Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Jonas Ziganyige (71) mstaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi Juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi (48) mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni katika mgogoro wa mipaka.

Mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio hilo Julai 9, 2022 ambapo marehemu alifika eneo akiongozana na Recy Renso (52) kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake, ndipo mtuhumiwa akatoka ndani akiwa na hasira akampiga risasi Romward na baada ya tukio alikimbia kabla ya kukamatwa Julai 10, 2022 akiwa Kibaha Maili Moja, Pwani alikokuwa amejificha.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Muliro Jumanne amesema wameipata silaha aliyotumia ambayo ni Mark IV ikiwa na risasi 4, atafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili.

Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendelea pia na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya Uhalifu na Wahalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Watuhumiwa 8 sugu wa uvunjaji nyumba na kuiba vifaa vya magari akiwemo Jumanne Omary (28) Mkazi wa Mikwambe na wenzake 7 wamekamatwa wakiwa na Tv flat screen za aina ya mbalimbali 4, laptop mbili, sab ufa moja, simu aina mbalimbali tano pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu vikiwemo mikasi miwili mikubwa ya kuvunjia, panga moja, kisu kimoja, Prize na Bisibisi, Tochi na Nyaraka mbalimbali.

Pia gari lenye namba za usajili T.787 DGW aina ya Toyota Gaia limekamatwa kwa kuhusishwa na kutumiwa kwenye vitendo vya kihalifu.

Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani kwa kufanya vitendo hivyo watakamatwa na watajikuta wakiwa katika msuguano mkali wa kiseria na vyombo vya dola.
Sasa mtu wa miaka 71 unagimbania mpaka wa nini!!??
wakati jioni imeshafika
 
Unafanyajje mauaji alafu unakamatwa kizembe hivo Ani maiili Moja ndo kamaliza kujificha.. Tena former Tpdf
... Hahahh
 
Nipo msibani hapa wazo. Kesho tutazika. NADHANI HUZUNI NA SONONEKO LA FAMILIA HII NI KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.
Hilo eneo jamaa alienda kuangalia ni la rafiki yake yupo nje ya nchi, alimuomba akaangalie. Huyo babu wa miaka 71 kwa wenge akadhani huyu ni mmiliki nikiua huyu namiliki ardhi yote hii...POMBE NA BANGI VINAATHIRI SANA WANAJESHI.
Nimejifunza! Kumbe Uchawa nao ni Hatari...
 
Unatishwaje na raia? Chomoa cha moto maliza kazi, jamaa nalo jinga mtu ana cha moto unaanza kumwomba nipige uone, unakula ya kichwa, hiki kibabu nadhani kilikuwa kibodigadi cha Nyerere moja tu jamaa chali
Sasa ndio muda wa ile Puru yake Sealed ikatumike na wajuba wa huko magereza.
 
Baadhi ya wanajeshi wana tabia moja ambayo sio sawa wanapostaafu wakiingia uraiani bado wanakuwa na mawazo ya kibabe kitu ambacho sio kweli na ndio maana nimesema baadhi.Mtaani kwetu yupo mmoja alikuwa hivyo alikuwa anataka kila mtu amsujudie.Alikufa kifo cha mungu tu kuugua lakini wakati anaugua nadhani ndio aliona madhara ya matendo yake hakuna mtu alikuwa anakwenda kumsalimia amekufa kama mbwa akazikwa kama mbwa
Hao Askari wasumbufu huko mtaani ujue walistaafu wakiwa na vumilia vumbi tu mabegani(V),Ni Mara chache Sana kukuta senior officer wa jeshi ana mambo ya kikuda.Hua wanajielewa sana.
 
Ukubwa wa eneo sasa linalogombewa
Utakuta vihatua 3,4 tu
Na siku zote ugomvi wa ardhi huwa mmbaya sana,kama watu hamuelewani iko siku ardhi hiyo hiyo
Itammeza mtu

Ova
ni kweli hii mm ikinitokea siku tukaitisha kikao pamoja n B mkubwa alikuepo na serikali ya mitaa
alichofanya bi mkubwa alimuuliza yule jirani yangu
mipaka yako iko wapi akaonesha akamuuliza mara tatu akaonesha mara 3
kumbe alikuwa kashamuandaa fundi akamuita fundi akachimba akachomeka zile bikoni ndefu za kufungia senyenge akaitia mpk nusu
kisha akatugeukia wote akasema mpk huo hapo na nyie wote mashaidi kesi ikaisha hapo

nilichukia sana jamaa kumega eneo letu ila akampa ushindi na kesi ikaisha
akaniambia MWANANGU hatua 2 kitu gani
BABAAKO tulokuja kununuaga wote kashakufa kaliacha mimi niliye HAI sina hata kazi nalo

Sasa umerithi wewe nawe utakufa atarithi mwanao
ikaisha hivyo
miaka kadhaa mbele watu wakamjengea mbele hana hata pakuhifadhi gari
gari yake anahifadhi kwenye uwanja wangu
huwa namuangalia tu anavyojichekeshachekesha
Watu wa bara wanapenda sana migogoro ya ardhi hasa kanda maalum na ukanda wa kaskazini

Sisi wazaramo ARDH ni kitu cha kawaida sana ROHO ya mtu ina thamani kubwa kuliko ARDHI
 
Hao Askari wasumbufu huko mtaani ujue walistaafu wakiwa na vumilia vumbi tu mabegani(V),Ni Mara chache Sana kukuta senior officer wa jeshi ana mambo ya kikuda.Hua wanajielewa sana.
Hadi akamiliki silaha alikuwa mtu mkubwa jeshini
 
Mtu unajua ni mjeda, anachomoa chamoto anakoki upo tu, mjinga sana, na hiki kibabu siajabu alishakitishia maisha, kikamfanyia timing kama kako vitani darfur
kwa hile video wameshtukizwa maana alikuja direct na kumpiga risasii
 
Back
Top Bottom