Msisitizo! Hakuna kipaji (inborn ability), mtu huwa na uwezo wa kitu fulani baada ya kuzaliwa

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
23,984
Reaction score
51,055
Wazungu walituaminisha kuwa Kuna watu huzaliwa wakiwa tayari na uwezo wa kufanya vitu fulani, mathalani, kucheza mpira, kuimba, n.k, ili tunaposhimdwa kufanya mambo fulani, turidhike kwa kuamini kuwa hatukuzaliwa na uwezo wa kutenda/kufanya mambo hayo.

Ukweli ambao watu wengi hawaujui ni kuwa, Kila mtu huzaliwa akiwa hajui chochote, maana yake wote tumezaliwa tukiwa sawa lakini sababu fulani fulani zimefanya wengine wawe na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kuliko wengine.

Hivyo, ni kosa kusema mtu fulani ana kipaji kisa amewazidi watu wengine katika kutenda jambo fulani. Ni vizuri tuwe tunasema mtu fulani ana uwezo wa kufanya kitu fulani. Mfano, Messi ana uwezo wa kucheza mpira kumshinda Ronaldo.

Nasanzuka!
 
Binadamu tumetofautiana,

Wapo ambao wana nguvu za mwili hasa waafrika ndio maana tumedominate kukimbia, ngumi, rugby, basket, n.k. wakati wazungu, waarabu, wachina, n.k. wana vifaa vizuri vya mazoezi ila tunawapita.

Wapo ambao wana uwezo mkubwa wa kujifunza au kufundishika kirahisi, hawa hapa kwetu ni kama wahaya, lakini akili za maisha, kugundua vitu, n.k. bado ndogo

Wapo ambao wana akili ya kugundua vitu, kusolve matatizo mapya, na hii ndio akili kubwa sana, hapa unawakuta wa Israel - Karibia kila kampuni kubwa ya teknolojia unayoijua wana ofisi za ugunduzi na uboreshaji wa teknlojia Israel, kule China huwa ni viwanda.

Wapo wenye uwezo mkubwa wa kusocialize kama wazaramo, wanaelewa kirahisi hisia za wengine, kuweza kudhibiti hasira kwenye matani, kumfanya hata mtu mkimya awe muongeaji, n.k.

wapo wenye uwezo mkuvwa wa kuwa na bidii ya kufanikisha mambo bila kuchoka, mtu yupo tayari kushinda dukani jumatatu mpaka jumatatu bila likizo alfajiri hadi usiku huku akiuza kwa faida ndogo na akijibana ila lengo lake aje kuwa na duka kubwa,

wapo wenye uwezo mkubwa wa uvumilivu, hapa naweza kuwaweka wanawake wa kihehe na wabena,
 
Binadamu tumetofautiana,

Wapo ambao wana nguvu za mwili hasa waafrika ndio maana tumedominate kukimbia, ngumi, rugby, basket, n.k.

Wap

wapo wenye uwezo mkubwa wa uvumilivu, hapa naweza kuwaweka wanawake wa kihehe na wabena,
Na hayo yote mtu hazaliwi nayo, bali husababishwa na semehu alikokulia mtu, umbo la mtu, tabia ambayo mtu hujizoesha na factors zingine.
 
Kwa kiasi flani lakini bado wana uwezo maalum wa ziada tofauti na mwengine.

Ndio maana hata shule ikiwa na kila kitu huwa kuna jamii flani inafanya vizuri darasani, jamii nyingine hata zikeshe na madaftari uwezo wao wa kujifunza ni mdogo au wa kawaida, huhitaji msaada wa ziada wa walimu wa tuition.
 
Ukifuatilia watoto wanaotoka katika jamii hizo mbili utagundua kuwa Kuna utofauti.

kwa mfano, watoto wa wahaya huenda wanafanya vyema darasani kwa sababu katika jamii yao wanamwona msomi kama mtu anayeheshimika, huku waman'gati wakimchukulia msomi kawaida, ndiyo maana watoto lazima watofautiane kwenye performance.

Mimi huwa najiuliza, kwa nini India na China hawana wachezaji wazuri wa mpira wa miguu, ilihali Brazil na mataifa mengi ya ulaya wanatoa wachezaji wazuri? Je ni kwaba wahindi hawazaliwi na uwezo wa kusakata kabumbu? 🤔.
 
Wazungu walituaminisha kuwa Kuna watu huzaliwa wakiwa tayari na uwezo wa kufanya vitu fulani, mathalani, kucheza mpira, kuimba, n.k, ili tunaposhimdwa kufanya mambo fulani, turidhike kwa kuamini kuwa hatukuzaliwa na uwezo wa kutenda/kufanya mambo hayo.

Ukweli ambao watu wengi hawaujui ni kuwa, Kila mtu huzaliwa akiwa hajui chochote, maana yake wote tumezaliwa tukiwa sawa lakini sababu fulani fulani zimefanya wengine wawe na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kuliko wengine.

Hivyo, ni kosa kusema mtu fulani ana kipaji kisa amewazidi watu wengine katika kutenda jambo fulani. Ni vizuri tuwe tunasema mtu fulani ana uwezo wa kufanya kitu fulani. Mfano, Messi ana uwezo wa kucheza mpira kumshinda Ronaldo.

