Abaraham ni baba wa mataifa mengi.... Ni makosa sana kujimilikisha Canaan ni ya Waisrael kisa tu aliishi Abraham. Abaraham alikua na uzao mkubwa sana hapo middle east sasa kivipi tena Yakobo pekee ndio adai umiliki??? Vipi kizazi cha Ishmael au Esau na wenyewe hawana haki ya Canaan??
Anyway Abraham alitokea Ur iloyopo Sumeria ya kale/Mesopotamia. So still hakuwa mtu wa kwanza kukanyaga hapo Canaan na ndio maana hapo Jerusalem tayari kulikua na mfalme Melchizedek aliyemlaki baada ya vita ya Abraham na Neodechlaomer
soma Biblia we mwenye kichwa kizito. Biblia ndio inasema hivyo, Ibrahim alikuwa na watoto wawili tu, Ishmael mtoto wa kambo aliyezaa na Mmisri, na Isaka mtoto wa ndoa aliyezaa na Sara. awali alitaka kumpa urithi na mbaraka Ishmael kwasababu ni mtoto wa kwanza, lakini Mungu akasema "hapana" utazaa mtoto, yaani Isaka huyo ndiye atamiliki. Ishmael alifukuzwa nyumbani kwa Ibrahim akiwa na mamake Hajir, wakaenda huko jangwa la arabuni na wakawazaa waarabu. baraka pekee aliyopewa ni uzao mkubwa na ndio maana waarabu ni wengi mno.
huku nyuma kwenye ndoa Mungu aliendeleza uzao wa Isaka akazaa mapacha, Esau na Yakobo, Esau ni baba wa wazungu wakati Yakobo ni baba wa Wayahudi/waisrael, tunasema ni baba wa waisrael kwasababu Yakobo alibadilisha jina akaitwa Israel na alikuwa na watoto wa kiume 12 waliokuja kuleta koo 12 za Waisrael hadi leo hii na ndio makabila yao.
Yakobo alizaa mtoto aitwaye Yusufu aliyeuzwa utumwani misri, kule alikuwa waziri mkuu hukohuko utumwani na Yakobo na familia yake wanaondoka Caanan ambako walikuwa wanaishi wakaenda misri, kule walizaliana mno wamisri wakaogopa watapinduliwa wakaamua kuwabadilisha wawe watumwa. wakatesa miaka 400. Musa akazaliwa miongoni mwao.
Musa aliagizwa na Mungu awachukue waisrael wote awarudishe kwenye nchi yao ya ahadi, Kaanani, nchi ambayo Mungu alikuwa amempa babu yao Ibrahim na akaahidi kuwa kizazi chake kupitia Isaka ndicho kitakachorithi pale, ndio wakaanza safari ya jangwani kwa miaka 40 hadi Joshua alipowafikisha kaanani.
pale kaanani baada ya kuondoka miaka 400 iliyopita walikuta kuna wafilist wamevamia (wapalestina wamevamia), Mungu akawaelekeza wawaue wote, lakini waisrael hawakuwaua, Mungu akawaambia hao watakuwa mwiba kwenu maisha yenu yote, na ndio maana hadi leo hii wafilisti/wapalestina ni mwiba kwa waisrael.
ukiangalia falme zote zilizopita kabla ya Daudi, walikuwa wanapigana na hawa watu. tuanzie kwa sauli tu, then Daudi, then nabii Samson na baadaye suleiman. walikuwa wanapigana na WAfilisti mara kwa mara na ulikuwa kama mchezo wa simba na yanga, mtu akipata nguvu tu anatangaza vita wanapigana atakayepigwa basi, siku nyingine tena hivyohivyo. na vita hiyo haitakuja iishe hadi Yesu atakaporudi.
Ibrahim alipewa eneo sio hilo tu, bali hadi maeneo ya karibia na Syria, jordan yote, lebanon yote ni mali ya israel Kibiblia, na kuna siku yatakuja kutwaliwa yote kama ilivyotwaliwa golan. Jordan inaogopa sana israel kwasababu wameshasoma mistari ya kwenye Biblia/Torah, na wanajua wakikinukisha israel inaweza kuwashambulia ikapora maeneo kama ilivyofanya kwa Golan heights kwasababu wayahudi wanaamini ni yao, na ni imani sahihi. hiyo ni chai tu, ufafanuzi zaidi siku nyingine.