Mstari mwekundu wa Iran umeshavukwa lakini bado wanatii amri

Mstari mwekundu wa Iran umeshavukwa lakini bado wanatii amri

hayo ni matokeo ya vita, subiri tuone hadi mwisho. sasa mbona hamas wameshaanza kutoa video za mateka wakiomba israel isitishe mapigano, kama wangekuwa hawajakamatika kwanini wanatamani vita iishe? si kwasababu hawana pa kutokea, israel amesema vita hiyo kwake ni ngumu na ni ya muda mrefu, Gaza ni eneo lililozungukwa, pande, na jana Israel wameshazunguka na kufunga njia toka kusini wakiwatenganisha wapalestina waliokimbilia kusinina upande wa gaza wa kaskazini, hivyo Gaza ya kaskazini ambako hamas wamejificha kumeshazungukwa, hawana pa kutokea, na hawawezi kukaa pale mwaka mmoja, wataishiwa chakula, silaha, maji, mafuta ya kuendeshea mitambo na magari, na watakamatwa kama panya tu. its just a matter of time. ingelikuwa hawajazungukwa, wangeweza kukimbia nchi, ila hawana pa kutokea israel amezunguka kote wenyewe wapo katikati, upande wowote wakichomoza kichwa watafyekwa.
Pengine ni kweli uyasemayo lakini nahisi utakuwa hujui kwamba Hamas wana njia za chini ya ardhi hapo Gaza zinazoweza kuwatoa nje ya mji.
 
nchi kama Saudia zina ratiba ya kukutana na viongozi wa Marekani wiki ijayo kuzungumzia masuala ya Gaza na uwezekano wa kusitisha vita. Inawezekana wanachokusudia kukizungumza sio kusitishwa vita bali wana ajenda nyengine tofauti .
Si walimkwepa Biden alipokwenda Israel!!
 
Pengine ni kweli uyasemayo lakini nahisi utakuwa hujui kwamba Hamas wana njia za chini ya ardhi hapo Gaza zinazoweza kuwatoa nje ya mji.
ramani yake haionyeshi kama zimetoka nje ya mji. wangekuwa na upenyo huo, wangeshatoroka wote. na, wakitoka nje ya mji, aidha waende baharini au watokelezee kwenye ardhi ya israel ambako vifaru vipo, kwasababu Gaza imezungukwa.
 
Niwah kusema humu kwa mtoa mada mmoja ....watu wanachukulia kimihemuko ya kidini na skin color hii vita.. wakat wakubwa wa dunia wala hawako huko

Nikasema suluhisho la hii vita ni mpaka wakubwa waamue.. maana wote hao wanachagua upande kutokana na kuangalia watafaidikaje Arab league wote wataishia kutoa matamko.. ni waislam wenzao na ni waraab wenzao.. ila sababu kwa hao the likes of Saudia na iran.. wanaona they have more to loose wakiingia.. na hawana maslah ya moja kwa moja pale ..

Hao Misri, Syria, Iran (nazungumzia viongoz na wafanyabiashara wao) sio raia wa kawaida wa hizo Inchi.. wote wanajua wakishajitoa muhanga kuingia basi hawana maisha marefu kwenye uongozi..na watakosa kula
Mema Ya nchi Zao wakikumbuka ya Sadam
Na ghadafi.. wanapiga kimya

Huyo bashaar wa Syria aliponea chupuchupu kutolea na hapo ni sababu alikuwa anagombewa na wakubw awa Europe wawili.. la
Sivyo kama Mrusi angekuwa hana Maslah Syria zaman sasa hv Syria ni Iraq au Libya ingine

So Iran anaenda kimachale nia ya kuingia anayo ila desire ya kuendelea kula utamu wa kula mema ya nchi ni kubwa so anauma na kupuliza..

Misri utawala wa sasa hv ni puppet wa westerns.. same as Syria.. Jordan na hatak hata kuuguswa maana anajua Akijifanya kidomo ataletewa raman za karne ya kwanza aambiwe jiko la familia ya Musa ilikuwaga hapo pia yeye anapaswa kuchapa lapa..baadhi ya maeneo..

