Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
- Thread starter
- #41
Mimi huwa nafuatilia maneno yao halafu napima na vitendo vyao.Nikiangalia naona maneno ni mengi na vitendo ni vichache na kinyume cha maneno.Halafu pia we ni muongo na uchambuzi wako hauna mashiko.NETANYAHU MWENYEWE ALISEMA HAKUNA MPAKA WA RAFAH KUFUNGULIWA MPAKA ISRAEL ITOE TAMKO.Ndio maana Emir wa Qatar Althani alitumika kuzungumza na Netanyahu ili aruhusu magari ya msaada kuingia.Akaanza kuruhusu magari 20 kwa siku kuingia mpaka msaada utosheleze.Halafu hujasema kuwa USA anapiga kelele Iran isijihusishe na vita pia ushasahau kama Mfalme Wa Jordan alitamka katika kikao cha Arab peace summit kuwa kama mgogoro ukiendelea na Gaza ikikandamizwa waarabu hawatosita kuingilia vita.Tizama taarifa ya habari kijana USA kila uchwao anatafuta namna ya kuwaziba masikio waarabu kupitia vikao ili wasije kubali wito wa Iran kuisaidia hamas.Naona kuna mengi huyafuatilii yanakupita.Pia haukufuatilia kuwa Muhammad bin Salman amesitisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel na amemtamkia Biden kuwa kama Iran itachukua hatua zaidi kuwatetea Palestina basi wao wataungana nao.Wakati huo Jordan,Iraq na Pakistan imefunga balozi za Israel na kuwafukuza na mpaka ndege za Israel haziruhusiwi kutua katika viwanja vyao.Usisahau Pia kuwa Iraq imetamka wazi kuwa kama italazimika mpaka makundi ya washika silaha yataungwa mkono kama ukandamizaji utaendelea Palestina.Hapo tayari hata kama vita itaisha Israel atakua na anguko la kidiplomasia pale middle east na kupitia mkutano wa arab peace summit ulofanyika Misri mataifa ya kiarabu yashakiri na kusema kuwa hawajihisi salama tena kuwepo na Israel kwa yanayoendelea.Kizazi hiki huwenda kinakaa kimya je unadhani kizazi kijacho kitafanyaje na kama hivi Israel supporter wake mkubwa ni USA ???
Unavyoona wewe hapa ilipofika Jordan alipaswa kusema au kuchukua hatua ya kuvunja mkataba na kuacha mpaka wazi.Au unavyoona wewe Misri ni wa kulalamika kuwa watu wanakufa kwa njaa au ni kutoa tamko napeleka misaad na ukiizuia au kunipiga napambana na wewe.
Unajua kuwa upekuzi wa malori unafanyika ndani ya Misri na Rafah imepakana na Gaza na haikupakana na Israel.