Mstari mwekundu wa Iran umeshavukwa lakini bado wanatii amri

Baadae msilalamike tena mafuta yamepanda ooh chakula mbona tunalima lakini bei juu
Furahieni sana tena na party juu
Ila kilio kitakuja soon
Mkuu Ujue kuna siku ulinichekesha sana kuhusu walimu kuchapa wanafunzi fimbo. Ukauliza hivi bado tu wanafunzi wanachapwa fimbo ndo maana hakuna ufumbuzi na ugunduzi Tanzania na hakutawahi kuwepo.
 
Unasema au unatuambia.Kwa sababu kukemea uovu ni jukumu la wote.Mafuta yakipanda yanapanda kwa sote.
Ukiona Israel anapiga hospitali na kuuwa watu kwa kiu na njaa na wewe waambie sitisha vita.
Nakemea sana vita kwa sababu naijua sana na nimeshiriki Tatu sio moja
Najibu kwa hao wanaofurahia vita sio mimi
Siwezi kuwa na roho katili hapana bali ukisoma vizuri nakemea wanaofurahia hii vita na kusema itawarudia nyie kama Iran na Israel watapigana
Please soma bila jazba always tuko pamoja
 
Mkuu Ujue kuna siku ulinichekesha sana kuhusu walimu kuchapa wanafunzi fimbo. Ukauliza hivi bado tu wanafunzi wanachapwa fimbo ndo maana hakuna ufumbuzi na ugunduzi Tanzania na hakutawahi kuwepo.
Ilikuwa ni uchungu Mkuu
Ila ni ukweli mchungu
Watoto wanakariri tu
Usitegemee jembe la mkono litakuwa thing of the past
 
Iran mtoe hapo
 
ngoja watu waingie kwenye mfumo vizuri...HAO MASHOGA WATALIA MACHOZI YA DAMU
 
Unadhani Iran haja react mpaka sasa?Hivi unajua kinachoendelea huko shebaah farms kati ya IDF na hizbollah?Pole yako,Iran ana react kwa kumtumia Hizbollah kaa ujue hilo na hizhollah kapatiwa long range ballistic missiles tayari ambapo kama Hassan Nasrallah akisema wanaingia full scale war zitatumika.
 
Wanatumia ndege.Hawapo katikati.Vifaru vimeshaingia mara mbiii na kulazimika kurudi nyuma.Siku ya Ijuma vilichakazwa kweli.
Kama umeviona katikati onesha wapi vilipo.
Mkuu mbona unatufanya Sisi watoto na hatuna habari.
Makomandoo wa IDF waliopo vitongoji ndani ya Gaza na vifaru wanafanya nini mkuu?
Unapoleta habari ujue kuna waandishi wa habari humu.
 
Sasa kurusha maroketi na kuvizia askari wa mpakani...Ndio kupigana.
Tofautisha propaganda na uhakisia.
Hizbolah haina uwezo hata wa kuchukua inchi moja ya aridhi ya Israel
 
Mnaleta ushabiki kwenye uhai wa watu
Watu wanakufa watoto wamama wababa wazee na vikongwe ila waisrael na wapelestina wa bongo mnaleta uahabiki duuuh
 
Halafu pia we ni muongo na uchambuzi wako hauna mashiko.NETANYAHU MWENYEWE ALISEMA HAKUNA MPAKA WA RAFAH KUFUNGULIWA MPAKA ISRAEL ITOE TAMKO.Ndio maana Emir wa Qatar Althani alitumika kuzungumza na Netanyahu ili aruhusu magari ya msaada kuingia.Akaanza kuruhusu magari 20 kwa siku kuingia mpaka msaada utosheleze.Halafu hujasema kuwa USA anapiga kelele Iran isijihusishe na vita pia ushasahau kama Mfalme Wa Jordan alitamka katika kikao cha Arab peace summit kuwa kama mgogoro ukiendelea na Gaza ikikandamizwa waarabu hawatosita kuingilia vita.Tizama taarifa ya habari kijana USA kila uchwao anatafuta namna ya kuwaziba masikio waarabu kupitia vikao ili wasije kubali wito wa Iran kuisaidia hamas.Naona kuna mengi huyafuatilii yanakupita.Pia haukufuatilia kuwa Muhammad bin Salman amesitisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel na amemtamkia Biden kuwa kama Iran itachukua hatua zaidi kuwatetea Palestina basi wao wataungana nao.Wakati huo Jordan,Iraq na Pakistan imefunga balozi za Israel na kuwafukuza na mpaka ndege za Israel haziruhusiwi kutua katika viwanja vyao.Usisahau Pia kuwa Iraq imetamka wazi kuwa kama italazimika mpaka makundi ya washika silaha yataungwa mkono kama ukandamizaji utaendelea Palestina.Hapo tayari hata kama vita itaisha Israel atakua na anguko la kidiplomasia pale middle east na kupitia mkutano wa arab peace summit ulofanyika Misri mataifa ya kiarabu yashakiri na kusema kuwa hawajihisi salama tena kuwepo na Israel kwa yanayoendelea.Kizazi hiki huwenda kinakaa kimya je unadhani kizazi kijacho kitafanyaje na kama hivi Israel supporter wake mkubwa ni USA ???
 
Wakichelewa kuzitumia watalaumiwa.Watoto kila siku wanafukiwa kwenye vifusi.Haipendezi baada ya mwezi Israel aseme kamaliza kazi na baadae aanze kujadili ujanja mwengine kwa genge la Mahmoud Abbas
 
Wakichelewa kuzitumia watalaumiwa.Watoto kila siku wanafukiwa kwenye vifusi.Haipendezi baada ya mwezi Israel aseme kamaliza kazi na baadae aanze kujadili ujanja mwengine kwa genge la Mahmoud Abbas
Hakijulikani kitafanyika nini maana kila mmoja anasema muelekeo wa vita unategemea Hassan Nasrallah ataiamuru nini Hizbollah maana hakutoa kauli mpaka sasa.Ila kiuhalisia kama full scale war itaanza kusini mwa Lebanon IDF haina uwezo wa ku repel mashambulio kote kote .Chochote kinaweza kutokea na ndio maana kuna vikao vingi vinakaliwa kujadili mzozo wa Gaza.
 
Ndio maana zimepelekwa meli vita2 huko middle East kutoka USA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…