Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Leo nimemuona Kikwete pale kwenye msiba Monduli. Hali yake haikuwa ya kawaida kabisa na mwishowe aliondoka na sijui hata alipoenda.

Sasa sijui alikuwa na tatizo la kiafya au ni kitu gani? Alikuwa hawezi kukaa kwa utulivu kwenye kiti chake. Na sura yake ikionyesha kama vile alikuwa na maumivu flani.

Mwili wake ulikuwa una swing back and forth akiwa amekaa kwenye kiti. Na ni jambo ambalo naona kama alikuwa akishindwa kuji control. Baada ya muda kile kiti chake kilikuwa wazi kabla hata Rais hajaondoka. Kwasababu kiitifaki, hakuna anayeruhusiwa kuondoka kabla ya rais.
Pengine alikua amebanwa na mkojo kwa muda mrefu.
 
Kwa hiyo ulitaka awe anatabasamu mje mseme mzee wa msoga kafiwa na rafiki yake kipenzi ila anacheka cheka tu. au ulitaka atajwe ili nini?.

Tujifunze wakati mwingi kufanya mambo bila kutaka umma usikie, laylow kwenye mambo mengi itakusaidia sana.

Wewe hujui kuwa wanaosimamia mienendo ya hii nchi wangeweza kuhoji na kidadisi kutajwa kwa JK kama ambavyo sasa hivi wanahoji na kudadisi kutokutajwa kwake. Sasa kipi bora hapo?.

Usishangae ukakuta ni JK wenyewe kaomba asitajwe popote na familia kwenye shukrani, kwani sadaka haihitaji kutajwa kwa wanadamu.

Ukijifunza mfumo wa maisha wa JK na wa EL uka mix pamoja ukapata hybrid utafanikiwa sana mambo yako iwe biashara, siasa au kuishi na jamii na hautashangaa kwanini hajatajwa.
 
Kama ulisikia hotuba ya Chegeni kule kanisani Azania na shangwe alizopigiwa na watu wote pamoja na wanafamilia, na leo ameitwa mwanafamilia. Lakini pia Bashe aliyemtemea nyongo Jk baada ya kumkaribisha tena Lowassa ndani ya CCM anavyopendwa na familia. Utaelewa familia inavyomchukulia swahiba wa zamani wa marehemu.
Ngoja niitafute utube
 
Anayetoa Urais siyo Kikwette bali ni kra za wananchi. Yeye kama Mwenyekiti wa CC ya CCM alihusika kupitisha majina 5 na kumkata Lowassa. Aliwaweka Bemard Membe, January Makamba, Magufuli, Migiro na Amina Salum.

Kama una akili utagundua kuwa January Makamba au Amina Salum hawakuwa na CV ya kumpita Lowassa
Kilichomuangusha Mwanangarash ni tuhuma mbaya za ufisadi.
Hata Kikwete alishawahi kulisemea hili siku ile ya mwisho ya Kampeni.
Alisema chama kingepata shida sana kwenye kumtetea na kumnadi.
 
Hakuna kitu kama hiki. Wana ccm ndio walifanya JK awe Rais.
Ni kweli. Nakumbuka zile kampeni za Kikwete awamu ya kwanza ya Urais zilipendeza na dunia nzima ilijua kuwa Tanzania kuna demokrasia na kwa mara ya kwanza nilisikia usemi wa "Chaguo la Mungu". Watanzania kumbukumbu zetu ni fupi sana!
 
Sasa Bashe na Huyo Chegeni na JK, mbona ni mbingu na ardhi, Huyo Bashe JK ndio alimleta kwenye kalamu God father wake anayemfanya aishi mjini.

Marehemu angekuwa na nguvu hiyo sidhani kama alipaswa kumtegemea JK ili awe Rais, angeweza pia kumzunguka na kujiweka kitini.
BWM aliweza kuzungukwa JK akawa Rais na sio SAS, basi EL naye angetumia nguvu hiyohiyo kujifanya Rais baadala ya JK.

