Ngwathra
Platinum Member
- Jul 11, 2007
- 7,258
- 14,942
Wazungu walituaminisha kuwa Kuna watu huzaliwa wakiwa tayari na uwezo wa kufanya vitu fulani, mathalani, kucheza mpira, kuimba, n.k, ili tunaposhimdwa kufanya mambo fulani, turidhike kwa kuamini kuwa hatukuzaliwa na uwezo wa kutenda/kufanya mambo hayo.
Ukweli ambao watu wengi hawaujui ni kuwa, Kila mtu huzaliwa akiwa hajui chochote, maana yake wote tumezaliwa tukiwa sawa lakini sababu fulani fulani zimefanya wengine wawe na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kuliko wengine.
Hivyo, ni kosa kusema mtu fulani ana kipaji kisa amewazidi watu wengine katika kutenda jambo fulani. Ni vizuri tuwe tunasema mtu fulani ana uwezo wa kufanya kitu fulani. Mfano, Messi ana uwezo wa kucheza mpira kumshinda Ronaldo.
Nasanzuka!
Hamna mzungu anayeaminisha hayo kwanza kwao kuna mjadala ambao haujawahi kupata majibu unaongelea "nature against nurture" binadamu anazaliwa kama computer tupu (hardware) inakuwa jinsi ilivyo baada ya kuwekwa software so kila mtu anaweza kuwa somebody kwa kuwezeshwa,