Msimamo mkali wa Lisu ndio uliomfanya Mbowe atoke gerezani

Msimamo mkali wa Lisu ndio uliomfanya Mbowe atoke gerezani

Hayo ni malidhiano ni kuwa chawa, watu wanatekwa, wanakufa,alafu unaita malidhiano, huo ni usaliti kwa taifa
Kwani hao wanaofanya hivyo mtawafanya nini?.Lissu mwenyewe kaishia kubweka tu pembeni bila kuchukua hatua yoyote ngumu ili apate haki kwa waliomdhuru wawajibishwe.sana sana atapanda ndege akalalamikie kwa wazungu ambao wala hawana masaada wowote.Njia sahihi ilikua hiyo hiyo ya mazungumzo kwasababu chadema haina nguvu yoyote ya dola yakupambana na wadhalimu wenye dola inayopokea kila amri yakuumiza watu.
 
Mkuu kila jambo linamwisho wake, haki ya mtu hajai kipotea ila chelewa tu
 
H
Jamani Lisu ni hazina ya taifa,
Ni Tunu ya taifa, Lisu ndio mtu aliejitoa kwa ajili ya kupigania haki ya kweli kwa Tanzania. Amejotoa kimwil,kiroho,kiakili kwa ajili ya ukombozi wa watanzania.
Bila msimamo mkali wa Lisu Mbowe angekuwa BAdo yupo gerezani mpaka leo, Lisu ndio alimwambia rais mtoe kwanza Mbowe ndipo tuendeleee na maridhiano.
Wapiga kura ndani ya chadema mpeni kura za ndio lisu kwa ajili ya masilai mapana ya taifa letu pendwa la Tanzania. Haki HUINUA TAIFA. RUSHWA NI ADUI WA HAKI. lisu ni mpango wa Mungu.nawatakia sikukuu njema Mungu ibariki Tanzania by mwinjilist wenu Gabeji.
Huo ndio ukweli ulio wazi....kukutana kwa lissu na Samia ubelgiji ndo kulipelekea mbowe kutoka
 
Kwa kweli Lissu anaweza kuonekana ana msimamo mkali lakini Tanzania ni nchi legelege sana hata mtu akiwa na msimamo wa kawaida anaonekana ana msimamo mkali.

Mambo anayoongelea Lissu ya haki za binadamu, uwazi, usawa, simpke logic tu, si extreme. Tatizo ukimwambia Ntanzania kwamba kupata kazi uliyosomea ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu, kwa sababu yeye hajui katiba wala haki za binadamu, na wewe Lissu ni mtqalamu wa sheria na haki za binadamu, anaweza kukuona wewe Lissu ni extreme.

Ni sawa na watu wanaosema fulani ana Kiingereza kigumu sana, wakati kiukweli ni Kiingereza cha kawaida sana tatizo Watanzania wengi hata Kiingereza cha kawaida tu ni mgogoro, hivyo ukiongea Kiingereza cha kawaida kimataifa, Tanzania kinaonekana kigumu.

Na kabla watu wasiojua kusoma kwa ufahamu hawajanishambulia kuwa namdogosha Lissu, sina nia ya kumdogosha Lissu, naonesha kuwa Lissu si extremist hivyo, namtetea Lissu, tatizo ni Watanzania wengi wanacheza chini ya kiwango mchezaji akicheza kawaida anaonekana anakimbia sana.

Nchi nyingine mtu kama Lissu ndiye mbunge average.
Kuna ambao wanakwambia kaletwa na Mungu wakati ata anayoyaongea hayathibitishwa popote.ni porojo za kawsida tu kwenye siasa.yaani sisi ni taifa la vilaza sana.nikama wadumafu wa fikra.
 
Kuna ambao wanakwambia kaletwa na Mungu wakati ata anayoyaongea hayathibitishwa popote.ni porojo za kawsida tu kwenye siasa.yaani sisi ni taifa la vilaza sana.nikama wadumafu wa fikra.
Anayoyaongea yapi hayajathibitishwa popote?

Nimetaja baadhi hapo mambo ya haki za binadamu, uwazi, usawa, hizi ni universal principles, watu wameweka mpaka Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Wewe unasema Universal Declaration of Human Rights haijathibitishwa popote?

Unaelewa hata Universal Declaration of Human Rights ni nini?
 
Acha kujizima data kijana, watesi wa Lissu walikuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha anapotea hapa duniani
je unajua flight ya kumpekeleka Nairobi ilipatikanaje? Kwa kibali gani, kwa finance zipi? Au ndiyo kuchongoa mdomo.
Hayo mambo yanahusiana vipi na ulaji rushwa wa sultan Mbowe, kupitia Abdul na Mama yake?
 
Anayoyaongea yapi hayajathibitishwa popote?

Nimetaja baadhi hapo mambo ya haki za binadamu, uwazi, usawa, hizi ni universal principles, watu wameweka mpaka Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Wewe unasema Universal Declaration of Human Rights haijathibitishwa popote?

Unaelewa hata Universal Declaration of Human Rights ni nini?
Haki HUINUA taifa
 
Back
Top Bottom