Nasanzuka!
nilivyoanza kuusoma uzi wako niliona una kitu hv xema kwenye eti mec anaweza kuliko cr7 umebugi jomba yan mpaka uzi umeanza kunuka
 
Wazungu walituaminisha kuwa Kuna watu huzaliwa wakiwa tayari na uwezo wa kufanya vitu fulani, mathalani, kucheza mpira, kuimba, n.k, ili tunaposhimdwa kufanya mambo fulani, turidhike kwa kuamini kuwa hatukuzaliwa na uwezo wa kutenda/kufanya mambo hayo.

Ukweli ambao watu wengi hawaujui ni kuwa, Kila mtu huzaliwa akiwa hajui chochote, maana yake wote tumezaliwa tukiwa sawa lakini sababu fulani fulani zimefanya wengine wawe na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kuliko wengine.

Hivyo, ni kosa kusema mtu fulani ana kipaji kisa amewazidi watu wengine katika kutenda jambo fulani. Ni vizuri tuwe tunasema mtu fulani ana uwezo wa kufanya kitu fulani. Mfano, Messi ana uwezo wa kucheza mpira kumshinda Ronaldo.

Nasanzuka!
uzi wako nimzur xema kweny et mec anauweza kuliko cr7 dah uzi umenuka
 
umesema vema kabisa, maana kama vipaji tunazaliwa navyo. Basi TAJIRI nae ana kipaji.
 
Binadamu tumetofautiana,

Wapo ambao wana nguvu za mwili hasa waafrika ndio maana tumedominate kukimbia, ngumi, rugby, basket, n.k. wakati wazungu, waarabu, wachina, n.k. wana vifaa vizuri vya mazoezi ila tunawapita.

Wapo ambao wana uwezo mkubwa wa kujifunza au kufundishika kirahisi, hawa hapa kwetu ni kama wahaya, lakini akili za maisha, kugundua vitu, n.k. bado ndogo

Wapo ambao wana akili ya kugundua vitu, kusolve matatizo mapya, na hii ndio akili kubwa sana, hapa unawakuta wa Israel - Karibia kila kampuni kubwa ya teknolojia unayoijua wana ofisi za ugunduzi na uboreshaji wa teknlojia Israel, kule China huwa ni viwanda.

Wapo wenye uwezo mkubwa wa kusocialize kama wazaramo, wanaelewa kirahisi hisia za wengine, kuweza kudhibiti hasira kwenye matani, kumfanya hata mtu mkimya awe muongeaji, n.k.

wapo wenye uwezo mkuvwa wa kuwa na bidii ya kufanikisha mambo bila kuchoka, mtu yupo tayari kushinda dukani jumatatu mpaka jumatatu bila likizo alfajiri hadi usiku huku akiuza kwa faida ndogo na akijibana ila lengo lake aje kuwa na duka kubwa,

wapo wenye uwezo mkubwa wa uvumilivu, hapa naweza kuwaweka wanawake wa kihehe na wabena,
Qur'an inasema Allaah amemtoa mwanadamu kwenye kutoka tumboni akiwa haujui chochote.
DSpRahHXUAIPxdK.jpg

Hapo kila mtu kazaliwa mjinga , Ugeniaz , Elimu ni acquired characteristics mtu anapata akija Duniani kutokana na sababu mbalimbali
 
Qur'an inasema Allaah amemtoa mwanadamu kwenye kutoka tumboni akiwa haujui chochote.
View attachment 3571019

Good! Ndo maana naishauri serikali iwahimize wananchi waache kutumia neno kipaji au ibadilishe definition ya kipaji.
 
Qur'an inasema Allaah amemtoa mwanadamu kwenye kutoka tumboni akiwa haujui chochote.
View attachment 3571019

Hapo kila mtu kazaliwa mjinga , Ugeniaz , Elimu ni acquired characteristics mtu anapata akija Duniani kutokana na sababu mbalimbali
Wote tunatoka matumboni ila hata rangi za ngozi tofauti, urefu tofauti, sura tofauti, Dna tofauti, n.k.
 
Kabla hujambishia mzungu jitahidi uwe na sababu za kisayansi na sio kuchomekea imani za kishirikina kwenye maelezo yako. Huu uzi wako upo kiimani bila facts.. NINASHAURI HUU UZI UPUUZWE.
Kwani mzungu ndiye nani? Wazungu nao hudanganya kama watu wengine.

Kwanza hebu niambie wewe unakipji gani kabla hatujaendelea.
 
Wazungu walituaminisha kuwa Kuna watu huzaliwa wakiwa tayari na uwezo wa kufanya vitu fulani, mathalani, kucheza mpira, kuimba, n.k, ili tunaposhimdwa kufanya mambo fulani, turidhike kwa kuamini kuwa hatukuzaliwa na uwezo wa kutenda/kufanya mambo hayo.

Ukweli ambao watu wengi hawaujui ni kuwa, Kila mtu huzaliwa akiwa hajui chochote, maana yake wote tumezaliwa tukiwa sawa lakini sababu fulani fulani zimefanya wengine wawe na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kuliko wengine.

Hivyo, ni kosa kusema mtu fulani ana kipaji kisa amewazidi watu wengine katika kutenda jambo fulani. Ni vizuri tuwe tunasema mtu fulani ana uwezo wa kufanya kitu fulani. Mfano, Messi ana uwezo wa kucheza mpira kumshinda Ronaldo.

Nasanzuka!
Vipaji vipo na huwa vinajipambanua kupitia Natural instincts!
 
Back
Top Bottom