Msonde maagizo yako yanaipoteza elimu

Unaishi zamani sana sasa

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Kwanini?tukianza mjadala wa CBC hatutamaliza humu,ni ngumu sana kutenganisha CONTENT BASED na COMPETENCE BASED Kwa wanafunzi wa primary na SEKONDARI ,Kwa vyuo vya kati na vikuu inawezekana.

Kuna vitu ilitakiwa vifanyike ndo tuanze kuhimiza competence based Kwa shule za vijijini.
 
Reactions: K11
Yes yes, walizoea kitonga!!!
 
Umemjibu vyema sanaa.
Yeye naye ni sampuli za akina msonde humu jamvini, hakuna anachoelewa kwenye sekta ya Elimu lakini kanajifanya kama vile ni muelewa

Mm ni Mwl sifichi kitu na naipenda kazi yangu, na mm ni kijana, nimeishi quarters za walimu nchi hii tangu nikiwa mtoto mdogo up to now nafanya kazi ya ualimu

Kuna changamoto nyingi zinaikumba sekta hii na hipo siku nitayaleta kwenu hapa tuyajadili, lengo nikusaidia serikali yetu na nchi kwa ujumla, kumbuka hakuna maendeleo bila Elimu bora
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Si tu hivyo,eti Mwl yuko darasani awe anachungulia kwenye lesson plan ili ajue ni tendo gani lifuate?

Mpwayungu!
Hivi ukifuata muongozo unavyosema mada ya wave pale kidato cha 4 ulitakiwa huifundishe miezi mingapi vile?
Vp Electromagnetism?
 
Mi ni mmoja kati ya watu ambao wanaunga mkono COMPETENCE BASED EDUCATION 100% ndio tunayoihitaji lakini kiukweli hiyo hatuwezi kukurupuka bila kujiandaa hasa katika mazingira ya utoaji wa elimu kiujumla
1.Walimu wa hiyo kitu waandaliwe na waliopo wanolewe kisawasawa (wengi wa sasa ni CONTENT BASED)
2.Madarasa vitabu na miundombinu yote ya shule iwe katika standard ya hali ya juu pamoja na upatikanaji wake.
3. Mitaala iboreshwe zaidi. Ni lazima tuweke vipaumbele kama nchi tuwe na dira yetu, utoaji wa elimu uendane na falsafa za nchi yetu na mahitaji ya falsafa hiyo.
4. Jamii ilazimishwe kupeleka watoto shule utake usitake, haya mambo ya kuelimishwa yamepitwa na wakati.
5. Muhimu kabisa, maslahi ya walimu ambao ndio watendaji wakuu wa shughuli hii yaboreshwe ifikie hatua kila mtu atamani kuwa mwalimu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nimesoma post yako sijaona hata solution moja zaidi ya malalamiko

Hamtaki kuwajibishwa, hamtaki kutoa taarifa,

Time sasa Kwa kila civil servant kuwa na ajira za mikataba and based on performance
 
Una uhakika kiasi gani kuwa ni Mwl?

Ikiwa madai yako ni ya kweli,mwenye kosa ni nani kati ya huyo Mwl na baraza la mitihani waliompitisha kwa mchujo mpaka akafika hapo?

Kuwa mkubwa kichwani ndo ulingane na Honi Sigara.
 
Nimesoma post yako sijaona hata solution moja zaidi ya malalamiko

Hamtaki kuwajibishwa, hamtaki kutoa taarifa,

Time sasa Kwa kila civil servant kuwa na ajira za mikataba and based on performance
Huku ndo kukurupuka, uwa shida yenu ni akili samahani lakini if nimekukwaza, kwani tunashida na hizo ajira za mkataba? Mara ngapi tunaomba tuajiiriwe kimkataba? Tena hizi ajira za kufungana kwa welding haya anayataka nani?

Mm silalamiki nikuwa najaribu kutoa picha halisi na ugumu uliopo kutokana na sera na mawazo ya kijinga kwenye sekta ya Elimu kama hizo za msonde ok

Nahitaji niwe kwenye ajira ya mkataba ili nifanye mambo yangu vyema ok, mm siwezi lalamika ila viongozi wetu hawana akili kichwani full stop, mtu mzima msomi unafeli vipi kusaidia jamii??
 
Umenena UKWELI.
Huyu A MKENDA ana maono mazuri na anaitakia mema elimu yetu,shida mfumo wetu utamkataa na kumuona mpuuzi kabisa.

Wewe fikiria eti somo la hisabati darasa la 7 ni kuchagua majibu?

Kidato cha 4 asiyependa kupata division 1 ndo ata ng'ang'ana kusoma Basic Mathematics,ila km anataka kupata one kupitia masomo mengine ni kuteleza tu kwakuwa F ya Basic Mathematics haina athari hasi kwenye matokeo ya jumla km zamani.

Kitakachotokea ni kwamba licha ya uchache wa Walimu wa hili somo lkn pia wana wakati mgumu sana kumshawishi mtoto alipende somo hili.

Lkn mwisho wa siku Mwl huyu naye kasainishwa mikataba iliyotajwa na mtoa mada.

Tujiandae kushuhudia uhaba mkubwa wa Walimu wa masomo yanayohusiana na kukokotoa lkn pia wataalamu wa mahesabu hapa nchini baadae kidogo ktk kipindi ambacho tunaigiza kulipa kipau mbele somo la computer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…