Mstari mwekundu wa Iran umeshavukwa lakini bado wanatii amri

Pengine ni kweli uyasemayo lakini nahisi utakuwa hujui kwamba Hamas wana njia za chini ya ardhi hapo Gaza zinazoweza kuwatoa nje ya mji.
 
nchi kama Saudia zina ratiba ya kukutana na viongozi wa Marekani wiki ijayo kuzungumzia masuala ya Gaza na uwezekano wa kusitisha vita. Inawezekana wanachokusudia kukizungumza sio kusitishwa vita bali wana ajenda nyengine tofauti .
Si walimkwepa Biden alipokwenda Israel!!
 
Pengine ni kweli uyasemayo lakini nahisi utakuwa hujui kwamba Hamas wana njia za chini ya ardhi hapo Gaza zinazoweza kuwatoa nje ya mji.
ramani yake haionyeshi kama zimetoka nje ya mji. wangekuwa na upenyo huo, wangeshatoroka wote. na, wakitoka nje ya mji, aidha waende baharini au watokelezee kwenye ardhi ya israel ambako vifaru vipo, kwasababu Gaza imezungukwa.
 
Popote ukisikia US yupo na washirika wake basi ogopa, watu hatari saaana hawa kwa akili.
 
Ukweli ni kwamba waarabu wameichoka HAMAS, wengi sasa wanataka maendeleo kwenye nchi zao, hawana muda na pumba za dini za vita vita kila wakati, kwa sasa mlichoanzisha pambaneni kukimaliza wenyewe.
Upo sahihi mkuu, waarabu wamechoka vita vya kipuuzi, mambo ya kukumbatia udini na kupambana na adui usiyemuweza ni upuuzi.
 
Kwanini amtumie Hezbollah asiingie yeye kama yeye?
 
Yale mameli ya US na UK yaliyokwenda huko bahari ya mediteranian ni kwa ajili ya kumtuliza muarabu, ni kama mtu amekukaba huku akikuwekea kisu shingoni, huwezi kufurukuta.

Sasa hivyo ndivyo muarabu alivyo kwa sasa, yeyote akizingua tu hatoweza kubaki salama, hasahasa Iran. Ile mimeli si mchezo, haipo bure ile mimeli.
 
Wewe tulia tutawachakaza hao Israel hutawaona tena. Tumewawekea mtego sehemu. Watapigika kinyama....
 
Makundi kama haya ya meli yapo takribani manne kwa ajili ya kuitetea Israel, unadhani waarabu wajinga kuufyata mkia?
 
ramani yake haionyeshi kama zimetoka nje ya mji. wangekuwa na upenyo huo, wangeshatoroka wote. na, wakitoka nje ya mji, aidha waende baharini au watokelezee kwenye ardhi ya israel ambako vifaru vipo, kwasababu Gaza imezungukwa.
Kwani Israel wameizunguka Palestina yote!? Si wamelizunguka eneo la Gaza tu, sasa kivipi wakose kwa kwenda au iwe baharini pekee!?na mpango wa kutoroka nchi yao mbona hauingii akilini,ili waende wapi sasa!? Wanahamahama kwa lengo la kumpoteza adui na kutafuta nafasi nzuri yakumuangamiza.
 
nenda kwenye ramani kaangalia GAza imezungukwa na nini. kuna kaupenyo kadogo sana kusini kwenye Rafa ambako ukitoka unachomokea Misri, ila kote wamezungukwa na Israel na bahari.
 
nenda kwenye ramani kaangalia GAza imezungukwa na nini. kuna kaupenyo kadogo sana kusini kwenye Rafa ambako ukitoka unachomokea Misri, ila kote wamezungukwa na Israel na bahari.
Inasikitisha sana
 
Kwanini amtumie Hezbollah asiingie yeye kama yeye?
Kwanini ajihangaishe kuingia Moja kwa Moja ilhali hizbollah wapo????
Pia kumbuka kama akijihusisha Moja kwa Moja tension itakuwa kubwa maana Iran ni nchi inayojikongoja kwa economic sanctions pia inaandamwa na Wazungu Kila kukicha.
Na mlivyo waoga Hamas tu imewafanya mlete mameli yote hayo.
Usiwachukulie waarabu wadhaifu kwanza wameanza kumharibia Israel kidiplomasia.
Turkiye ,Jordan,Qatar,Saudia,Iraq,Pakistan, wote wamefunga balozi za Israel wakifuatiwa na Bolivia,Chile,Brazil,Colombia pia wamefuta mahusiano ya kidiplomasia na Israel.
Hiyo inakupa picha Gani kijana????
 
Makundi kama haya ya meli yapo takribani manne kwa ajili ya kuitetea Israel, unadhani waarabu wajinga kuufyata mkia?View attachment 2799948
Hizo meli zote kama Iran pekee ikaamua kutumia cruise missiles hazibaki ng'oo.
Na kwa taarifa Yako WAARABU HAWAJAUFYATA HOUTHI WA YEMENI WAMERUSHA DRONES NA MAKOMBORA KUELEKEA ISRAELI USS NAVY WAKAYADUNGUA IRAQ WAMERUSHA MAROKETI NA HIZBOLLAH LEO HII NAVYOKWAMBIA KALIPUA POST NNE ZA IDF MPAKANI NA LEBANON NA KUUA RAIA MMOJA WANAJESHI WATATU NA MAJERUHI KADHAA.
 
Nilidhani pana Taifa kubwa hata moja lililofunga ubalozi wake, kumbe ni hao tu.Netanyahu hana hata habari nao watajirudisha wenyewe.
 

Imebidi nitabasamu tu hapo pa Iran akiamua [emoji4][emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…