Msimvimbisheni kichwa Mwingira, hana uwezo wa kupambana na Serikali

Kuongelea maswahibu yako na mitazamo yako kuhusu serikali ndo kupambana na serikali? Yesu aliposema yeye ni mfalme wa wayahudi, Je, alikuwa anapambana na watawala wa kiyahudi au alikuwa anaeleza ukweli ulivyo?
 
Nchi hii ina ushabiki kwenye kila kitu, iwe mpira,muziki,siasa nk. Watanzania kila mda wanataka umbea wa kushangilia na hapo ndio wanasiasa wanapo take advantage. Nchi hii tatizo sio viongozi, tatizo ni wananchi ambao wengi ni majuha na mbumbumbu...
 
Serikali ya kifedhuli kama hii inapaswa kukemewa bila kujali nguvu iliyonayo kwani wanao iongoza ni watu na huumia kwa makaripio kama binadamu wengine, na hivyo huanza kujirekebisha hata kama si kwa uwazi sana kificha aibu yao!
 
Una maana gani? Unashangilia Serikali kuua raia? Unaona ni Sawa? Unashauri raia waendelee kukaa kimya hata wasipotendewa haki? Wanapouawa?
Wapi nimeshangilia ?

Wapi nimesema wakae kimya?

Ukweli ni nini ?
 
''Busara ni moja, usijiingize kupigana VITA ambayo unajua kabisa HUWEZI KUSHINDA.''
 
Serikali yoyote ya kishetwani ndivyo inavyowafanyiaga raia wake
 
Yaani unabwabwaja kama hauna meno vile. Wewe unaishi tz au marekani? Live practical life not theories bwashee. Tz rais ni zaidi ya Mungu.
Ndo tunataka tuonfikane na huo ujinga. Hata wale walianza Kama sisi kumwabudu rais ili walifikia hatu wakamuona wa kawaida na sisi tunaweza. It begins with you
 
Anaweza asiwe msafi Ila yule mumiani wenu alikuwa tatizo
 
Umemsahau mtu mmoja yuko wapi Jiwe maana ndio alikuwa mtoa amri za watu kupotea
 
Wajuzi walimshambulia @zittokabwe Aliposema kuhusu Kijana aliyeagizwa na Mwendazake Kumuua na kuchoma nyumba yake ya Mwandiga kigoma, Ndio hao hao wanamshangilia Askofu Mwingira anaposema Amenusurika kifo mara Tatu na Dada aliyekua anamtonya aliuliwa hotelini na watu wa Serikali.

C&P

===========
Hii nchi USHABIKI na UNAFIKI viko kiwango kikubwa sana.

Hapo unaambiwa Kusema ukweli lakini huo ukweli ili uonekane ni kweli inategemeana ni nani kasema.
 
Lakini hivi..mimi nikikuambia nyumbani kwako kuna shetani je ntakua ni nmesema wewe ni shetani? Mbona Mwingira alikua akikemea shetani alieyejivinjari mahali..je kwanini mnamtwisha maneno??
 
..Mwananchi anayetaka kupambana na Serikali huku akisahau kuwa yeye ni laghai na tapeli wa sadaka za wengine akishughulikiwa kama mhuni kwa sababu tofauti na genge la wahuni basi ninyi wahuni wenzake msipige kelele
Hivi nchi hii ina freedom of expression kweli?

Mtu Katika maoni yake, ndiyo unamuita muhuni??
 
Ndio kawaida ya waasi, baada ya kupingana na Ukatoriki dhambi ya uasi inazidi kumtafuna' hawa ndio wachumia tumbo wa kiprotestant na mauchawi yao ya Nigeria
 
Unazungumzia dola iliyo chini ya serikali haramu?
 

Hiyo unayojaribu kuielezea ni nadharia tu, lkn Mkaruka anaongea hali halisi ambayo ipo duniani kote.
Nenda Kenya kaulize mauaji ya wapinga serikali wakuoneshe. Juzi juzi kuna masheikh wawili wameuawa Mombasa.
Stop fight with your government, you will never win.
 
Ni kweli hawa ndivyo walivyo hata Mzee wa Upako wakati wa Magufuli alikuwa anasifia sana ilipokuja suala la kusajili makanisa kila mwaka..leo hii amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali....hata huyu hakuna lolote kuna sehemu tu mrija wake umebinywa....na bahati mbaya sana wale wengine wanafurahi wanafikiri ni mwenzao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…