Raia wa kawaida wataandamana nawatapiganana wao kwa wao ila nothing will change

China na Urusi wote wanalaan ila sababu hawana maslah hawana haja ya kujitia hasara

Dunia ya sasa hv tutakusaidia tukiona fursa kwako kama hakuna ache ufe tu.. angalia somali na sudan wanavyochinjana..
Wakubwa wanauza silaha tu

Wakubwa wote maisha yao kuliana timing nani awe wa kwanza kufulia mwingine akamate usukan awe anatawala dunia.. Urusi hatak ya USSR yajirudie, china akiangalia Japan alikuwaga super power akamvimbia USA na Westerns nao anawatumikia anaona mh ngoja kwanza..
Popote ukisikia US yupo na washirika wake basi ogopa, watu hatari saaana hawa kwa akili.
 
Ukweli ni kwamba waarabu wameichoka HAMAS, wengi sasa wanataka maendeleo kwenye nchi zao, hawana muda na pumba za dini za vita vita kila wakati, kwa sasa mlichoanzisha pambaneni kukimaliza wenyewe.
Upo sahihi mkuu, waarabu wamechoka vita vya kipuuzi, mambo ya kukumbatia udini na kupambana na adui usiyemuweza ni upuuzi.
 
Unadhani Iran haja react mpaka sasa?Hivi unajua kinachoendelea huko shebaah farms kati ya IDF na hizbollah?Pole yako,Iran ana react kwa kumtumia Hizbollah kaa ujue hilo na hizhollah kapatiwa long range ballistic missiles tayari ambapo kama Hassan Nasrallah akisema wanaingia full scale war zitatumika.
Kwanini amtumie Hezbollah asiingie yeye kama yeye?
 
Yale mameli ya US na UK yaliyokwenda huko bahari ya mediteranian ni kwa ajili ya kumtuliza muarabu, ni kama mtu amekukaba huku akikuwekea kisu shingoni, huwezi kufurukuta.

Sasa hivyo ndivyo muarabu alivyo kwa sasa, yeyote akizingua tu hatoweza kubaki salama, hasahasa Iran. Ile mimeli si mchezo, haipo bure ile mimeli.
 
Tangu jeshi la IDF liweke vifaru vyake pembezoni mwa Gaza ikitishia kuingia ndani ya Gaza kuwasaka Hamas,Iran imekuwa ikitoa maonyo makali kwa Israel isithubutu kufanya hivyo kwani itakuwa ni kuvuka mstari mwekundu katika mzozo huo ikiashiria na wao wataingilia kati kupambana kuwatetea wapalestina.

Tangu Ijumaa iliyopita jeshi hilo La IDf limetangaza kuvusha vifaru vyake kuingia Gaza. Ijapokuwa vifaru hivyo vimekuwa vikipata upinzani mkali na kulazimika kurudi nyuma kutoka kwa Hamas, hata hivyo ni kweli vimevuka mpaka na vimeuvuka huo mstari mwekundu uliochorwa na Iran.

Kinyume na kurudisha mapigo kwa kasi Iran imeendelea kutoa matamko ya kubembeleza na kulalamika na kuonya zaidi kwa kusema wao wameambiwa wasiingilie vita hivyo lakini mbona Marekani inazidi kuiunga mkono Israel.

Uungaji mkono huo wa Marekani na washirika wake hasa UK ni kweli upo na uko kwa maneno na vitendo.Bado tu Iran inaendelea kushuhudisha watu kuwa hao walioamrisha wakae kimya wanavunja makubaliano.

Muda huo huo Israel ikiwa imevuka mpaka na ndege zinadondosha mabomu ikiwemo aina mpya ya Iron sitng, nchi kama Saudia zina ratiba ya kukutana na viongozi wa Marekani wiki ijayo kuzungumzia masuala ya Gaza na uwezekano wa kusitisha vita. Inawezekana wanachokusudia kukizungumza sio kusitishwa vita bali wana ajenda nyengine tofauti .

