Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Nikizinduka usingizini najikuta macho ni makavu sana (dry eyes). Ili niweze kuona inanibidi nisubiri kwa muda wa dakika Moja hivi ndio macho yanarudia hali yake ya unyevu. Huu ni ugonjwa gani na tiba yake ni nini?
 
nina tatizo la kubabuka uso, alaf una mabaka naeza paka mafuta hata mara kumi kwa cku shida n nn msaada plz yan uso kla mara kupauka @Dr Sajjad Fazel
 
nina tatizo la kubabuka uso, alaf una mabaka naeza paka mafuta hata mara kumi kwa cku shida n nn msaada plz yan uso kla mara kupauka @Dr Sajjad Fazel

Mkuu, samahani nilifikiri nishakujibu. Labada nilisahao kutuma lakini nilikuwa nishaandika jibu.
Ningekushauri upakae dawa hii kwa muda wa wiki moja; Sonaderm cream kila siku usiku unapolala.
Alafu, nipemajibu unaendeleaje.

Asante
 
Dr. Tatizo langu ni haemorroids/bawasili nitumie dawa gani niweze kuziondoa?

Unaweza kupakaa tube ya Anusol maeneo hayo yanayokusumbuwa kutwa mara mbili. Pia kula matunda na mboga mengi. Kunywa maji ya lita 3 au 4 kila siku. Fanya hivyo, alafu niambie unavyoendelea.

Asante.
 
Kuna jamaa yangu ameniadithia tatizo lake nikasema ngoja niulize.Inawezekana vp mtu kuwa mzima wa afya gafla amepata msichana amelala nae usiku kucha jogoo hasimami baadae akatafuta meingine jogoo akasimama kama kawaida kulikoni hapa dkt
 
Dr. Natoka kiasi kikubwa cha ute mweupe kama karatasi ukeni, hautoe harufu, nawashwa kiasi kidogo na sisikii maumivu. Nimepima UTI na fungus nimeambiwa sina mambukizi hayo. Ute huo huongezeka zaidi nikikaribia siku zangu. Ni ute mwingi mpaka nguo ya ndani inalowa sana. Huu ni mwaka wa tatu sasa kila nikipima wanasema hawaoni fungus.
 
Dr. Uso wangu una mafuta mengi sana mpaka natamani niyauze..

Nimejaribu kutumia cosmetics mbali mbali za kufanya skin kuwa dry lakini hazijasaidia..

Unanisaidiaje niweze kuondokana na hali hii?

Maanake nikiwa juani usoo una ng'aa kweli kama sentimila ya ISUZU na mimi sipendi mng'ao huo.
 
Back
Top Bottom