Msimamo wangu kuhusu viongozi wa Chadema ni tofauti kidogo!!

Msimamo wangu kuhusu viongozi wa Chadema ni tofauti kidogo!!

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Sijuani hata na mmoja wao, hata kwa sura tu sijawahi kuwaona live. Nipo upande wao kwa sababu mara zote mimi nipo upande wa kundi linaloonewa. Huu msimamo wangu popote pale.

Naumizwa sana na anayopitia Mh. Tundu Lissu gerezani. Nimekuwa nikimuombea sana. Naumizwa sana na hawa wengine wanaotekwa na kufunguliwa kesi za ajabu ajabu. Kuna yule dada wa Kanda ya Ziwa, sijui Kahama alifunguliwa kesi ya uhaini. Kuna mwingine jana Katibu wa Sugu Kanda ya Nyasa kakamatwa. Naumia zaidi yanapofanywa haya mambo kwa kina dada. Najiuliza hivi wakamataji mbona mnakosa utu kabisa mpaka mnakamata kina dada?

Ninasikitishwa sana kijana mdogo John Pambalu kushikiliwa eti kosa Uhaini?! Ni mateso mwanzo mwisho.

Hapa ni kama risasi ya mwisho ni John Heche tu. Ukiangalia zaidi unaona kabisa hili genge halina cha kupoteza mpaka muda huu. Ni kama timu ifungwe 3-0 haiwezi tena kukaa nyuma kulinda goli. Kama wamefanya kwa Nchimbi bila madhara, wewe ni nani?!

Ukiangalia katika kupitia mateso yote haya hakuna watu walio nyuma yao. HAWAPO
Labda kidogo Wazungu na Haki za Binaadamu, lakini kwa Wananchi Watanganyika-HAKUNA. Watanganyika wapo nyuma yenu kimawazo, kimoyo na kuwaunga mkono kimaneno. Lakini kivitendo, sio kweli.

Angalia maumivu mnayopitia, weka kwenye mizani na reaction ya Watanganyika, Haviendani kabisa. Heche anaumiza kichwa sana, anashangazwa na watu kuwa na mwitikio wa vitendo kwenye mambo ya mipira na ujinga-ujinga wa mitandaoni, kuliko hatma yao.

Inashangaza kuona mwitikio wa vitendo kwenye mambo ya umiss halafu kukawa kimya kwa binadamu anayeongoza mapambano kupewa kesi ya uhaini.

Hata wakandamizaji wamepima hilo, chochote tutakachofanya hakuna reaction ya vitendo zaidi ya maneno.

Kiukweli silaha pekee iliyobaki ilikuwa ni umoja wetu, kushikamana na kusema hapana. Fikiria Yanga au Simba inataka kunyanganywa point, vurugu gani itatokea?!! Lakini sio kumpigania Lissu.

MAONI YANGU
Nawashauri mrudi nyuma kama sio kuendelea na maisha yenu binafsi, muwaache Watanganyika wateseke wateswe mpaka wakome. Waacheni wajipiganie wenyewe. Nyinyi mmeshafanya wajibu wenu, lakini pale wengine wanaposhindwa kufanya sehemu yao, inasikitisha sana.

John anapofunguliwa kesi ya Uhaini, familia yake inakuwaje.

Sioni maajabu ya hatua za kuwashtua hawa watesi wa Tanganyika, zaidi ya kuwaombea kifo tu.
 
Wewe jamaa, hao kenge ukijitokeza hadharani wanakuua. Lete mpango mkakati wa uhakika watu wajitokeze barabarani kukinukisha tena. Kinyume na hapo watu wataendelea na mapambano ya kwenye mitandao tu
 
Back
Top Bottom