Hayo yote yakitokea Gaza, kule ukanda wa magharibi na mashariki, kiongozi wa PLO ndio kabisa amepiga kimya kama kwamba ni mgonjwa huku walowezi wa kiyahudi wakiwaua wapalestina na kuwafukuza kwenye majumba na mashamba yoa.
Sambamba na walowezi jeshi la IDF limekuwa likipiga kutoka angani kama linavyofanya kule Gaza.

Kuhusu yanayowakuta wapalestina wa upande huo,raisi Biden ametoa tamko jepesi la kutaka walowezi waache kuwapiga wapalestina na upande wa Shinbet, shirika la ujasusi la Israel wametoa matamko kama hayo bila kutaka jeshi la IDF kuacha mashambulizi yake.

Kila mmoja kati ya wale walioonekana kuwa wangekuwa watetezi wakali na wenye sababu za kufanya hivyo kwa wapalestina katika muda ambapo misaada yao ni ya lazima, watakuwa wana sababu zao ambazo hawajaweza kuzidhihirisha.Kubwa linalofanana kwa wote ni kuhofia madaraka na mipango yao kwa hofu kuwa Marekani na Israel zitawapiga au zitawavunjia mipango yao hiyo.

Kwa mfano Saudia wana mradi wa kuigeuza nchi hiyo kuwa pepo ya dunia ambao wasingependa urudi nyuma na hasa kwa vile wameshatumia gharama kubwa sana mpaka hapo walipofika.Watu watasemaje ikiwa miradi hiyo haitokamilika.

Wakati watu wanakufa kwa njaa na kiu Gaza, Misri imetoa sababu za kilemavu za kutokufikisha misaada Gaza ikiilaumu Israel wakati kumbe mpaka wa Rafah wala haujapakana na Israel, ni baina yake na Gaza tu na pia upekuzi wa malori ya misaada hufanyika kilomita 62 ndani ya Misri kabla ya hata kufika huko Rafah.

Iran kwa upande wake iko karibu kukamilisha kurutubisha silaha zake za nyuklia na sijui zikikamilika wanakusudia kumpiga nani.
Kimya cha Mahmoud Abbas na viongozi wenzake wa PLO ni ahadi ya kumilikishwa Palestina pamoja na Gaza kitu ambacho baada ya Israel kufanikiwa kuikamata Gaza kama watafanikiwa wala hakitotekelezwa.
Maelezo na sababu ni kama hizo kwa Syria na Jordan.Kila mmoja akiwa na hofu ya kitu fulani alichonacho mkononi.
Kilichobaki ni Hamas wapigane kwa nafsi zao kwa silaha hafifu walizonazo wakitegemea msaada wa Allah mwenye nguvu za kweli na ambaye rehema zake huenea kote na huja wakati usiotegemewa.
Wewe tulia tutawachakaza hao Israel hutawaona tena. Tumewawekea mtego sehemu. Watapigika kinyama....
 
Makundi kama haya ya meli yapo takribani manne kwa ajili ya kuitetea Israel, unadhani waarabu wajinga kuufyata mkia?
1200px-US_Navy_031130-N-3653A-002_USS_George_Washington_(CVN_73)_Carrier_Strike_Group_formatio...jpg
 
ramani yake haionyeshi kama zimetoka nje ya mji. wangekuwa na upenyo huo, wangeshatoroka wote. na, wakitoka nje ya mji, aidha waende baharini au watokelezee kwenye ardhi ya israel ambako vifaru vipo, kwasababu Gaza imezungukwa.
Kwani Israel wameizunguka Palestina yote!? Si wamelizunguka eneo la Gaza tu, sasa kivipi wakose kwa kwenda au iwe baharini pekee!?na mpango wa kutoroka nchi yao mbona hauingii akilini,ili waende wapi sasa!? Wanahamahama kwa lengo la kumpoteza adui na kutafuta nafasi nzuri yakumuangamiza.
 
