Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Fungua biashara ndogo isiyozidi nusu ya hela uliyonayo then isimamie mwenyewe... Utaona returns nzuri tuu....biashara zote in nzuri kikubwa ni usimamizi.
kweli mkuu huu ushauri ni mzuri kabisa, kama ulivyosema ni mwajiriwa itakuwa ngumu kusimamia biashara yako!
 
Hoho zinalipa zaidi,lakini hata pilipili mbuzi zinalipa sana

Ni PM no yako tuongelee jinsi ya kutafuta masoko nje ya nchi

Kuna mahali nilisikia siku hizi zile hoho zetu za kienyeji soko lake sio kubwa sana kama zile nyekundu
 
changamoto so far labda ni ku expand kupata wigo mkubwa zaidi wa wateja, kwani huwa nawakopesha wale ninaowajua tu, na siku wanayolipwa mshahara naijua hivyo nawabana wananilipa, either wanalipa principal+interest au wanalipa intetest tu kama mambo yao bado hayajatengamaa, interest sio kubwa ni 5% kwa siku 30, nikikopesha 100,000 nalipwa 5,000 baada ya siku 30 kama interest, nikopesha 10,000,000 yote napata 500,000 baada ya siku 30 kama interest

Ila kuwa makini mkuu hiyo kitu wakati mwingine inaharibu mahusiano kweli pale inapofika muda wadaiwa wanakwepa kulipa
 
Ila kuwa makini mkuu hiyo kitu wakati mwingine inaharibu mahusiano kweli pale inapofika muda wadaiwa wanakwepa kulipa
when i do business i mind it, it and only it, not my relationships, not my pride, not a woman, not my brothers not my sisters, its MY BUSINESS first
 
Mm ndugu yangu nakupa ushauti naamini mzuri kuliko yoooote uliipata.
Kama bado pesa unayo benk nakushauri 1.maliza mwezi Acha jazi ya kuajiriwa.
2. Tafuta mradi m1 kati ya bidaboda au bajaji au kicary usimamie mwenyewe. Huo usafiri ununue mwenyewe kwa pesa zako hizo.
3. Naamini pesa zitabaki weka benki bila ya riba. Maana riba haimzidishii mtu bali zinamrudisha mtu nyuma.
4. Tumia vizuri kilato chako bila kujinyima na bila kufuja. Zinazobakia endelea kuhifadhi benki.
5. Kwa mwenendo huo naaamini mtaji utaendelea kukua. Nakushauri tafuta kiwanja. Mdogo mdogo kama kampeni za magufuli mwishowe utajenga . Maisha murua kabisa.
 
Kaka daladala faida halisi baada ya gharama zote ni ngapi daladala ya route ipi?
Biashara iyo ya daladala co nzuri itakukost ujutie

Tafta kiwanja jenga hata vyumba vitatu zen pangisha ule faida tu akuna loss ambazo utapata
 
Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya
...maswali gani haya sasa....tumia hela bana....we vipi bana...kuna mambo mengi waweza kufanyia...ikiwemo kuto.mbea....sio jasho lako hilo...
 
Pesa milioni kumi kwa sasa haina thamani kiviile. Hiyo ni hela ya kununulia kigari kama Kirikuu au Kibaby walker cha Kiporte. Cha muhimu wekeza kwenye biashara ambayo itakuwa ni rahisi kui manage na kuisimamia kwa mbaaali. Mfano unaweza kuanzisha biashara ya kuuza simenti au na kisha pembeni fungua kiwanda cha kufyatua matofali. Hapo nadhani itatosha...
 
Njoo unifungulie salon ya kike maana nina kila kitu mfano madraya makopo ya dawa viti nk hela ya kukodishia flem ndo sina ni PM tuongee business serious brow salon ya kike inalipa sana istoshe nina Wateja wng
 
Mkuu nitafute, nikupeleke Bar yenye mademu wakali!
 
Kwa mfano ninunue boda boda 8 kwa bei ya jumla.. nifungue account say BOA bank. Kila nikipewa cash nadeposit huko.. Then cash inflow niwe nanunua boda boda moja kila mwezi. After six months si naweza kukopa na kununua boda boda nyiingi zaidi au!???
Dahh kaz kweli kweli!!!
Nahitaji kutulia
Utaratibu mzuri wa bodaboda ukishanunua mkabidhi mtu unaemfaham kwa maandishi na mpe target akuletee elf20 kila cku au lak na40 kwa wiki kwa mda wa miez minne au mitano utakuta umerudisha pesa yako na faida.akishamaliza bodaboda inakuwa yake we unanunua ingine.kufanya hvyo atakusumbua na atatunza pikipiki kipindi chote sbb ni yake.
 
Yas mimi mzee wang alikufa.. so aliacha nyumba nne.. Watoto tuko watatu; tukagawana kila mmoja akapata yake ile moja tukauza. Sasa kila mmoja alipata mil 16 hiv. Mimi nikaenda Kibaha nikanunua kiwanja nikajenga vyumba 8.

Wezangu wakaanzisha biashara... Ni mwaka wa tatu sasa wenye biashara zishakufa na wapo kwenye msoto... Mmoja kauza nyumba tuliogawana.. So nina experience mkuu.. Wewe wekeza tu kwenye ujenzi itakusaidia baadae..


Mkuu kwa 16m uliwezaje kujenga nyumvba 8.
 
Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya
Ni jambo jema kama maisha yako ya kila siku hayototegemea kwa haraka pesa ya urithi uliyopatiwa, kwa sababu biashara nyingi ufa kutokana na mambo matatu;
1. aina ya bidhaa uliyochagua kutoendana na mazingira
2. aina ya biashara unayofanya haiendani na mahitaji yako ( inachukua muda mrefu kurejesha faida)
3. uwezo wa kustahimili kipindi cha mpito ( mwanzoni biashara inaweza isiwe na matunda makubwa)

naamini umeshapata ushauri wa nini ufanye hii ni nyongeza tu
 
kwa ushauri wangu hiyo hela wekeza katika taasisi za kifedha za kukuza mtaji kama vile utt pesa yako itakuwa kuna mifuko mbalimbali ya kununua hisa kadri bei ya vipande inavyvo panda ndio unapata faida na kuna mfuko ambao unatoa gawio kila baada ya miezi mitatu kama utawekeza kuanzia milioni mbili na kuna gawio kila baada ya mwaka mmoja kama utawekeza tsh milioni moja kumbuka hela yako ukiamua kuichukua unaweza ukaichukua ukitaka vilevile kuna mfuko wa umoja unaweza kuanzia elfu kumi na utawekeza kadri kulingana na uwezo wako na unapata faida bei jinsi inavyopanda na vilevile unaweza ukakopa hizo hisa ndio dhamana yako.
 
Back
Top Bottom