Msidharau BIMA za watoto wapendwa, ni muhimu sana kwa watoto zetu

inategemea ulikata bima gani mkuu,si kila bima ina tibu magonjwa yote na kupata dawa zote

BIMA zipo kwa makundi mkuu
Pamoja na hayo michango ya wanachama haiwiani na huduma wanazotoa
 
Hiyo Bima umekata mwenyewe au umelipiwa na kampuni alafu unakuja kutueleza huku, ukiachana na wafanyakazi wa serikali wenye NHIF ni wa TZ wangapi wanaomudu bima ya afya kwenye kampuni kama Jubelee, AAR, Resolution, Strategies nk? mtu kodi ya nyumba ya elfu 50 ni mtihani atapata milioni ya kudepost kama insurarence? USA tu kwenyewe serikali inawalipia watu wake bima ije iwe hapa kwetu ambapo tuna uchumi wa flyover na SGR?????????????
Shukuru Mungu kama unabahati ya kulipiwa hiyo bima na kampuni, make NHIF yenyewe ni shida tu, kila ukienda kwenye matibabu utaambiwa hayo hayako covered kwenye bima, hizo dawa haziko covered kwenye bima. Maisha yetu watanzania tunayajua wenyewe.
 
kuna bima ya afya iliyoboreshwa kifupi CHF. hii ni 30,000/= kwa mwaka kwa watu 6. Unatibiwa zahanati na hospitali ya wilaya. Tushindwe kukata hata hii??
Nielekeze vyema mkuu wangu
 
Mi Kuna mtu wangu wa karibu nasumbuliwa na maumivu ya mgongo mwaka wa pili huu kila wiki anaenda clinic Mara mbili na kila hitaji la muhimu anapewa bure hudma nzuri gharama zake kanipigia hesabu inakaribia 7M tangu alipaoanza lakin hajatoa hata shilingi mia ni bima tu inamsaidia dah
 
Bima wanashindwa kulipia ampicloxy tu wanasema haipo kwenye mpango wa bima hiyo ya kushusha korodani wataiweza?

Sijajua ni BIMA gani ila bima nyingi hata dawa za elfu 50 tu wanashindwa kutoa!! BIma nyingine wanakwambia usiende Aghakhani nenda Dispensary ,sasa maaana ya BIMA ni nini? Navyojua Kama BIMA ya Gari ukila mzinga mkubwa wanareplace gari,sasa BIMA hizi uchwara uchwara masharti kibao,mara subiri kwanza tupie simu ,mara jino halipo kwenye BIMA,mara umesahamaliza pesa yako ya BIMA yaani haileweki.

Sidhani Bima ya elfu 54 hizi zetu za kiswahili upate huduma za kutosha.
 
Bima ni wezi tu binafsi sijaona umuhimu wao
 
inategemea ulikata bima gani mkuu,si kila bima ina tibu magonjwa yote na kupata dawa zote

BIMA zipo kwa makundi mkuu
Mkuu nilisikia bima ya NHIF walisitisha kupokea wateja wapya kwa muda,hii habari ya ukweli au stori tu za mitaani?
 
Pesa ni Muhimu lakini BIMA ni muhimu zaidi
Kwa hio Bakhresa,MOE wana bima za afya? Sijakwambia Bima ndio sio muhimu, ila bima ni mpango maalumu kwa masikini wasio na kipato cha uhakika.
Tafuta pesa, kuna watu wengi hawana bima ila wanamiliki pesa kwa hio afya ikiwasimbua kidogo tu india au ulaya kwenda checkup.Tuhamasishane kutafuta pesa,pesa ndio kila kitu bima sio kila kitu.Bima haiwezi kukupeleka India kutibiwa.
 
sawa
 
sawa
 
Jubileee unatibiwa baadhi ya hospital tu sio hospital zote wanapokea wanachama wa jubilee.

Kama mtu uko serious na afya yako na hutaki mbwembwe nyingi,NHIF yako inakutosha kabisa kabisa.
hospitali zote kubwa hupokea Jubilee. NHIF inakataliwa Agakhan kubwa zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…