Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Tumesema weee watu bado hawatali elewa. Bunduki au bastola unayo ya nini?! Una benki kwako?! Una mgodi wa madini yenye thamani?! Una….
Sasa matokeo yake ndio haya 🥵😡😂
 
We noma umeleta Mfano hai
Bado hajamwambia! Ndiyo anataka siku moja aje amwambie atowe mabati yake juu kwake! Sasa akisha mwambia ndiyo tunaweza sema huo ndiyo mfano Hi baada ya mrejesho!!!
 
Vita ya mchaga kwenye ardhi huwa hainaga mwisho
Mifumo yetu ya Sheria na haki kwenye Aridhi ikisimama vizuri tu,huyo Mchaga mbona ana surrender mapema tu! Mchaga kwenye Vita ya Aridhi huwa anapenda kucheza na watu wa ndani ili kufanikisha dhuluma yake!!
 
Isee mambo ya mipaka ni pasua kichwa, nina kakiwanja kangu 20×30M nilinunua mwaka 2010, nikafanikiwa kujenga na kuweka kaukuta kafupi mpakani kwa kua kulikua na kangema nyuma, baada ya miaka kadhaa yule kijana niliyekua nimepakana nae upande wa ukuta akamuuzia mhaya 1, tukafahamiana mshkaji fresh sana akajenga maisha yakaenda, Sasa mimi sio mkaaji wa pale nyumbani nahangaikia riziki mikoani narudi kila week nakaa siku 2 au tatu naondoka ila familia yangu ipo hapo, Sasa serikali ya kijiji ikaja kupima viwanja na kuweka bicon ili tupewe hati, sijui kilitokea nini mke wangu hakuwepo wa huyu jamaa jirani yangu hakuwepo mke wa jamaa akawaonyesha waweka bicon mpaka ndani ya ukuta wangu. Wakati mpaka halisi unaonekana kabisa nje ya ukuta niliojenga tena karibu 1m. Sio mimi wala wife hakuna aliyona ile bicon kumbe mama mmoja jirani aliona lile tukio la kuwekwa bicon ndani ya ukuta wangu. Baada kama siku tatu ndo akamwambia wife mbona bicon imewekwa huku, wife akavurugwa akanipigia baada ya week nilipopata nafasi nikaenda aisee kidogo nichanganyikiwe. Ikumbukwe natakiwa kuvunja ukuta sababu bicon ipo ndani ya eneo la jiran yangu na ukuta alikukuta wakati anauziwa,nikamfuata mwanaume mwenzangu namwambia vipi ananiambia hapo ndo mpaka, nikaita majirani wanao jua kile kiwanja pamoja na shahid jamaa amekataa katakata, mimi nikabomoa ukuta nikahamisha. Ugomvi ukahamia mimi na wife yeye anataka nikaze mimi nikamwambia sitaki. Mi nikasamehe maisha yakaenda, kumbe na upande wa juu huko yule mama alifanya hivyo hivyo kwa mama mwingine aliye pakana nae, yule mama akaongea na jamaa ikagoma kama mimi, yule mama akamwita shemeji yake kumbe ni mwajeshi kuja akamwambia nionyeshe mpaka ni upi, alipoonyeshwa tunashangaa kesho watu wakaja chimba mtaro tena ukutani kwa jamaa waka mimina zege wakapiga ukuta na nguzo za zege tena alijenga ndani kabisa ya kiwanja cha jirani yangu aliyenizulumu. Sashivi wanalia wanahangaika kila mtu hataki kuwasaidia. Yule mwanajeshi alienda kubadilisha ile karatasi ya mauziano na ana hati. Jamaa analalamika tu hadi leo
 
Unafanyajje mauaji alafu unakamatwa kizembe hivo Ani maiili Moja ndo kamaliza kujificha.. Tena former Tpdf
... Hahahh
Siyo Wanajeshi wote wana akili! Sifa kuu no moja ya Mwanajeshi aliyeivaa ni kua mvumilivi sana kwa raia wa Nchi yako hata Kama unajua unamilki AKA 47! Just be cool hata kama amekutusi!! Na Kama umeshindwa kumvumilia mpeleke kwenye vyombo vya Sheria huko wakamtafsirie hizo Sheria zinasemaje!!
 
Huyu mzee anaenda kuvuliwa nguo jela kizembe sana.
Pole kwa familia kwa kuwa na baba jinga!
 
Kupakana na askari yeyote wa jeshi la Tanzania ni changamoto kubwa sana. Wale wanao pakana nao nikiwemo mimi tulio wengi itakuwa tunajuta sana. Japo si wite, ila walio wengi wao wanajifanya wababe sana.
Ukipakana nao hao hakikisha mkishaelewana kwamba mpka ni huu, kesho yake jenga ukuta! Maana ukiacha wazi kwamba tumeshaelewana kesho anakuja kusogeza tena


Ila yote kwa yote watu wa morogoro wana ugomvi wa ardhi hatari
 
Mara nyingi nasema hawa ndugu zetu waliopo na waliopitia JWTZ wana ushamba sana wanajiona ni watu wa aina yake na kulazimisha kuogopwa na kujiona wapo juu ya sheria kumbe viraka tu yaani wanatumika kama tambara la deki wengi wakirudi mitaani wanakuwa wana stress na wengine kuwa walevi wa mataputapu, binafsi siwapendi kabisa.
 
Ukipakana nao hao hakikisha mkishaelewana kwamba mpka ni huu, kesho yake jenga ukuta! Maana ukiacha wazi kwamba tumeshaelewana kesho anakuja kusogeza tena


Ila yote kwa yote watu wa morogoro wana ugomvi wa ardhi hatari
Bado hujamalizia list
Mzee

Ova
 
Dawa yao watu kama hao unazungusha ukuta eneo lako lote unaacha wanaangaika nje ya ukuta huko
 
Namshauri Mulilo awe anaenda site asingoje taarifa za kuletewa mezani na hao nyakunyaku wake, taarifa anazopewa ni matangopori hazina uhalisia.
 
Mtu unajua ni mjeda, anachomoa chamoto anakoki upo tu, mjinga sana, na hiki kibabu siajabu alishakitishia maisha, kikamfanyia timing kama kako vitani darfur
BRO usimlamumu marehemu bila sababu mtu akichomoa akakoki hata ukimbie itakupata tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…