nenda kwenye ramani kaangalia GAza imezungukwa na nini. kuna kaupenyo kadogo sana kusini kwenye Rafa ambako ukitoka unachomokea Misri, ila kote wamezungukwa na Israel na bahari.
 
nenda kwenye ramani kaangalia GAza imezungukwa na nini. kuna kaupenyo kadogo sana kusini kwenye Rafa ambako ukitoka unachomokea Misri, ila kote wamezungukwa na Israel na bahari.
Inasikitisha sana
 
Kwanini amtumie Hezbollah asiingie yeye kama yeye?
Kwanini ajihangaishe kuingia Moja kwa Moja ilhali hizbollah wapo????
Pia kumbuka kama akijihusisha Moja kwa Moja tension itakuwa kubwa maana Iran ni nchi inayojikongoja kwa economic sanctions pia inaandamwa na Wazungu Kila kukicha.
Na mlivyo waoga Hamas tu imewafanya mlete mameli yote hayo.
Usiwachukulie waarabu wadhaifu kwanza wameanza kumharibia Israel kidiplomasia.
Turkiye ,Jordan,Qatar,Saudia,Iraq,Pakistan, wote wamefunga balozi za Israel wakifuatiwa na Bolivia,Chile,Brazil,Colombia pia wamefuta mahusiano ya kidiplomasia na Israel.
Hiyo inakupa picha Gani kijana????
 
Makundi kama haya ya meli yapo takribani manne kwa ajili ya kuitetea Israel, unadhani waarabu wajinga kuufyata mkia?View attachment 2799948
Hizo meli zote kama Iran pekee ikaamua kutumia cruise missiles hazibaki ng'oo.
Na kwa taarifa Yako WAARABU HAWAJAUFYATA HOUTHI WA YEMENI WAMERUSHA DRONES NA MAKOMBORA KUELEKEA ISRAELI USS NAVY WAKAYADUNGUA IRAQ WAMERUSHA MAROKETI NA HIZBOLLAH LEO HII NAVYOKWAMBIA KALIPUA POST NNE ZA IDF MPAKANI NA LEBANON NA KUUA RAIA MMOJA WANAJESHI WATATU NA MAJERUHI KADHAA.
 
Kwanini ajihangaishe kuingia Moja kwa Moja ilhali hizbollah wapo????
Pia kumbuka kama akijihusisha Moja kwa Moja tension itakuwa kubwa maana Iran ni nchi inayojikongoja kwa economic sanctions pia inaandamwa na Wazungu Kila kukicha.
Na mlivyo waoga Hamas tu imewafanya mlete mameli yote hayo.
Usiwachukulie waarabu wadhaifu kwanza wameanza kumharibia Israel kidiplomasia.
Turkiye ,Jordan,Qatar,Saudia,Iraq,Pakistan, wote wamefunga balozi za Israel wakifuatiwa na Bolivia,Chile,Brazil,Colombia pia wamefuta mahusiano ya kidiplomasia na Israel.
Hiyo inakupa picha Gani kijana????
Nilidhani pana Taifa kubwa hata moja lililofunga ubalozi wake, kumbe ni hao tu.Netanyahu hana hata habari nao watajirudisha wenyewe.
 
Hizo meli zote kama Iran pekee ikaamua kutumia cruise missiles hazibaki ng'oo.
Na kwa taarifa Yako WAARABU HAWAJAUFYATA HOUTHI WA YEMENI WAMERUSHA DRONES NA MAKOMBORA KUELEKEA ISRAELI USS NAVY WAKAYADUNGUA IRAQ WAMERUSHA MAROKETI NA HIZBOLLAH LEO HII NAVYOKWAMBIA KALIPUA POST NNE ZA IDF MPAKANI NA LEBANON NA KUUA RAIA MMOJA WANAJESHI WATATU NA MAJERUHI KADHAA.

Imebidi nitabasamu tu hapo pa Iran akiamua [emoji4][emoji4]
 
Back
Top Bottom