Msidharau BIMA za watoto wapendwa, ni muhimu sana kwa watoto zetu

Msidharau BIMA za watoto wapendwa, ni muhimu sana kwa watoto zetu

Sio kweli kuwa kila ugonjwa hutibiwa bure kwa BIMA yako.
Mimi mwanangu anaumwa pumu kila ikimpanda nikienda hospital kuna baadhi ya huduma naambiwa hazipo kwenye BIMA hivyo inanilazimu kutoa pesa mfukoni.
Duh, pole mm wangu analo tatzo kama hilo alilazwa BOCHI siku 2, hakuna hata kimoja nilicholipia au inategemea na bima
 
Na gharama za mtu mzima ni kiasi gani mkuu?yaani kwa mtu mwenye shughuli zake na sio mwajiriwa(kukatwa kwny mshahara).
Vipo vya aina 3

1.192,000
2.384,000
3.587,000

Hizo ndio gharama za bima za MTU mzima mkuu NHIF
 
Hebu JAmani fikirieni kipindi hiki umpeleke mtoto hospital halafu uambiwe ili tatzo lake liondoke inahtajika mil.3 na upuuzi wake kama sio kutaftiana kuhara ni nini?

Jamani nimetokea kuheshimu BIMA aseee nawasisitiza BIMA jamani,unaweza kwenda hospital ukfkiri unaumwa JINO daktari anakucheki anakwambia MDOMO mzima meno ni ya kureplace hahaha inahtajika 7Mil otherwise mapengo yanakuja very soooon.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Duh, pole mm wangu analo tatzo kama hilo alilazwa BOCHI siku 2, hakuna hata kimoja nilicholipia au inategemea na bima
bima za watoto hulipiii hata senti huwa zina cover kila kitu.
 
Asante sana mkuu, zamani nilikua Jubilee Insurance kabla sijatoka kwny ajira kwenda kupambana mtaani.

Nitaenda kuwaona NHIF.
Jubileee unatibiwa baadhi ya hospital tu sio hospital zote wanapokea wanachama wa jubilee.

Kama mtu uko serious na afya yako na hutaki mbwembwe nyingi,NHIF yako inakutosha kabisa kabisa.
 
Jubileee unatibiwa baadhi ya hospital tu sio hospital zote wanapokea wanachama wa jubilee.

Kama mtu uko serious na afya yako na hutaki mbwembwe nyingi,NHIF yako inakutosha kabisa kabisa.
Ntazingatia ushauri wako,thnxs mkuu.
 
Mkuu asante kesho nafuatilia cheti cha kuzaliwa nimkatie dogo Bima
 
VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYAView attachment 1697526
20200706_081602.jpg
 
Sijui niseme nini kwa wale wazazi mlio na watoto wa chini ya 18yrs na hamjawakatia BIMA bei ya bima ya mtoto ni 54,000 tu kwa mwaka mzima,mtoto anatibiwa kwa BIMA ugonjwa wowote utakaokatiza mbele yake.

Kwann nasema hivi, nina mwanangu wa kiume umri wake wa kwenda mfanyia circumsission/kumtahiri (3yrs) ukawadia nikajisemea ngoja nimpeleke mwanangu akafanyiwe kitu nijue akishapona basi nimuanzishe shule akacheze cheze huko.

Basi nikafika hospital daktari akahtaji muona mtoto na kuona uume wa mtoto,akamshika kisha akawa ana mminya minya kwenye korodani,Nikashangaa sana daktari ananiambia "mbona mtoto ana korodani 1?"

nikatoa macho! akasema hatuwezi mtahiri mtoto akiwa na korodani 1 n lazima tuishushe maaana itakua imebaki tumboni haijashuka, na ikishndkana basi tuitoe kabisa maana kuicha ndani n hatari sana kwa mtoto kwa huko mbeleni.

Basi tukaambiwa tulazwe,nikalazwa na mwanangu Mtoto akaja akafanyiwa operation korodani ikashushwa kisha akatahriwa...

Baada kama ya wiki nzima kuspend hospital,ukafka muda turuhusiwe sasa tukajiuguze nyumbani tuwe tunarudi clinic tu kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo ya vidonda vya mtoto.

Nikapewa discharge form na maform mengine mengine,kwakua kote huko BIMA ilikua inafanya yake,mimi nilikua na deal na malipo ya MSOSI TU.

My dear form ya gharama ikaonyesha total charges zote ni 3,210,000 Tsh yaani Milioni 3 na laki mbili na ishirini na moja.

Hebu JAmani fikirieni kipindi hiki umpeleke mtoto hospital halafu uambiwe ili tatzo lake liondoke inahtajika mil.3 na upuuzi wake kama sio kutaftiana kuhara ni nini?

Jamani nimetokea kuheshimu BIMA aseee nawasisitiza BIMA jamani,unaweza kwenda hospital ukfkiri unaumwa JINO daktari anakucheki anakwambia MDOMO mzima meno ni ya kureplace hahaha inahtajika 7Mil otherwise mapengo yanakuja very soooon.

Kuna.magonjwa mengi sana wapendwa tusiyoyajua hii dunia,kama hii ya korodani kubaki tumboni ndio kwanzaaaaaaa limekua brand new maskioni mwangu.

Anyway Narudia tena kuwasisitiza BIMA jamani kwa mnaoweza msipuzeeee msipuuzeee.

Asikiae na Asikie.
Sikuiz bima 194,000 per person ,achana na hbr za 54,000/-... Nina mapacha under 1 year..
 
Hili naloo neno,Kama kipimo tu Cha kuangalia gono au kashwende wametoa iwejeee wawezee kuweka operation
Wanakwepa majukumu yao mengi tu ila wana matumizi makubwa sana ya fedha kwenye kujilipa na kununua mashangingi
 
Back
Top Bottom