Mstari mwekundu wa Iran umeshavukwa lakini bado wanatii amri

Mimi huwa nafuatilia maneno yao halafu napima na vitendo vyao.Nikiangalia naona maneno ni mengi na vitendo ni vichache na kinyume cha maneno.
Unavyoona wewe hapa ilipofika Jordan alipaswa kusema au kuchukua hatua ya kuvunja mkataba na kuacha mpaka wazi.Au unavyoona wewe Misri ni wa kulalamika kuwa watu wanakufa kwa njaa au ni kutoa tamko napeleka misaad na ukiizuia au kunipiga napambana na wewe.
Unajua kuwa upekuzi wa malori unafanyika ndani ya Misri na Rafah imepakana na Gaza na haikupakana na Israel.
 
Ndio maana zimepelekwa meli vita2 huko middle East kutoka USA.
Ndio kaka inajulikana kuna meli vita mbili na manowari moja ikiwa na askari maji zaidi ya elfu ishirini.Ila kaka hiyo Iran ioneni hivyo hivyo yeye ndiye aliyetia ugumu wa Russia kuanguka huko Ukraine kwa kumsaidia Russia silaha za makombora na Drones na ukumbuke USA alitoa msaada mkubwa tu huku Ukraine na haukufua dafu.
 
Syria naye anaweza kuwa muamuzi mzuri wa vita kwani kila siku vituo vyake na viwanja vya ndege vinapigwa na Israel na hajawahi kurusha makombora kutoka milima ya Golan kushushia Tel Aviv.Hii ingekuwa ni fursa kujibu mapigo kwa ajili ya Gaza na kwake mwenyewe.
 
Russia na Ukraine ni kama vita imefika ukingoni.
 

Hapo mwishoni hapo dah 😭😭😭
 

Naked Truth 👆👆👆
 
Hii Dunia duh! Ivi ya urusi na ukraini imeisha? Na Sudani ikoje? Na drc ikoje? Kiukweli Dunia inalewesha
 
Ukweli ni kwamba waarabu wameichoka HAMAS, wengi sasa wanataka maendeleo kwenye nchi zao, hawana muda na pumba za dini za vita vita kila wakati, kwa sasa mlichoanzisha pambaneni kukimaliza wenyewe.
Huwa wanaamini kwenye fujo sana. Nchi zao zimeshakuwa magofu mfano hai Libya.
Kitendo cha kuvamia, kuua raia na kuwateka raia kwenda nao Gaza, ni kitendo ambacho hakivumiliki.
 
Kwanini hao Palestina hawashinikizi HAMAS kuwaachia mateka wa Israel ili Israel iache kushambulia?

Na kwanini hawapambani na HAMAS wanaowaponza? Mbona ni kama wanawakumbatia?
 
Mstari mwekundu umevukwa?Yemen washajiunga, na Hezbollah wanajiunga Ijumaa rasmi
 
Mstari mwekundu umevukwa?Yemen washajiunga, na Hezbollah wanajiunga Ijumaa rasmi
Kama unazijua ratiba vizuri.Vipi Syria na Jordan.Na ni ipi ratiba ya Misri.
 
Iran anapigana ila huwezi kumuona.ukisikia Syria na Iraq American military base zinapigwa ni Iran. Yemen , hizbullah hao wote wanafadhiliwa na Iran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…