtaje au isimtaje haifuti urafiki wao na pia familia ndio inatakiwa itambue ni Kikwete ndio amefanya mzee akazikwa kwa heshima hivyo Kwa sababu ya kuteuliwa Uwaziri mkuu.

Kama utaendelea kushabikia vitu vidogo vidogo na kuacha kujadili mambo makubwa tutakuwa hatuna namna zaidi ya kukupuuza
Lowasa ndio alifanya kikwete kuwa raisi usisahau hilo
 
Umeongea hisia zako tu. Nampenda Lowasa ila JK ni chuma cha pua. Yote uliyoandika ni yale ulitamani kuona yanatukia ila hakuna hata moja
Hakuna wa kumpuuza JK.
Ni umbeya tu wa watanzania walio wengi wa sio na shughul za kufanya ndio wamekua na mawazo kama haya
 
Kikwete hakuwa pale kwa ajiri ya kugawa uraisi
Sijasema Habari ya uraisi nimesema kuhusu utendaji kazi mzuri na Uongozi imara .
Wala sipo Kwenye malumbano ya kukatwa jina au la ,hayo nawaachia wenye ccm Yao .
Mimi ni independent voter yoyote mwenye kufanya kazi nzuri za maendeleo ya Ustawi wa jamii na nchi namuunga mkono .
 
Shida lowasa alikuwa mwizi
 
Mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa muda mfupi lakini angalia muitikio na namna msiba wake ulivyokuwa ndipo utakapojua JK aliona mbali kwamba marehemu alikuwa na nafasi kubwa ya kumfunika kwa kila kitu ndipo akafanya ya kufanya.

Pumzika kwa amani Lowassa, Mungu amekuinua katikati ya watesi wako hata katika msiba wako.
Hakuna hiko kitu, nguvu yake ya pesa ndio ilimpa wafuasi
 
sikia rafiki yawezekana wewe hujui,jk kwenye issue ya lowassa alifanya sawasawa na wala hana baya lolote alilofanya,sasa kuhusu haiba yake,wajihi wake,jk anaumwa kansa ya tezi dume hivi unategemea awe na nguvu vipi?,umri pia umekwenda hawezi kuwa mkakamavu,hebu tumwache jk please
Na bado angeonekana imara na mwenye bashsha anhesema kafurahi kumuona Mzee Lowassa kafariki. Achana na hao binadamu!
 
Shida lowasa alikuwa mwizi
Lowasa alifanya kazi nzuri , kanda ya ziwa wanamkumbuka kwa kutatua tatizo la maji,uanzishwaji shule za kata , alisimamia ujenzi wa taasisi ya moyo muhimbili, mloganzila, udom nk
Nadiriki kusema Tz tungeongozwa na Masai sokoine au lowasa tungekuwa mbali sana kimaendeleo .
Hawa ni watu wa maamuzi magumu .
 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
ni gunia zito sana, masaa machache yale alihisi kama ni miaka kadhaa. imagine!
 
Kwa hiyo mlotaka ampe urais kisa ni rafiki yake? Thank u kikwete uliangalia maslahi mapana ya nchi kuliko kujali uswahiba nchi itumbukie shimoni japo jpm ndo alikuwa rais mbovu sana kuwahi kutokea Dunia hii
ila yeye alimpigania akaupata uraia kwasababu ni rafiki yake, na alitumia hadi pesa yake ya mfukoni wakati huo msoga hakuwa na mihela waliyo nayo sasaivi. sema mwanadamu akipata huwa anasahau alikotoka.
 
Back
Top Bottom