Sasa kama alikuwa superpower na hela + rafiki yake RA walishindwaje kumzidi kete JK pale Dodoma na watu wao akina Sofia, Madabida, Nchimbi, Msindayi nk?
Jitahidi ujifunze, upate maarifa. Hakuna Rais anaejiweka Kitini.
 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Sawa ila tusioneane haya na kuacha upuuzi uendelee kisa kujenga ushwahiba.

Hata hivyo kwani Kikwete amekosea nini kwa Lowassa?
 
Mwenyekiti ndiye anateua watu wanaounda kamati kuu

Na lazima ateue wanaimtii
Mwenye mamlaka ya kukata majina ya watu kamati kuu ni JK (mwenyekiti ) peke yake?

Una ushahidi gani usio na shaka unaoonyesha EL alishinda uchaguzi na sio JPM? Tume ya uchaguzi Tanzania ilimtangaza JPM na sio EL.

Kukamatwa wajumlisha matokeo ya uchaguzi ni suala la dola na mamlaka zake, una uhakika gani kama hao watu hawakuwa wajumlisha uchaguzi bali walikuwa wanamanipulate kura.

Tujiepushe sana na "hearsay" za mitaani, maana Kila mtu anaweza kuongea la kwake ilimradi linamfavor na kumfurahisha yeye.

Toka 1995 mpaka uchaguzi wa mwisho 2020 wapinzani hulalamika wameibiwa kura na matokeo ni kwamba wameshinda, kuanzia Lyatonga Mrema mpaka TL, lakini ukijaribu kuutafuta ukweli unakutana na "hearsay" na story za vijiweni tu.

2025 tunakwenda kwenye uchaguzi mwingine huku tukilalama tume sio huru na blah blah nyingi halafu tukishindwa tunasema tumeibiwa kura, kwanini tusihakikishe tume inakuwa huru na Kila kitu tunajiridhisha nacho ndio twende kwenye uchaguzi ili tuepuke maneno ya tumeibiwa kura.
 
Mwenyekiti ndiye anateua watu wanaounda kamati kuu

Na lazima ateue wanaimtii

Unajua Kuna kitu kinaitwa CCM inner circle aka CC ya CCM wanakaa kwanza wazee kujadili?
Unajua Kuna kitu kinaitwa system ambayo imeweka macho yake CCM kuhakikisha anapatikana mtu sahihi?
 
Kilichomuangusha Mwanangarash ni tuhuma mbaya za ufisadi.
Hata Kikwete alishawahi kulisemea hili siku ile ya mwisho ya Kampeni.
Alisema chama kingepata shida sana kwenye kumtetea na kumnadi.
Uwongo wake tu. Huo ufisadi wa Lowassa unatajwa tu kuwa ni ufisadi lakini hatuambiwi ni wapi aliiba hizo hela. Kaa mfano ufisadi wa JK kwenye ESCROW account ya TAMESCO JK alichukua pesa Stanbic kupitia kwa Harbinder Singh
 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Lowasa alitaka kumuingiza chata JK kwenye makundi ya wezi (ingawa Lowasa mwenyewe alikuwa muadilifu ila makundi ya nyuma yake yalikuwa ya wezi).
 
Ilikuwaje waziri mkuu Kubabaika sana kutamka, "Jina la Bwana lihimidiwe" 🤔
 
Kikwete ni rafiki wa Hayati Lowassa au familia ya Lowassa? Asiyejua maana haambiwi maana..

Kama Kikwete na Lowassa ndio walikuwa marafiki ,familia hata imtaje au isimtaje haifuti urafiki wao na pia familia ndio inatakiwa itambue ni Kikwete ndio amefanya mzee akazikwa kwa heshima hivyo Kwa sababu ya kuteuliwa Uwaziri mkuu.

Kama utaendelea kushabikia vitu vidogo vidogo na kuacha kujadili mambo makubwa tutakuwa hatuna namna zaidi ya kukupuuza
Ulichoandika Ni sawa na kusema Yesu ndio kampa Mungu umaarufu
 
Back
Top Bottom